Ezekiel Njalla
New Member
- Jun 3, 2024
- 4
- 3
Shule za serikali zimefungwa tangu mwishoni wa wiki iliyopita tarehe 31/5/2024.
Waalimu tulijaza Ankara za fedha za nauli ya likizo hii mapema sana na kuziwasilisha kwa wahusika ofisi Halmashauri ya Wilaya ya Magu kabla shule hazijafungwa; tukitarajia kwamba malipo yangefanyika mapema au mara baada ya shule kufungwa ili waalimu waweze kusafiri kwa wakati ndani ya siku za likizo.
Mpaka Juni 03; 2024 fedha ya likizo ilikuwa haijalipwa kwa wahusika; tatizo liko wapi?
Au mnataka kutulipa likizo ikikaribia kwisha kama mlivyofanya likizo iliyopita?
Mkurugenzi tusaidie tupate fedha zetu za nauli ili twende safari zetu ndani ya siku za likizo ambazo zinayoyoma.
Mwishowe zitaanza hadithi za mfumo umegoma, mtaanza kusema fedha hazishuki kwa sababu mfumo umefungwa kuelekea mwaka mpya wa fedha unaoanza tarehe 01/7/2024.
Wako katika ujenzi wa Taifa;
Mwalimu EZEKIEL NJALLA.