Fedha zilizokuwa katika akaunti maalumu ya IPTL (Tegeta Escrow account), ni mali ya umma

Fedha zilizokuwa katika akaunti maalumu ya IPTL (Tegeta Escrow account), ni mali ya umma

Hapa naona Zitto analazimishwa kuungwa mkono na upinzani wakati yeye huwa hapendi kuungana wapinzanj wenzake kwani atawauzi ccm au ccm hawatamsifia. Ukipenda kujitenga na kujiona msomi na mbinafsi endelea mwenyewe na hao watakaokuunga mkono. Zitto akumbuke yeye ndio sehemu ya kuuvunja upinzani nguvu kwa kujifanya msomi, kuleta mawazo ya ukabila sijui ukanda huku akipata sifa toka ccm na kuvimba kichwa, leo inakuwaje tena kutaka msaada toka upinzani hata kama ni hoja yenye manufaa kwa wananchi?

kwa hiyo mkuu wewe uko upande wa zitto au singasinga
 
Hapo Zitto anaongelea Tax, tena ya Capital gain.

Zitto anaelewa sana kuhusu Tax evasion na Tax avoidance lakini hilo anajifanya kama halijui. Ananshangaza!

Hapo jamaa hawakufanya Tax evasion hapo ni simply Tax avoidance, kisheria.

Hakuna ujanja hapo, kama hawakufanya evasion, walichofanya "avoidance" ni halali kabisa.

Zitto anachoshindwa kueleza ni kuwa IPTL ilikuwa na mgogoro na kampuni ya Kitanzania, kaingia Singasinga kaiona opportunity na kajuwa vipi atatatuwa huo mgogoro, kaongea nao wamekubaliana, kawanunua, kawalipa, kavuta fedha walizokuwa walipwe wao.

Kinachofata hapo ni uhalali wa tax na ndio anauongelea Zitto, kachimbuwa kakuta hakuna tax evasion bali kuna tax avoidance ambayo kisheria ni halali, cha kushangaza hapo hagusii kabisa.

Sijui msichokielewa anachoongelea Zitto zaidi ya hicho ni nini?

Nadhani, Zitto angekuwa kidogo mjanja asingeongelea hilo la kampuni kuuzwa million 6, unless anajuwa anachokifanya ila anataka ku divert msimamo, kuna kila uwezekano na yeye kavuta au anataka kuvuta amma kwa Singa amma kwa IPTL amma kwa huyo Mtanzania mwingine ambae hatajwi sana humu, amma kisha vuta kwa mmoja wao, lakini yeye huyo Mtanzania ndio master-mind wa huu mkorogano na Zitto anajuwa sana hilo.

Hapo sasa hivi kuna kila mtu kutaka kuvuta kwa Singa kwa kupiga makelele, kwa sababu hapo ndio where the buck stopped.

My Take:
Nasema huyo Mtanzania ni mastermind kwa sababu yeye alifikiri akiwabana sana IPTL watakubali yaishe wachukuwe fedha wagawane halafu mitambo yote atabaki nayo yeye aanze kuchuma peke yake kiulaini.

Bahati nzuri au mbaya, Singa kaliona hilo akaingia kati na kuna kila sababu kakubaliana na IPTL kuwa wataumizwa, yeye ana njia mbadala watakuwa ni win win situation, pesa watapata na mitambo haitopotea na wamuamini yeye, na ndicho kilichofanyika.

Hapo aliyeumia ni Mtanzania mwenzetu, tena si kaumia kwa kuwa hajapata faida ya bure, la hasha, faida kapata ya bure tena kubwa sana, kwani yeye hajatia fedha yake katika hili sakata, yeye alikuwa kama godfather tu wa ku-facilitate mambo ndani ya Tanzania. Ndiyo norm kwa biashara zote kubwa duniani.

Alichoumia ni pale alipotaka kubana mpaka mitambo yote ibaki kwake. Kataka kula kiharamu zaidi, ndipo Singa alipoingia na ku rescue.

Sasa, Mbonde kuona hivyo ni lazima apigane, kwani kwa sasa fedha ya kuwalisha wapayukaji hovyo kama akina Tumbili anayo, na afanye nini zaidi? anachofanya ni "kama kukosa tukose wote", lakini amechelewa jamvini karamu imeshaliwa.

Mwisho wa siku, kisheria ataibuka Singa kidedea, labda afanyiwe umafia. Na Singa si mdogo huyo, Tanzania anaijuwa juu chini, kaishi sana pande za Iringa, kama kuna mtu anaikumbuka RCC Iringa, basi ni hao akina Singa, si wageni kabisa Tanzania hii.

Mengine yote ni kubwabwaja, porojo na kuhororoja, kuna mshiko wa watu kunyamazishwa na ndiyo maana unasikia kelele.

Hakuna wizi hapo wa mali ya umma kisheria, kuna "opportunity" na Watanzania kama ujuavyo ni ma "opportunists" kama fisi wanavyongoja mifupa au makopangola wanavyoona mzoga, hawachelewi! ndicho kilichopo.

Usione vinaelea vimeundwa.
Ungemalizia na jinsi Standard Chartered walivyopigwa bao na Kalasinga.
Waingereza watawaheshimu wabongo, hii industry nilikuwa naionea huruma lakini nadhani kuna vichwa vimeshehena.
Itachukua muda, ila watu wataelewa tu.
 
Kama kawaida ya watanzania, wana deal na messenger na kuacha message ambayo ndio ina manufaa kwao. Umaskini wa hii nchi sio bure, aina ya watu iliyonao inaeleza wazi kuwa nchi hii ina haki ya kuendelea kuwa maskini na akina Maswi wataendelea kupiga dili watakavyo at the expense of mtanzania maskini asiye na mtetezi.
 
Ungemalizia na jinsi Standard Chartered walivyopigwa bao na Kalasinga.
Waingereza watawaheshimu wabongo, hii industry nilikuwa naionea huruma lakini nadhani kuna vichwa vimeshehena.
Itachukua muda, ila watu wataelewa tu.

Standard Chartered hawakupigwa bao na Kalasinga, hata chembe.

Kalasinga kaeleza wazi kwenye press cinference kuwa kazinunua kampuni na madeni yake yote, kama Standard Chartered wanadai, wawasiliane na Singa.

Hili sakata hata walitamani kumuingiza Balozi wa Uingereza sasa hivi wamekaa kimya, jiulize kwanini?

Balozi wa Uingereza kawashushua au Kalasinga? wameufyata.

Kama nilivyoosema ni makopangola yamesikia harufu yakajuwa kuna mzoga, yamekuta mpaka mifupa imeshaliwa, sasa wafanye nini? anajitahidi waambulie japo vibahasha vya kufutia machozi. Hakuna zaidi.
 
Wacha kucheza na maneno, mwenyewe ulikiri umeshavipokea sana tu, au tukuwekee ulivyoandika?. Halafu utasambaza nini bila wewe kuvipokea vibahasha unavyosambaza? wacha kucheza na maneno.
Faiza, ni kweli zamani wakati nikiwa mwandishi wa newsroom nimevipokea sana hivyo vibahasha!. By then, I was working for money!, nilikuwa ninafanya kazi ili nipate pesa!.

Sasa its more than ten years sifanyi kazi ya mtu!, I don't work for money!, I made money, and now I use that money to work for me!. Nimeisha zitengeneza hizo fedha, sizitumikii tena fedha bali sass nazitumia hizo fedha to work for me!, ndio maana nimekuambia hizo bahasha kwa sass mimi ndio msambaza!. Kamwe hutakaa unione eti ninapokea bahasha!, ukiniona tuu mahali na kuna habari inahusika, jua niko pale kwa ajili ya kuzisambaza tuu!.

Angalizo!, bahasha hizi ninazozisambaza ni bahasha halali stahiki na stahili kwa waandishi, zinagawiwa wazi wazi bila kificho, na kila anayepata, ana sign kupokea!.

Na kwa msiojua, [h=3]Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni ..[/h]
Pasco
 
Hizo pesa za watoa huduma (service providers), malipo yao halali kwa huduma waliyotoa kama ilivyo kwenye mikataba yao ya kutoa huduma hiyo.

Zilikuwa public funds kabla hazijalipwa na mradi zimeshakusudiwa kulipwa watoa huduma na kupelekwa escrow account zimeshakuwa si public funds tena.

KUMBUKA.

unamaanisha ni utaratibu wa kawaida kwa Tanesco kumlipa service provider IPTL kwa kutumia account ya Tegeta Escrow. jipange upya kwa hoja yako kabla kibaruwa chako cha uposhaji FJ hakijaota majani
 
Mbona Zitto hajibu hoja ya Maswi kuwa hajachangia wizara ya nishat na madini toka 2011?

Mbona hajitokezi kumjibu nje ya bunge hadharani si nyuma ya keyboard?

Tokanlini Zitto ameanza kuwa mtetezi wa wanawake?

Alishachukua chake mdau! Ukiona Zotto anakomalia sana hoja ujue hajapa mshiko na anataka apewe mshiko, hii mndio tabia ya zitto ndugu.
 
Muhongo+px.jpg

The minister for Energy and Minerals, Prof Sospeter Muhongo.PHOTO|FILE By Elias Msuya ,The Citizen Reporter

Posted Sunday, June 29 2014 at 10:00

Dar es Salaam. Two MPs yesterday piled pressure on the government over the payment from the escrow account held by the Bank of Tanzania (BoT) to Pan African Power (PAP) — a private company.

Mr David Kafulila (Kigoma South – NCCR-Mageuzi) and Mr Zitto Kabwe (Kigoma North – Chadema) insisted that thorough investigations should be conducted to ascertain how the money was withdrawn from the account which was opened following a misunderstanding between the Tanzania Electric Supply Company (Tanesco) and Independent Power Tanzania Limited (IPTL).

They made the remarks during a live interview by a Swahili service of Deutsche Welle yesterday afternoon.

The minister for Energy and Minerals, Prof Sospeter Muhongo, who was invited to participate in the programme failed to turn up on grounds that the discussion was not beneficial to the government.

The two MPs made the remarks a day after the permanent secretary in the ministry of Energy and Minerals, Mr Eliachim Maswi said the documents they were using to push for their demands were fake.

Mr Maswi dared Mr Kafulila to use the documents outside the Parliament so that he could take legal measures against him.

However, Prime Minister Mizengo Pinda has directed the Prevention and Combating of Corruption Bureau and the Controller and Auditor General to investigate the matter.

Speaking during the Deutsche Welle programme, Mr Kabwe insisted that the $112 million which was withdrawn from the escrow account and handed to PAP was public money, contrary to the government position that the money belonged to the company.

“This is a very serious scandal and someone should be held accountable,” said Mr Kabwe.

Mr Kafulila said the controversy dated from 1994 and wondered why the government had done nothing to resolve it.

 
Mbona Zitto hajibu hoja ya Maswi kuwa hajachangia wizara ya nishat na madini toka 2011?

Mbona hajitokezi kumjibu nje ya bunge hadharani si nyuma ya keyboard?

Tokanlini Zitto ameanza kuwa mtetezi wa wanawake?

Huu ni upuuzi! kwa nini uamini kuwa hayo yanatosha kumfanya ZZK kuogopa kuhoji kwa namna yoyote ile ubadhilifu wa pesa za walipa kodi? Ninaamini kupinga kiburi cha Maswi kujiona ni mwanaume zaidi ya wanaume wengine kwa kuwa anafahamu kuwa alisimamia kumpa rushwa ZZK ili akae kimya kwenye ukiukaji wa taratibu za serikali kunaleta picha ya kuwa wanawake hawana sauti katika mambo muhimu nchini. Maswi akae kimya ili mfumo umsafishe kama hahusiki.
 
unamaanisha ni utaratibu wa kawaida kwa Tanesco kumlipa service provider IPTL kwa kutumia account ya Tegeta Escrow. jipange upya kwa hoja yako kabla kibaruwa chako cha uposhaji FJ hakijaota majani

Ni utaratibu wa kawaida kwenye biashara kubwa na kwenye dispute.
 
....uwa najiuliza mpaka haya yote yanatokea huwa mkuu wa nchi hana taarifa kweli?.Tukianzia kwenye issue ya Richmond,EPA na ESCROW ni wazi hakuna leadership....scandals zote binafsi naona ni uzembe wa nchi kwa maana kuwa yametokea lakini kana kwamba hakuna kitu kilichotokea!.Naumia sana kuona jamii yangu wana kufa maskini huku taifa ikipoteza kwa makusudi utajiri wake!....wajue tutakuja usiku ata mchana kuwanyanganya.
 
Tatizo si zitto wala kafulila wala werema wala maswi. Tatizo ni jk kaingiza wahuni ikulu
 
Mbona Zitto hajibu hoja ya Maswi kuwa hajachangia wizara ya nishat na madini toka 2011?Mbona hajitokezi kumjibu nje ya bunge hadharani si nyuma ya keyboard?Tokanlini Zitto ameanza kuwa mtetezi wa wanawake?
Zitto anaweza kukuweka ndani na kukuhudumia km wanawake wengine
 
Ni utaratibu wa kawaida kwenye biashara kubwa na kwenye dispute.

Kama unasema ni utaratibu unaotumika kama kuna dispute na ICSID walitoa huku kuwa Tanesco walilipiswa hela nyingi kwa kutumia PPA ya kihuni. sasa inakuwaje unasema hela yote iliyokuwa Tegeta Escrow account ni halali kupewa mtoa huduma IPTL. kuhusu swala la Tax evasion na Tax avoidance ni swala dogo lakini pia la muhimu. la muhimu zaidi ni inakuwaje share za kampuni ambayo ilkuwa kwa liquidator imeweza kuuza share zake kwa singasinga ambae amefanya ufisadi mbaya kenya na tena anamiliki vitalu vya gas tanzania ambako tulikuwa tukilalamika mikataba ya gasi mibovu ya kuharakishwa.jipange upya
 
Zitto we endelea kutupigania Wanyonge, wanaokubeza ni wahuni tu, sisi Wananchi tulio wengi tunakuunga mkono.
 
Kwa mara nyingine serikali kupitia viongozi na watendaji wake akiwamo Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), wamedai kwamba kiasi cha Dola za Marekani milioni 250 zilizopaswa kuendelea kuwapo katika ‘Tegeta Escrow Account' si mali ya serikali na hivyo si mali ya umma. Akaunti hiyo ilifunguliwa na serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) pamoja na kampuni ya Independent Power Limited (IPTL).

Kwa bahati mbaya sana viongozi wa serikali wamekuwa wakiendelea kurudia kuueneza huo uongo kwamba fedha hizo si mali ya umma. Inasikitisha pia kwamba vyombo vya habari vimekuwa navyo vikibeba na kusambaza huo uongo bila kuhoji na kuchunguza. Inashangaza sana pia asasi za kiraia nazo zimekaa kimya. Inatisha na kushangaa tena kuona wapinzani wakimwachia suala hili Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, pekee wakati mapambano dhidi ya rushwa ni ajenda kuu ya wapinzani. Kafulila amekuwa akiendelea kuhoji suala hilo bungeni peke yake bila kupata kuungwa mkono na kupewa msaada wa aina yoyote kutoka kwa wenzake wa kambi ya upinzani bungeni.

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ilielekeza kuwapo kwa ukaguzi maalumu kwenye akaunti hiyo ya Tegeta escrow account iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kuwa ndani yake kulikuwapo fedha za umma. PAC haina sababu yoyote ya kufuatilia fedha za watu binafsi. Mwaka 2009 iliyokuwa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) ilitoa maelekezo kwa BoT kutothubutu kutoa fedha hizo. Agizo hilo la POAC lilitokana na sababu kwamba fedha hizo zilikuwa ndani ya hesabu za Tanesco.

Akaunti ya ‘Tegeta escrow' ilifunguliwa kutokana na kuwapo kutoelewana kuhusiana na gharama halisi na halali za umeme unaozalishwa na IPTL na kuuzwa kwa TANESCO. Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa (ICSID) katika uamuzi wake wa Februari, 2014 ilitoa hukumu kuonyesha kwamba Tanesco walitozwa kiwango cha juu zaidi ya kilichopaswa kulipwa kwa IPTL. Kwa uamuzi huo ni dhahiri kwamba fedha zilizokuwa zimehifadiwa kwenye akaunti hiyo maalumu ya escrow zilipaswa kugawanywa kwa IPTL na Tanesco baada ya hesabu kufanyiwa marekebisho upya kwa viwango halali.

Hesabu za mwaka wa fedha ulioishia Disemba 2012 za Tanesco zinaonyesha wazi kwamba fedha hizo ni mali ya shirika hilo la umma linalomilikiwa na serikali kwa asilimia mia moja. Fedha za kampuni ni suala la kisheria kama inavyobainishwa katika sheria ya kampuni ya mwaka 2002.

Kwa maelezo hayo na hoja hizo, inakuaje serikali ianze kudai kwamba fedha hizo si mali ya umma? Hivi inawezekanaje kwa fedha za mtu binafsi zikaingizwa katika hesabu za shirika la umma linalomilikiwa na serikali kwa asilimia 100? Ni lini fedha hizo zimekoma kuwa za umma? Je ni baada ya baadhi ya watendaji wa serikali kula njama za kuzichukua fedha hizo kwa kushirikiana na ‘mwekezaji' aliyechafuka kwa ufisadi duniani?

Serikali inadanganya waziwazi kudai kwamba fedha hizo si mali ya umma. Umma una haki ya kukumbushwa kwamba madai hayo yalitolewa pia katika lile sakata la ufisadi maarufu wa EPA unaofanana kwa kila hali na huu wa sasa wa ‘Tegeta Escrow'.

Hoja nyingine ni kwamba, Mbunge Kafulila alisema kwamba Jaji Utamwa wa Mahakama Kuu ya Tanzania hakutoa uamuzi wa kuchukuliwa fedha kutoka akaunti ya ‘Tegeta Escrow'. Nimepitia kwa makini hukumu ya Jaji Utamwa na kubaini kwamba hakuna popote alipotaja akaunti ya ‘Escrow'. Hata hivyo, nilipopitia muhstasari wa kikao kati ya TANESCO, IPTL na Wizara ya Nishati na Madini, ndipo kwa mara ya kwanza nikakuta wametafsiri uamuzi wa mahakama wakidai kwamba fedha zote za ‘Tegeta Escrow' zipewe kampuni ya PAP (inamilikiwa kwa asilimia 50 na Harbinder Singh na 50% na Simba Trust iliyosajiliwa Australia). Hiki ndicho kikao kilichofanya maamuzi ya kuiba na kugawana wenyewe fedha hizo (Hukumu ya Jaji Utamwa na muhstasari wa kikao vinaambatanishwa).

Wote waliohudhuria kikao hicho kilichojipa mamlaka ya kutafsiri hukumu ya Mahakama Kuu, wanapaswa kuchunguzwa na kufikishwa mahakamani kwa mujibu wa sheria zilizopo. Inawezekana vipi uamuzi wa mahakama ukatafsiriwa na kikao cha Wizara? Muhstasari wa kikao hicho ndio uliowasilishwa Benki Kuu (BoT) kuhalalisha madai kwamba fedha hizo lazima zitolewa kutoka akaunti ya Escrow.

Fedha zinazohusiana na akaunti ya Escrow ni Dola za Marekani milioni 250, katia ya hizo Dola milioni 122 zilizokuwa BoT zimeshatolewa na kiasi kilichosalia Dola milioni 128 zitalipwa na Tanesco kutokana na fedha zake kwa madai ya kushindwa kulipa kwa wakati. Fedha zilizolipwa ni zile ambazo zimetoka Wizara ya Nishati na Madini ambayo kisheria ndio walipaswa kulipia gharama za uzalishaji umeme (capacity charge) fedha zilizotoka kwa walipa kodi.

Ikumbukwe kwamba uhamishaji wa asilimia 70 ya hisa za IPTL kwenda PAP umeambatana na nyaraka za kughushi kutokana na kutokuwepo kabisa kwa uthibitisho wa cheti halisi cha hisa (share certificate) kutoka kampuni ya Mechmar kwenda kampuni ya Piperlink. Nyaraka za TRA zinaonyesha kwamba hisa hizo (70%) ziliuzwa kwa Shilingi za Kitanzania milioni sita (6) tu. Na bado hakuna ushahidi kuonyesha kwamba uhamishaji huo wa hisa ulipata baraka za mamlaka husika kama inavyotakiwa na sheria za nchi.

Wakati huyo anayejiita mmiliki mpya wa IPTL aliposaini mkataba wa kuchukua fedha kutoka akaunti ya Escrow zilizokuwapo BoT, hakuwa mmiliki halali kisheria kwani kodi ililipwa siku moja baada ya wao kupokea fedha kutoka BoT. Sheria inataka kutolewa kwa cheti na Kamishna wa TRA kama uthibitisho kwamba kodi yote imelipwa ipasavyo (Sheria ya Fedha ya 2012 kifungu cha 29).

Ni nani wamiliki wengine wa kampuni ya PAP? Uchunguzi ni muhimu ukawalenga vigogo na wanasiasa wakubwa wakiwamo watendaji waandamizi wa Wizara ya Nishati na Madini.
Inapaswa tutafakari kuona kwamba Harbinder Singh aliyechukua fedha za Escrow, anamiliki vitalu vya mafuta na gesi kupitia kampuni iitwayo HydroTanz ambayo nayo imesajiliwa nchini Australia, ikiwa na anwani sawa na ya kampuni ya Simba Trust. Kitalu hicho cha mafuta kinaitwa ‘Mnazi Bay North', jirani kabisa na ugunduzi mkubwa wa hivi karibuni mkoani Mtwara.

Tunatarajia kwamba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), atafichua ukweli wa sakata hili na TAKUKURU itawafikisha mahakamani wahusika bila kujali nyadhifa zao serikalini.
Kauli ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, kwamba kuna watu waliokula rushwa na kwamba nyaraka zinazotajwa ni karatasi za kuuzia vitumbua, ni kauli zenye kuonyesha kutapatapa kwa watendaji serikalini. Hakuna hata mahali pamoja ambapo nimemtaja mtu kuwa ni mwizi zaidi ya kuwasilisha hoja zinazohitaji majibu mwafaka na si matusi, vitisho na tuhuma za kuzusha. Nyaraka za TRA haziwezi kuwa za kufungua maandazi kama ambavyo hukumu ya Jaji wa Mahakama Kuu haiwezi kuwa karatasi za kufungia maandazi na badala yake ni nyaraka halali zinazohitaji maelezo kutoka kwa viongozi na watendaji wa serikali badala ya kuropoka na kuporomosha matusi.

Hali kadhalika, Bunge lina kila sababu kupitia sheria yake ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kulinda hadhi yake kutoka kwa watendaji kama Maswi ambao wanatoa matamshi ya kuonyesha kwamba chombo hicho ni chombo cha watu wasiofaa na kwamba watu wanaofaa wanazungumza nje ya Bunge. Maswi na wengine kama wana ushahidi wa rushwa dhidi ya mbunge ama yeyote hawapaswi kupayuka ovyo bali kwa nafasi zao wanaweza kuwasiliana na vyombo vya dola kama TAKUKURU na polisi ili wachunguze na kuchukua hatua kama ambavyo vinawachunguza wao.

Kauli ya Maswi kwamba "wanaume" hawazungumzi ndani ya Bunge si tu udhalilishaji wa chombo hicho bali pia inaashiria ugonjwa wa mfumo dume uliotawala miongoni mwa viongozi wetu kwa maana kwamba wanaume ndio wenye hadhi, uwezo na heshima na wanawake ni dhaifu na wasiostahili heshima. Tufumbue macho tuone na tuondoe hisia binafsi zenye kubebwa na itikadi, chuki na misimamo yetu ya kisiasa. Tuwe wazalendo ili tuweze kusimamia utaifa.

Source: Mtandao wa Mabadiliko

:yield:
 
Back
Top Bottom