Fedha ya matumizi ya kawaida kuwa kubwa kuliko ya matumizi ya maendeleo ina maana gani?

Fedha ya matumizi ya kawaida kuwa kubwa kuliko ya matumizi ya maendeleo ina maana gani?

View attachment 1812485
BAJETI ina matumizi mengi ya kawaida kuliko Matumizi ya maendeleo ya nchi?

Hivyo kweli tutaendelea
nchi yetu kiuchumi? Bajeti aliyotoa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Mwigulu ili ipitishwe na Wabunge ni bajeti mbaya haifai kupitishwa Wabunge.

Tunamuomba Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu atueleze Shilingi Trilioni 11.93 zitatumika kwa ajili ya Matumizi yapi ya kawaida? Wakati pesa aliyoweka ya Maendeleo ni ndogo sana Shilingi Trilioni 1.02.

Maendeleo gani yatakayoweza kuifanikisha Tanzania kwa Pesa ya Shilingi Trilioni 1.02.? Hebu atufafanulie zaidi Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Mwigulu.
Matumizi ya kawaida = Mishahara
Matumizi ya maendeleo = barabara, madaraja n.k.
 
Labda ni kwa sababu bajeti ya mwaka Jana inayoisha mwaka huu fedha za maendeleo bado ziko kwenye mzunguko wa kazi zinazoendelea.....
 
We n mwehu tu.... kipindi cha JPM si ndy ilikuwa trlion 10 matumiz ya kawaida na trln 1 maendeleo
Sio kitu kibaya na cha kujenga chuki kwa Magufuli, na kwa hilo upo sawa kabisa, mtu halazimishwi kumpenda kiongozi.

Inapokuja suala la mkate wa Taifa hapa huhitaji ubabaishaji na chuki kuanalyse mahitaji na allocation of national resources.

Pesa ni za kwetu na maendeleo tunayataka au kutopata maendeleo ni better option? Kuwa na maendeleo ni suala la kuangalia kwa umakini lazima tuhakikishe mahitaji ya leo na kesho yanapatikana to be catered for.
 
Were mjinga recurrent expenditure ya namna hiyo kama ilivyoanishwa kwenye tovuti yao ni matumizi ya hovyo ambayo hayapaswi kubarikiwa na sisi walipa kodi!!!
Wewe ni pimbi lini uliwahi kuona bajeti ya maendeleo kubwa kuliko matumizi ya kuendesha serikali?

Au umezaliwa enzi za JK? Iko hivyo toka Uhuru
 
Sh. Trillion 10.48 kwaajiri ya deni la serikali/taifa... Hizi pesa ni nyingi Sana kulinganisha na ujumla wa bajeti kuu ya wizara zote....

Kama pesa zote hizo zinalipa deni ingekuwa deni linapungua kuliko sasa kuongezeka... Miaka mitatu tu ingepunguza nusu ya deni la taifa...

Hizi bajeti ni tarakimu tu tofauti na uhalisia...
Na bado mwendazake ameacha deni Tilioni 71,,kukopa sherehe kulipa matanga
 
Wwe Mungu amekuupa macho möawili huoni, amekupa masikio mawili husikii sasa nitakwambia kitu gani mpaka uniamini? Hilo deni la taifa ni 39t+ ulitaka alimalize kwa muda miaka 5? Inawekana kweli? Hawakuwea kulipa utawala uliopita hilo la deni la taifa ni 39t+ ataweza kulipa Marehemu Magufuli kwa muda wa miaka 5? Kama huna macho ya kuona aliyoyafanya Hayati Dr.Magufuli nyamaza kimya.

Yeye kwake deni limepaa kwa 31t, yaani 1/3 ya marais wengine wote wanne waliomtangulia. Sasa suala sio kusema sioni, bali sema mira fulani ndio iliyoleta hilo deni badala ya kuongea kama bendera fuata upepo.
 
Wizara ya fedha ndio inalipa mishahara na ruzuku ya Chadema usishangae matumizi ya kawaida kuwa makubwa hivyo bwashee!
mmh.....wanatumia over 12tr kwa wizara moja tu? Bajeti yetu yote ni around 30tr tu. Kuna kitu hakijawekwa sawa katika ripoti hiyo....ama na mwandishi au huko ilikotoka.
 
Kilaza
Inawezekana bajeti ya maendeleo ikategemea zaidi misaada ya wahisani kama ilivyokuwa huko nyuma!. Tunarudi enzi za kutembeza bakuli au kukopa zaidi!!.

Awamu ya nne kuna mkuu mmoja aliwahi kuwatonya watendaji wake kuwa huko Duniani kuna pesa nyingi sana hazina kazi, ili kuzipata unatakiwa ujue namna ya kuomba!. Tunaenda mbele na kinyumenyume kama kaa. 😳[emoji848]
 
Wewe ni pimbi lini uliwahi kuona bajeti ya maendeleo kubwa kuliko matumizi ya kuendesha serikali?

Au umezaliwa enzi za JK? Iko hivyo toka Uhuru

Nchi zote zisizokuwa na VISION ndio bajeti zake zinakuwa namna hiyo!!! Bora liende mradi watu wanapata mshahara na kujigawia posho!!!
 
Wewe unajuwa Bajeti ya Taifa Pesa zake zinatoka wapi? Kama sio Wizara ya Fedha? Na kama Bajeti ya Wizara ya fedha imeidhinisha pesa ndogo za Maendeleo ya nchi Pesa ya Shilingi Trilioni 1.02. Bajeti ya Taifa itakuwa imo humo humo ndani yake. Kwani Bajeti ya Taifa ipo chini ya Wizara ya Fedha.
Kila Wizara ina Bajeti yake, halafu kuna Bajeti Kuu ya Serikali yote, ambayo kwa miaka ya hivi sasa imefika 29-31tn/-
Suala la Matumizi ya kawaida kuwa juu kuliko matumizi ya Maendeleo naona miaka yote liko hivyo hasa kwa hela za ndani, kwani fedha za Maendeleo ni za mikopo yenye riba au masharti nafuu, misaada ya wahisani nk, hizo zote hufanya bajeti ya Maendeleo kupanda!
Kama mtu anatakwimu za miaka 5, atagundua iko hivyo kwa miaka yote.
 
Hata kama ni bajeti ya Wizara ya fedha , hizo trllion zote hizo kuwa matumizi ya kawaida ni matumizi gani hayo? Waziri atoe mchanganuo wa matumizi hayo ya kawaida!
Weka bajeti ya miaka mitano ya nyuma mfululizo tufanye ulinganifu, nje ya hapo tutasema ni chuki tu na mawazo hasi.
 
Inawezekana bajeti ya maendeleo ikategemea zaidi misaada ya wahisani kama ilivyokuwa huko nyuma!. Tunarudi enzi za kutembeza bakuli au kukopa zaidi!!.

Awamu ya nne kuna mkuu mmoja aliwahi kuwatonya watendaji wake kuwa huko Duniani kuna pesa nyingi sana hazina kazi, ili kuzipata unatakiwa ujue namna ya kuomba!. Tunaenda mbele na kinyumenyume kama kaa. 😳[emoji848]
Kwani mwaka jana bajeti si ilikua Trillion 13, lakini bajeti kuu ilitengwa Trillion 31 nyingi zikiwa za wahisani. Ni lini hatujaomba bakuli? Jambo dogo tu la petition ya ZZK kuzuia fedha kwa sababu ya issue za mimba wahisani walivyotaka kugoma mbona watu walitokwa na povu? Ni lini hatujawahi kutembeza bakuli? Tuacheni kudanganyana kwa vitu vilivyo bayana
 
Jmn msilaumu haraka haraka kwanza

wizara ya fedha ndo kuna Benki Kuu humo na malipo ya deni la Taifa

labda tupate mchanganuo na kulinganisha pia na mwaka jana

mwenye taarifa kamili aweke
 
Nchi hii ina shida!! Elimu Elimu Elimu!! Mleta mada, ni kawaida kuwa na matumizi ya juu kuliko matumizi kwa ajili ya maendeleo!! Angalia hata mshahara wake, ni kiasi gani kinakwenda kwenye chakula, nyumba, usafiri, mavazi, matibabu, starehe halafu linganisha na unasevu kiasi gani. Ukiweza kusevu zaidi ya 20% ya mshahara wako kwa ajili ya maendeleo kila mwezi - wewe ni mwamba.

Sio kila jambo kuwa mnalipinga - wizara ya fedha maendeleo kwake inaweza kuwa ni kutoa mafunzo, kujenga office mpya, kuongeza wafanyakazi, kuweka mifumo mipya. Usielewe maendeleo kupitia ufahamu wako wa barabara, hospitali, nk (hizo ni wizara nyingine). Unachoweza kusema ni kwanini matumizi ya kawaida yawe makubwa!!
 
Kwani mwaka jana bajeti si ilikua Trillion 13, lakini bajeti kuu ilitengwa Trillion 31 nyingi zikiwa za wahisani. Ni lini hatujaomba bakuli? Jambo dogo tu la petition ya ZZK kuzuia fedha kwa sababu ya issue za mimba wahisani walivyotaka kugoma mbona watu walitokwa na povu? Ni lini hatujawahi kutembeza bakuli? Tuacheni kudanganyana kwa vitu vilivyo bayana
Kwa hiyo wewe unaona ni sawa bajeti zetu ziendelee kutegemea wahisani? Hata kama mwaka jana ilikuwa tegemezi,kwa maoni yako ni halali kutembeza bakuli? Kama kuna udanganyifu unaendelea, ni dhambi kwa mlipakodi kuonyesha wasiwasi wake kuhusu mwenendo wa matumizi ya Serikali?.
 
New order kafafanua vizuri. Msome na umuelewe.
Hoja nyingine ambayo ni upotoshaji ni kuonekana kana kwamba jambo la matumizi ya kawaida ni jipya huko nyuma halikuwahi kutokea, kitu ambacho si kweli.
 
New order kafafanua vizuri. Msome na umuelewe.
Hoja nyingine ambayo ni upotoshaji ni kuonekana kana kwamba jambo la matumizi ya kawaida ni jipya huko nyuma halikuwahi kutokea, kitu ambacho si kweli.
Maswali yangu nimeyealekeza kwako kwa sababu wewe ndie uliyeninukuu kwenye hoja hii, New Order ana mawazo yake, siamini kuwa anawaza kwa niaba yako, wewe binafsi una mawazo gani kwenye hili?..,au ni kuunga mkono alichosema mtu mwingine?
 
Ina maana beberu mweusi ni mwizi kuliko beberu mweupe. Watu wanajilipa posho kwa kufanya kazi walizoajiriwa kufanya, OVYO

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Back
Top Bottom