Fedha na Mungu ndiyo mtetezi wako, jitahidi utafute kwa bidii hivyo vitu viwili

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
• Siku ukikamatwa kwa kosa la kuzurura mjini hapo mtetezi wako ni Mungu na fedha tu, vinginevyo utapewa hata kesi ya mauaji.

• Siku ukishikwa na ugonjwa barabara hapo mtetezi wako ni Mungu na pesa tu.

• Siku ukifukuzwa kazi ndipo utajua kuwa mtetezi wako ni pesa na Mungu tu.

• Siku utakapojibiwa majibu ya hovyo na sekretari huko utakapopeleka mavyeti kwa mabosi ndipo utajua kuwa mtetezi wako ni pesa na Mungu tu.

Jitahidi uwe navyo vyote au angalau kimoja.

Hao watu ambao unasema unao wa kutosha siku ukipatwa na la kupatwa hutawaona wakiambatana nawe mpaka mwisho.

• Siku Muhimbili wakikuambia mapafu yako Ili yakae sawa wape milioni 14 wayasafishe ndipo utajua kuwa mtetezi wako alipaswa awe Mungu na pesa pekee na sio hao marafiki zako wa kuongozana kwenye birthday party
 
Mungu kwanza kisha pesa kiasi maana chanzo cha maasi yote ulimwenguni ni chapaa.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
100%
 
Ukiwa na Mungu utapata vyote ikiwemo fedha.
 
Unamsema Chongolo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…