Februari 16 Serikali ilisema umeme mwisho kukatika. Ulipo umeme upo?

Februari 16 Serikali ilisema umeme mwisho kukatika. Ulipo umeme upo?

Mzalendo07

Member
Joined
Feb 24, 2014
Posts
71
Reaction score
120
Nchi inaingozwa na kauli za uwongo bila kuhusisha wataalamu moja kwa moja kila kitu ni siasa

20240215_074150.jpg
 
waruhusu makampuni mengine yawekeze kama ilivyo kwenye makampuni ya simu

ila wanaogopa ya TTCL yasije kuikuta TANESCO

Tatizo ubabaishaji mwingi, kujiamini hakuna
 
Sehemu ulipo umeme upo? Waziri na mama alisema leo ndio mwisho wa mgao nchini.

Kimara hapa muda huu umeme umekatika, kuna mtu kanambia na Ubungo haupo

Nimeskia na Mbezi beach wamekata

Ulipo umeme upo?
 
Ukiwa mwanasiasa lazima uwe muongo tu.
watu wa hovyo sana hawa..
Kwangu wamekata tokea saa 1 asubuhi
 
Ulipo umeme upo? alisema leo ndo mwisho wa mgawo nchini

Kimara hapa muda huu umeme umekatika kuna mtu kanambia na ubungo haupo

Nimeskia na mbezi beach wamekata

Ulipo umeme upo?
Usipende sana kuwasikiliza au kuwaamini wanasiasa. Tangu umeambiwa mitambo ya umeme Rufiji itaanza kuwashwa January 2024, Treni za SGR itaanza safari zake January, 2024 na kila siku unaambiwa kuna meli zinashusha tani za sukari bandarini lakini ukija huku mtaani ndio kwanza sukari inazidi kupanda bei hadi 6,500 kwa kilo moja na bado haipatikani kirahisi hata kwa hiyo bei. Bado tu unaamini maneno ya wanasiasa? Au ni mpaka damu zitoke masikioni kama Kenge ndio uache kuawaamini wanasiasa?
 
Nilipo haupo toka sa 11 asubuhi, nimelala saa 7 usiku haukuwepo. Nahisi ulirudi usiku ukakaa kama masaa matatu yasiyozidi manne
 
Back
Top Bottom