KERO Fedha za nauli ya likizo kwa waalimu inalipwa lini Magu DC?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Pesa yao iliwe na maofisa wao halafu wavute subira!! Mchezo huu mpaka lini? Mbona wakati wa aliyekuwa DED Magu LUTENGANO MWALWIBA mambo haya hayakuwepo? Hata kama yalikuwepo ilikuwa kwa kiasi kinachovumilika, ila siyo sasa!!
Mambo ya serikali ndivyo yalivyo...


Cc: Mahondaw
 
Huku geita wilaya ya nyang'hwale mpaka sasa kimya yani hawa maafsa watafika mbinguni wamechoka yani hela ya likizo inakuwa kama hisani.
Wakakati ni haki yetu yani hawa mbwa tungekuwa na uwezo wa kuwacharaza mboko.wangekula mboko mpaka basi.
 
Hili ni janga sio huko tu Namtumbo, newala mambo ni hayo hayo tu
 
Hili ni jukwaa gani?

Leo ndio mara yangu ya Kwanza kuingia jukwaa hili la majungu.

Kwan nyie hamfaham kwamba zoezi la PEPMIS limevuruga ratiba nyingi ofisi ya DEO?
 
Hili ni jukwaa gani?

Leo ndio mara yangu ya Kwanza kuingia jukwaa hili la majungu.

Kwan nyie hamfaham kwamba zoezi la PEPMIS limevuruga ratiba nyingi ofisi ya DEO?
Una hakika na usemayo kwamba malalamiko yanayotolewa ni majungu?
Mchezo wa kuchelewesha kulipa fedha za likizo kwa waalimu imekuwa ni tabia ya Halmashauri ya Magu DC hata kabla ya mfumo wa PEPMIS.
Mpaka wamenyung'unywa kwenye mitandao ya kijamii ndio wameamua kuwalipa waalimu fedha zao za likizo; juzi Jumatatu 09/6/2024 ndio wameachia fedha hizo, zaidi ya wiki moja baada ya shule kufungwa; kwa nini wakati waalimu walishawasilisha ankara za madai ya nauli zao mapema sana kabla ya shule kufungwa na fedha hizo zipo kwenye Kasma ya Other Charges (OC) ya Halmashauri?
Walikuwa wanazifanyia biashara ya kununulia mpunga au kukopesha kama anavyofanya Afisa Taaluma Johari Mwasha?
Waache kukandamiza haki za waalimu; wawape stahiki zao kwa wakati.
Naibu Katibu Mkuu Charles MSONDE; chondechonde, wang'oe Johari Mwasha na Jack Buhatwa hapa idarani; wanaumiza sana waalimu; maafisa hao ni perpetrators wa uonevu na rushwa!!
Asante sana Mwl. Ezekiel Njalla kwa kuvunja ukimya na kuwachora hao watu mtandaoni; usiogope hakuna atakayekudhuru maana unasimamia haki ukiwa kama kiongozi.
Mwl. Njalla una degree ya education; unafaa hata kuwa Afisa Taaluma hapo Elimu Msingi Wilayani.
Wapelekeni Johari na Buhatwa wakafundishe wasiendeleze uonevu wao na rushwa; mbona maofisa wengine wanarudishwa madarasani?
 
Vip Dec huko Magu Dc

Malalamiko ni hayo hayo au wamejirekebisha?
 
Roga gido hao
 
Roga gido hao
 
Wasomeeni dua mbaya hao wote wanaowatesa hakuna namna
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…