Fedha zilizokuwa katika akaunti maalumu ya IPTL (Tegeta Escrow account), ni mali ya umma

Fedha zilizokuwa katika akaunti maalumu ya IPTL (Tegeta Escrow account), ni mali ya umma

Utakuwa unafaidi "matunda" ya nchi wewe kama Prince Rizmoko

Mkuu hakuna haja ya sisi kugombana ktk mitandao bila sababu, wanasiasa mama yao ni mmoja, hawa wanaoitwa wakombozi wa nchi, hawajachukua madaraka, fuso used 600M, wanajikopesha 160M, na mengineyo, je wakichukua madaraka si itakuwa balaa?
 
Hao jamaa ni wajinga sana, wana lialia wakati wanajua kuwa tanesco ilikuwa inalipa deni la huduma ya umeme kwenye escrow account ili wale shareholders waliokuwa na kesi mahakamani waelewane kwanza ili hizo pesa zilipwe kwao,.....
 
Kwa mara nyingine serikali kupitia viongozi na watendaji wake akiwamo Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), wamedai kwamba kiasi cha Dola za Marekani milioni 250 zilizopaswa kuendelea kuwapo katika ‘Tegeta Escrow Account’ si mali ya serikali na hivyo si mali ya umma. Akaunti hiyo ilifunguliwa na serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) pamoja na kampuni ya Independent Power Limited (IPTL).

Kwa bahati mbaya sana viongozi wa serikali wamekuwa wakiendelea kurudia kuueneza huo uongo kwamba fedha hizo si mali ya umma. Inasikitisha pia kwamba vyombo vya habari vimekuwa navyo vikibeba na kusambaza huo uongo bila kuhoji na kuchunguza. Inashangaza sana pia asasi za kiraia nazo zimekaa kimya. Inatisha na kushangaa tena kuona wapinzani wakimwachia suala hili Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, pekee wakati mapambano dhidi ya rushwa ni ajenda kuu ya wapinzani. Kafulila amekuwa akiendelea kuhoji suala hilo bungeni peke yake bila kupata kuungwa mkono na kupewa msaada wa aina yoyote kutoka kwa wenzake wa kambi ya upinzani bungeni.

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ilielekeza kuwapo kwa ukaguzi maalumu kwenye akaunti hiyo ya Tegeta escrow account iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kuwa ndani yake kulikuwapo fedha za umma. PAC haina sababu yoyote ya kufuatilia fedha za watu binafsi. Mwaka 2009 iliyokuwa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) ilitoa maelekezo kwa BoT kutothubutu kutoa fedha hizo. Agizo hilo la POAC lilitokana na sababu kwamba fedha hizo zilikuwa ndani ya hesabu za Tanesco.

Akaunti ya ‘Tegeta escrow’ ilifunguliwa kutokana na kuwapo kutoelewana kuhusiana na gharama halisi na halali za umeme unaozalishwa na IPTL na kuuzwa kwa TANESCO. Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa (ICSID) katika uamuzi wake wa Februari, 2014 ilitoa hukumu kuonyesha kwamba Tanesco walitozwa kiwango cha juu zaidi ya kilichopaswa kulipwa kwa IPTL. Kwa uamuzi huo ni dhahiri kwamba fedha zilizokuwa zimehifadiwa kwenye akaunti hiyo maalumu ya escrow zilipaswa kugawanywa kwa IPTL na Tanesco baada ya hesabu kufanyiwa marekebisho upya kwa viwango halali.

Hesabu za mwaka wa fedha ulioishia Disemba 2012 za Tanesco zinaonyesha wazi kwamba fedha hizo ni mali ya shirika hilo la umma linalomilikiwa na serikali kwa asilimia mia moja. Fedha za kampuni ni suala la kisheria kama inavyobainishwa katika sheria ya kampuni ya mwaka 2002.

Kwa maelezo hayo na hoja hizo, inakuaje serikali ianze kudai kwamba fedha hizo si mali ya umma? Hivi inawezekanaje kwa fedha za mtu binafsi zikaingizwa katika hesabu za shirika la umma linalomilikiwa na serikali kwa asilimia 100? Ni lini fedha hizo zimekoma kuwa za umma? Je ni baada ya baadhi ya watendaji wa serikali kula njama za kuzichukua fedha hizo kwa kushirikiana na ‘mwekezaji’ aliyechafuka kwa ufisadi duniani?

Serikali inadanganya waziwazi kudai kwamba fedha hizo si mali ya umma. Umma una haki ya kukumbushwa kwamba madai hayo yalitolewa pia katika lile sakata la ufisadi maarufu wa EPA unaofanana kwa kila hali na huu wa sasa wa ‘Tegeta Escrow’.

Hoja nyingine ni kwamba, Mbunge Kafulila alisema kwamba Jaji Utamwa wa Mahakama Kuu ya Tanzania hakutoa uamuzi wa kuchukuliwa fedha kutoka akaunti ya ‘Tegeta Escrow’. Nimepitia kwa makini hukumu ya Jaji Utamwa na kubaini kwamba hakuna popote alipotaja akaunti ya ‘Escrow’. Hata hivyo, nilipopitia muhstasari wa kikao kati ya TANESCO, IPTL na Wizara ya Nishati na Madini, ndipo kwa mara ya kwanza nikakuta wametafsiri uamuzi wa mahakama wakidai kwamba fedha zote za ‘Tegeta Escrow’ zipewe kampuni ya PAP (inamilikiwa kwa asilimia 50 na Harbinder Singh na 50% na Simba Trust iliyosajiliwa Australia). Hiki ndicho kikao kilichofanya maamuzi ya kuiba na kugawana wenyewe fedha hizo (Hukumu ya Jaji Utamwa na muhstasari wa kikao vinaambatanishwa).

Wote waliohudhuria kikao hicho kilichojipa mamlaka ya kutafsiri hukumu ya Mahakama Kuu, wanapaswa kuchunguzwa na kufikishwa mahakamani kwa mujibu wa sheria zilizopo. Inawezekana vipi uamuzi wa mahakama ukatafsiriwa na kikao cha Wizara? Muhstasari wa kikao hicho ndio uliowasilishwa Benki Kuu (BoT) kuhalalisha madai kwamba fedha hizo lazima zitolewa kutoka akaunti ya Escrow.

Fedha zinazohusiana na akaunti ya Escrow ni Dola za Marekani milioni 250, katia ya hizo Dola milioni 122 zilizokuwa BoT zimeshatolewa na kiasi kilichosalia Dola milioni 128 zitalipwa na Tanesco kutokana na fedha zake kwa madai ya kushindwa kulipa kwa wakati. Fedha zilizolipwa ni zile ambazo zimetoka Wizara ya Nishati na Madini ambayo kisheria ndio walipaswa kulipia gharama za uzalishaji umeme (capacity charge) fedha zilizotoka kwa walipa kodi.

Ikumbukwe kwamba uhamishaji wa asilimia 70 ya hisa za IPTL kwenda PAP umeambatana na nyaraka za kughushi kutokana na kutokuwepo kabisa kwa uthibitisho wa cheti halisi cha hisa (share certificate) kutoka kampuni ya Mechmar kwenda kampuni ya Piperlink. Nyaraka za TRA zinaonyesha kwamba hisa hizo (70%) ziliuzwa kwa Shilingi za Kitanzania milioni sita (6) tu. Na bado hakuna ushahidi kuonyesha kwamba uhamishaji huo wa hisa ulipata baraka za mamlaka husika kama inavyotakiwa na sheria za nchi.

Wakati huyo anayejiita mmiliki mpya wa IPTL aliposaini mkataba wa kuchukua fedha kutoka akaunti ya Escrow zilizokuwapo BoT, hakuwa mmiliki halali kisheria kwani kodi ililipwa siku moja baada ya wao kupokea fedha kutoka BoT. Sheria inataka kutolewa kwa cheti na Kamishna wa TRA kama uthibitisho kwamba kodi yote imelipwa ipasavyo (Sheria ya Fedha ya 2012 kifungu cha 29).

Ni nani wamiliki wengine wa kampuni ya PAP? Uchunguzi ni muhimu ukawalenga vigogo na wanasiasa wakubwa wakiwamo watendaji waandamizi wa Wizara ya Nishati na Madini.

Inapaswa tutafakari kuona kwamba Harbinder Singh aliyechukua fedha za Escrow, anamiliki vitalu vya mafuta na gesi kupitia kampuni iitwayo HydroTanz ambayo nayo imesajiliwa nchini Australia, ikiwa na anwani sawa na ya kampuni ya Simba Trust. Kitalu hicho cha mafuta kinaitwa ‘Mnazi Bay North’, jirani kabisa na ugunduzi mkubwa wa hivi karibuni mkoani Mtwara.

Tunatarajia kwamba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), atafichua ukweli wa sakata hili na TAKUKURU itawafikisha mahakamani wahusika bila kujali nyadhifa zao serikalini.

Kauli ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, kwamba kuna watu waliokula rushwa na kwamba nyaraka zinazotajwa ni karatasi za kuuzia vitumbua, ni kauli zenye kuonyesha kutapatapa kwa watendaji serikalini. Hakuna hata mahali pamoja ambapo nimemtaja mtu kuwa ni mwizi zaidi ya kuwasilisha hoja zinazohitaji majibu mwafaka na si matusi, vitisho na tuhuma za kuzusha. Nyaraka za TRA haziwezi kuwa za kufungua maandazi kama ambavyo hukumu ya Jaji wa Mahakama Kuu haiwezi kuwa karatasi za kufungia maandazi na badala yake ni nyaraka halali zinazohitaji maelezo kutoka kwa viongozi na watendaji wa serikali badala ya kuropoka na kuporomosha matusi.

Hali kadhalika, Bunge lina kila sababu kupitia sheria yake ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kulinda hadhi yake kutoka kwa watendaji kama Maswi ambao wanatoa matamshi ya kuonyesha kwamba chombo hicho ni chombo cha watu wasiofaa na kwamba watu wanaofaa wanazungumza nje ya Bunge. Maswi na wengine kama wana ushahidi wa rushwa dhidi ya mbunge ama yeyote hawapaswi kupayuka ovyo bali kwa nafasi zao wanaweza kuwasiliana na vyombo vya dola kama TAKUKURU na polisi ili wachunguze na kuchukua hatua kama ambavyo vinawachunguza wao.

Kauli ya Maswi kwamba “wanaume” hawazungumzi ndani ya Bunge si tu udhalilishaji wa chombo hicho bali pia inaashiria ugonjwa wa mfumo dume uliotawala miongoni mwa viongozi wetu kwa maana kwamba wanaume ndio wenye hadhi, uwezo na heshima na wanawake ni dhaifu na wasiostahili heshima. Tufumbue macho tuone na tuondoe hisia binafsi zenye kubebwa na itikadi, chuki na misimamo yetu ya kisiasa. Tuwe wazalendo ili tuweze kusimamia utaifa.

Zitto Kabwe

ningependa kuona maoni ya FaizaFoxy .... je hapa Mheshimiwa Zitto yuko sahihi au kachemsha?
 
Last edited by a moderator:
Liko Tatizo....leo jioni niliwasikiliza sana Kafulira na Zitto kuhusu ac ya tegeta escrow. Wanamaelezo mazuri lakini hawathubutu kutaja kama ni serikali ya ccm na wanaccm wenyeewe ndo changizo kubwa la ufisadi kiasi hiki!
 
Hizo pesa za watoa huduma (service providers), malipo yao halali kwa huduma waliyotoa kama ilivyo kwenye mikataba yao ya kutoa huduma hiyo.

Zilikuwa public funds kabla hazijalipwa na mradi zimeshakusudiwa kulipwa watoa huduma na kupelekwa escrow account zimeshakuwa si public funds tena.

KUMBUKA.

Hivi hizi hela zilienda huko kwa sababu ya Ugomvi wa share Holders ? au Ugomvi wa IPTL na Tanesco kuhusu gharama za Umeme?
 
Ningeshauri tuingie msituni kuikomboa hii nchi kutoka mikononi mwa mkoloni mweusi kwani kwa ujinga wa waTz (sio upole/upendo) na akili ya CCM (eg. bi Asha Bakari) wamejipanga kuhakikisha nchi haichukuliwi kwa kipande cha karatasi

Ndugu yangu wewe ulitegemea Mwigulu apelekwe pale kimchezo?Hiyo ndio Kazi iliyompeleka pale.
 
Hoja nzuri na makini kutoka kwa Zitto.Pia ni vibaya kutanguliza lawama kwa upinzani kuwa umemuachia hili suala Kafulila pekee!

John Mnyika ameliongelea hili ndani na nje ya Bunge mara nyingi.Lilikuwepo pia kwenye hotuba yake kwa niaba ya kambi ya upinzani.Yeye na Kafulila wamewasilisha ushahidi kwa spika kuhusiana na jambo hilohilo.

Muda mwingine ni vizuri kuachana na haya mawazo ya kibinafsi na umimi au "usisi wa Kigoma".Zitto asijitenge na kambi ya upinzani pale maslahi ya taifa yanapolindwa hata na watu asiowapenda.
 
ningependa kuona maoni ya FaizaFoxy .... je hapa Mheshimiwa Zitto yuko sahihi au kachemsha?

Hapo Zitto anaongelea Tax, tena ya Capital gain.

Zitto anaelewa sana kuhusu Tax evasion na Tax avoidance lakini hilo anajifanya kama halijui. Ananshangaza!

Hapo jamaa hawakufanya Tax evasion hapo ni simply Tax avoidance, kisheria.

Hakuna ujanja hapo, kama hawakufanya evasion, walichofanya "avoidance" ni halali kabisa.

Zitto anachoshindwa kueleza ni kuwa IPTL ilikuwa na mgogoro na kampuni ya Kitanzania, kaingia Singasinga kaiona opportunity na kajuwa vipi atatatuwa huo mgogoro, kaongea nao wamekubaliana, kawanunua, kawalipa, kavuta fedha walizokuwa walipwe wao.

Kinachofata hapo ni uhalali wa tax na ndio anauongelea Zitto, kachimbuwa kakuta hakuna tax evasion bali kuna tax avoidance ambayo kisheria ni halali, cha kushangaza hapo hagusii kabisa.

Sijui msichokielewa anachoongelea Zitto zaidi ya hicho ni nini?

Nadhani, Zitto angekuwa kidogo mjanja asingeongelea hilo la kampuni kuuzwa million 6, unless anajuwa anachokifanya ila anataka ku divert msimamo, kuna kila uwezekano na yeye kavuta au anataka kuvuta amma kwa Singa amma kwa IPTL amma kwa huyo Mtanzania mwingine ambae hatajwi sana humu, amma kisha vuta kwa mmoja wao, lakini yeye huyo Mtanzania ndio master-mind wa huu mkorogano na Zitto anajuwa sana hilo.

Hapo sasa hivi kuna kila mtu kutaka kuvuta kwa Singa kwa kupiga makelele, kwa sababu hapo ndio where the buck stopped.

My Take:
Nasema huyo Mtanzania ni mastermind kwa sababu yeye alifikiri akiwabana sana IPTL watakubali yaishe wachukuwe fedha wagawane halafu mitambo yote atabaki nayo yeye aanze kuchuma peke yake kiulaini.

Bahati nzuri au mbaya, Singa kaliona hilo akaingia kati na kuna kila sababu kakubaliana na IPTL kuwa wataumizwa, yeye ana njia mbadala watakuwa ni win win situation, pesa watapata na mitambo haitopotea na wamuamini yeye, na ndicho kilichofanyika.

Hapo aliyeumia ni Mtanzania mwenzetu, tena si kaumia kwa kuwa hajapata faida ya bure, la hasha, faida kapata ya bure tena kubwa sana, kwani yeye hajatia fedha yake katika hili sakata, yeye alikuwa kama godfather tu wa ku-facilitate mambo ndani ya Tanzania. Ndiyo norm kwa biashara zote kubwa duniani.

Alichoumia ni pale alipotaka kubana mpaka mitambo yote ibaki kwake. Kataka kula kiharamu zaidi, ndipo Singa alipoingia na ku rescue.

Sasa, Mbonde kuona hivyo ni lazima apigane, kwani kwa sasa fedha ya kuwalisha wapayukaji hovyo kama akina Tumbili anayo, na afanye nini zaidi? anachofanya ni "kama kukosa tukose wote", lakini amechelewa jamvini karamu imeshaliwa.

Mwisho wa siku, kisheria ataibuka Singa kidedea, labda afanyiwe umafia. Na Singa si mdogo huyo, Tanzania anaijuwa juu chini, kaishi sana pande za Iringa, kama kuna mtu anaikumbuka RCC Iringa, basi ni hao akina Singa, si wageni kabisa Tanzania hii.

Mengine yote ni kubwabwaja, porojo na kuhororoja, kuna mshiko wa watu kunyamazishwa na ndiyo maana unasikia kelele.

Hakuna wizi hapo wa mali ya umma kisheria, kuna "opportunity" na Watanzania kama ujuavyo ni ma "opportunists" kama fisi wanavyongoja mifupa au makopangola wanavyoona mzoga, hawachelewi! ndicho kilichopo.

Usione vinaelea vimeundwa.
 
Hivi hizi hela zilienda huko kwa sababu ya Ugomvi wa share Holders ? au Ugomvi wa IPTL na Tanesco kuhusu gharama za Umeme?

It doesn't matter ni ugomvi upi, kama ni wa Tanesco na IPTL basi umeisha, kama ni ma shareholders pia umeisha.

Post ya juu hapo #50 nimeelezea hili sakata likoje.

Wajinga ndio waliwao.
 
Hapa naona Zitto analazimishwa kuungwa mkono na upinzani wakati yeye huwa hapendi kuungana wapinzanj wenzake kwani atawauzi ccm au ccm hawatamsifia. Ukipenda kujitenga na kujiona msomi na mbinafsi endelea mwenyewe na hao watakaokuunga mkono. Zitto akumbuke yeye ndio sehemu ya kuuvunja upinzani nguvu kwa kujifanya msomi, kuleta mawazo ya ukabila sijui ukanda huku akipata sifa toka ccm na kuvimba kichwa, leo inakuwaje tena kutaka msaada toka upinzani hata kama ni hoja yenye manufaa kwa wananchi?
 
Hapo Zitto anaongelea Tax, tena ya Capital gain.

Zitto anaelewa sana kuhusu Tax evasion na Tax avoidance lakini hilo anajifanya kama halijui. Ananshangaza!

Hapo jamaa hawakufanya Tax evasion hapo ni simply Tax avoidance, kisheria.

Hakuna ujanja hapo, kama hawakufanya evasion ni halali kabisa.

Zitto anachoshindwa kueleza ni kuwa IPTL ilikuwa na mgogoro na kampuni ya Kitanzania, kaingia Singasinga kaiona opportunity na kajuwa vipi atatatuwa huo mgogoro, kaongea nao wamekubalina kawanunua kawalipa, kavuta fedha walizokuwa walipwe wao.

Kinachofata hapo ni uhalali wa tx na ndio anauongelea Zitto, kachimbuwa kakuta hakuna tzx evasion kuna tax avoidance ambayo kisheria ni halali.

Sijui msichokielewa anachoongelea Zitto zaidi ya hicho ni nini?

Nadhani, Zitto angekuwa kidogo mjanja asingeongelea hilo la kampuni kuuzwa million 6, unless anajuwa anachokifanya ila anataka ku divert msimamo, kuna kila uwezekano na yeye kavuta au anataka kuvuta kwa singa na IPTL na huyoMtanzania mwingine ambae hatajwi sana humu, lakini yeye ndio master-mind wa huu mkorogano.

Hapo sasa hivi kuna kila mtu kutaka kuvuta kwa Singa kwa kupiga makelele.

My Take:
Nasema huyo Mtanzania ni mastemind kwa sababu yeye alifikiri akiwabana sana IPTL watakubali yaishe wachukuwe fedha wagawane halafu mitambo yote atabaki nayo yeye aanze kuchuma peke yake kiulaini.

Bahati nzuri au mbaya, Singa kaliona hilo akaingia kati na kuna kila sababu kakubaliana na IPTL kuwa wataumizwa, yeye ana njia mbadala watakuwa ni win win situation, pesa watapata na mitambo haitopotea na wamuamini yeye, na ndicho kilichofanyika.

Hapo aliyeumia ni Mtanzania mwenzetu, tena si kaumia kwa kuwa hajapata faida ya bure, la hasha, faida kapata ya bure tena kubwa sana, kwani yeye hajatia fedha yake katika hili sakata, yeye alikuwa kama godfather tu waku facilitate mambo ndani ya Tanzania. Ndiyo norm kwa biashara zote kubwa duniani.

Alichoumia ni pale alipotaka kubana moaka mitambo yote ibaki kwake. Kataka kula kiharamu zaidi, ndipo Singa alipoingia na ku rescue.

Sasa, Mbnde kuona hivyo ni lazima apigane, kwani kwa sasa fedha ya kuwalisha wapayukaji hovyo kama akina Tumbili anayo, na afanye nini zaidi? anachofanya kama kukosa tukose wote, lakini amechelewa jamvini karamu imeshaliwa.

Mwisho wa siku, kisheria ataibuka Singa kidedea, labda afanyiwe umafia. Na Singa si mdogo huyo, Tanzania anaijuwa juu chini, kaishi sana pande za Iringa, kama kuna mtu anaikumbuka RCC Iringa, basi ni hao akina Singa si wageni kabisa Tanzania hii.

Mengine yote ni kubwabwaja, porojo na kuhororoja, kuna mshiko wa watu kunyamazishwa na ndiyo maana unasikia kelele.

Hakuna wizi hapo wa mali ya umma kisheria, kuna "opportunity" na Watanzania kama ujuavyo ni ma "opportunists" kama fisi wanavyongoja mifupa au makopangola wanavyoona mzoga, hawachelewi! ndicho kilichopo.

Usione vinaelea vimeundwa.

Mtannzania unayemzungumzia ni Ishomire Rugemalila? Yeye si ameshalipwa akaamua kunyamaza?

uhusiano wa hii issue na kina Muhongo na Maswi ukoje? ... ukiangalia kwa mbali unapata picha kuwa kina Muhongo na Maswi hawataki kujihusisha na hizi kelele wanataka ziishe haraka au kama zinaendelea wasiingizwe huko ndani! .... pia sielewi roles za wabunge wa upinzani & wa CCM (wanaopigia kelele hii issue), Spika (anayejaribu kunyamazisha kelele), TANESCO, Werema kama AG
 
Huyo Ishomire or whatever he is, ndiyo master-mind wa mgogoro, kashtuka ngoma iko wavuni.

Mhongo na Maswi, wanaonewa tu, hawana chochoe katika hili, wao wameingia Wizarani IPTL tayari wana mgogoro na Tanesco na wamepelekwa mahakamani.

Kuwaingiza hao ni ujinga tu watu fulani fulani ambao siasa zimewashinda na kilichobaki wanatafuta kila aina ya harufu ya uvundo waifanye ndio pakutokea.

Wanasiasa wa Tanzania wamekosa ubunifu, wao wako kwenye kutafuta media support kwa njia ya mkato, na waandishi wetu si unajuwa? kibahasha kikiingia mfukoni wataandika chochote utakacho. Kama unabisha muuliza Pasco, mzee wa vibahasha.

Uozo mtupu, waandishi uozo, wanasiasa uchwara. Matokeo ndio huu upuuzi, hakuna chochote cha maana. Mwenye kufikiri japo kiduchu anajuwa kua hapa hakuna wizi kuna "opportunity".
 
Mwenye akili za kauzimwa tu ndio hatamuelewa Zitto anasubiri bwana zake wahafidhina waseme ndio aingie kibla,anayesema Zitto mla rushwa si ndio inatakiwa aweke ushahidi mezani?acheni ukilaza mnakubali ingizwa mkenge na fisadi Maswi?achen unafiki wa kimburula mkitegemea Zitto kudharirika hiyo ni ndoto usiitegemee kabisa
 
waandishi wetu si unajuwa? kibahasha kikiingia mfukoni wataandika chochote utakacho. Kama unabisha muuliza Pasco, mzee wa vibahasha.

Uozo mtupu, waandishi uozo, Matokeo ndio huu upuuzi, hakuna chochote cha maana.
FF, kuniita "mzee wa vibahasha" so kunitendea haki!, watu humu watadhani mimi ndio mzee wa kupokea hivyo vibahasha!. Kwenye vibahasha mimi ni msambaza sio mpokea!.

Hili la waandishi uozo nalikubali na ndio reflection ya jamii yetu sisi Watanzania, tukianzia serikali uozo mtupu, inayoongozwa na chama uozo mtupu kilichoozoa kwa rushwa, kinatoa harufu nzito ya uvundo wa rushwa, huku kikiwa na wafuasi uozo mtupu kama kina FF, ambao kila wakipumua ni harufu ile ile ya uozo mtupu!, wanaounda jamii ya uozo mtupu, na waandishi kama sehemu ya hii jamii ya uozo mtupu, ndio wanaowandikia uozo mtupu, na jamii inapokea uozo mtupu, na kuusoma huo uozo mtupu, na kuuamini huo uozo mtupu hivyo Tanzania kuwa ni taifa la uozo mtu katika ujumla wake na ndio maana hakuna chochote cha maana!.

Kama serikali ni uozo mtupu!, bunge nalo ni uozo mtupu!, mahakama nayo ni uozo mtupu!, what do you expect kwa taifa let alone sisi waandishi uozo mtupu?!.

Mungu Saidia!.

Pasco.
 
Wacha kucheza na maneno, mwenyewe ulikiri umeshavipokea sana tu, au tukuwekee ulivyoandika?

Halafu utasambaza nini bila wewe kuvipokea vibahasha unavyosambaza? wacha kucheza na maneno.
 
Hapo Zitto anaongelea Tax, tena ya Capital gain.

Zitto anaelewa sana kuhusu Tax evasion na Tax avoidance lakini hilo anajifanya kama halijui. Ananshangaza!

Hapo jamaa hawakufanya Tax evasion hapo ni simply Tax avoidance, kisheria.

Hakuna ujanja hapo, kama hawakufanya evasion, walichofanya "avoidance" ni halali kabisa.

Zitto anachoshindwa kueleza ni kuwa IPTL ilikuwa na mgogoro na kampuni ya Kitanzania, kaingia Singasinga kaiona opportunity na kajuwa vipi atatatuwa huo mgogoro, kaongea nao wamekubaliana, kawanunua, kawalipa, kavuta fedha walizokuwa walipwe wao.

Kinachofata hapo ni uhalali wa tax na ndio anauongelea Zitto, kachimbuwa kakuta hakuna tax evasion bali kuna tax avoidance ambayo kisheria ni halali, cha kushangaza hapo hagusii kabisa.

Sijui msichokielewa anachoongelea Zitto zaidi ya hicho ni nini?

Nadhani, Zitto angekuwa kidogo mjanja asingeongelea hilo la kampuni kuuzwa million 6, unless anajuwa anachokifanya ila anataka ku divert msimamo, kuna kila uwezekano na yeye kavuta au anataka kuvuta amma kwa Singa amma kwa IPTL amma kwa huyo Mtanzania mwingine ambae hatajwi sana humu, amma kisha vuta kwa mmoja wao, lakini yeye huyo Mtanzania ndio master-mind wa huu mkorogano na Zitto anajuwa sana hilo.

Hapo sasa hivi kuna kila mtu kutaka kuvuta kwa Singa kwa kupiga makelele, kwa sababu hapo ndio where the buck stopped.

My Take:
Nasema huyo Mtanzania ni mastermind kwa sababu yeye alifikiri akiwabana sana IPTL watakubali yaishe wachukuwe fedha wagawane halafu mitambo yote atabaki nayo yeye aanze kuchuma peke yake kiulaini.

Bahati nzuri au mbaya, Singa kaliona hilo akaingia kati na kuna kila sababu kakubaliana na IPTL kuwa wataumizwa, yeye ana njia mbadala watakuwa ni win win situation, pesa watapata na mitambo haitopotea na wamuamini yeye, na ndicho kilichofanyika.

Hapo aliyeumia ni Mtanzania mwenzetu, tena si kaumia kwa kuwa hajapata faida ya bure, la hasha, faida kapata ya bure tena kubwa sana, kwani yeye hajatia fedha yake katika hili sakata, yeye alikuwa kama godfather tu wa ku-facilitate mambo ndani ya Tanzania. Ndiyo norm kwa biashara zote kubwa duniani.

Alichoumia ni pale alipotaka kubana mpaka mitambo yote ibaki kwake. Kataka kula kiharamu zaidi, ndipo Singa alipoingia na ku rescue.

Sasa, Mbonde kuona hivyo ni lazima apigane, kwani kwa sasa fedha ya kuwalisha wapayukaji hovyo kama akina Tumbili anayo, na afanye nini zaidi? anachofanya ni "kama kukosa tukose wote", lakini amechelewa jamvini karamu imeshaliwa.

Mwisho wa siku, kisheria ataibuka Singa kidedea, labda afanyiwe umafia. Na Singa si mdogo huyo, Tanzania anaijuwa juu chini, kaishi sana pande za Iringa, kama kuna mtu anaikumbuka RCC Iringa, basi ni hao akina Singa, si wageni kabisa Tanzania hii.

Mengine yote ni kubwabwaja, porojo na kuhororoja, kuna mshiko wa watu kunyamazishwa na ndiyo maana unasikia kelele.

Hakuna wizi hapo wa mali ya umma kisheria, kuna "opportunity" na Watanzania kama ujuavyo ni ma "opportunists" kama fisi wanavyongoja mifupa au makopangola wanavyoona mzoga, hawachelewi! ndicho kilichopo.

Usione vinaelea vimeundwa.

umeeleweka..thanx
 
Back
Top Bottom