Fedha zilizokuwa katika akaunti maalumu ya IPTL (Tegeta Escrow account), ni mali ya umma

Fedha zilizokuwa katika akaunti maalumu ya IPTL (Tegeta Escrow account), ni mali ya umma

Mkuu msituni kuna nyoka wenye sumu kali, nakushauri uende kwanza wewe, ukirudi salama ndiyo uwashawishi wenzio, pia mimi kamwe hunishawishi kwenda kugongwa na nyoka kwa fedha za makampuni ya watu ambayo hayanigawii hata elfu kumi, kama maisha magumu nakushauri upambane kutafuta pesa badala ya kusingizia siasa, utakufa masikini.
Leo hujapewa buku 7? Mbona uko msituni?
 
Hivi ni lini hasa serikali hii ya WEZI itang'oka madarakani? Wananchi tujiandikishe kwa wingi kwenye daftari la kudumu, na hima tujitokeze sote kuuangusha utawala huu wa kifisadi kupitia sanduku la kura.

View attachment 168485
 
Not anymore. Hizo na madudu mengine yajayo ni CCM campaign funds 2015.Ushindi lazima.
 
02/07/2014 | Posted by Mwandishi Wetu


MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), amesema kuwa dola za Marekani milioni 250 zilizopaswa kuendelea kuwapo katika akaunti ya ‘Tegeta Escrow’ ni mali ya serikali na hivyo ni mali ya umma.

Zitto amesisitiza kuwa si kweli kama viongozi na watendaji wa serikali akiwamo Mwanasheria Mkuu (AG), wanavyodai kwamba fedha hizo si mali ya serikali na hivyo si mali ya umma.


Kupitia makala yake katika gazeti hili, Zitto anasema akaunti hiyo ilifunguliwa na serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) pamoja na Kampuni ya Independent Power Limited (IPTL).

“Kwa maelezo hayo na hoja hizo, inakuwaje serikali ianze kudai kwamba fedha hizo si mali ya umma? Hivi inawezekanaje kwa fedha za mtu binafsi zikaingizwa katika hesabu za shirika la umma linalomilikiwa na serikali kwa asilimia 100?

“Ni lini fedha hizo zimekoma kuwa za umma? Je, ni baada ya baadhi ya watendaji wa serikali kula njama za kuzichukua fedha hizo kwa kushirikiana na ‘mwekezaji’ aliyechafuka kwa ufisadi duniani?” anahoji.
Zitto anaendelea kuhoji ni nani wamiliki wengine wa Kampuni ya PAP inayodai kuinunua Kampuni ya IPTL?


“Uchunguzi ni muhimu ukawalenga vigogo na wanasiasa wakubwa wakiwamo watendaji waandamizi wa Wizara ya Nishati na Madini,” anasema.
Kwamba inapaswa tutafakari kuona kwamba Harbinder Singh aliyechukua fedha za Escrow, anamiliki vitalu vya mafuta na gesi kupitia kampuni iitwayo HydroTanz ambayo nayo imesajiliwa nchini Australia, ikiwa na anwani sawa na ya Kampuni ya Simba Trust.


Anasema kitalu hicho cha mafuta kinaitwa ‘Mnazi Bay North’, kilichopo jirani kabisa na ugunduzi mkubwa wa hivi karibuni mkoani Mtwara.
 
Fedha za Escrow ni mali ya umma

02/07/2014 | Posted by Zitto Kabwe

KWA mara nyingine serikali kupitia viongozi na watendaji wake akiwamo Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), wamedai kwamba kiasi cha dola za Marekani milioni 250 zilizopaswa kuendelea kuwapo katika ‘Tegeta Escrow Account' si mali ya serikali na hivyo si mali ya umma.

Akaunti hiyo ilifunguliwa na serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) pamoja na kampuni ya Independent Power Limited (IPTL).
Kwa bahati mbaya sana viongozi wa serikali wamekuwa wakiendelea kurudia kuueneza huo uongo kwamba fedha hizo si mali ya umma. Inasikitisha pia kwamba vyombo vya habari vimekuwa navyo vikibeba na kusambaza huo uongo bila kuhoji na kuchunguza.

Inashangaza sana pia asasi za kiraia nazo zimekaa kimya. Inatisha na kushangaa tena kuona wapinzani wakimwachia suala hili mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, pekee wakati mapambano dhidi ya rushwa ni ajenda kuu ya wapinzani.


Kafulila amekuwa akiendelea kuhoji suala hilo bungeni peke yake bila kupata kuungwa mkono na kupewa msaada wa aina yoyote kutoka kwa wenzake wa kambi ya upinzani bungeni.
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ilielekeza kuwapo kwa ukaguzi maalumu kwenye akaunti hiyo ya Tegeta escrow account iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kuwa ndani yake kulikuwapo fedha za umma.


PAC haina sababu yoyote ya kufuatilia fedha za watu binafsi. Mwaka 2009 iliyokuwa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) ilitoa maelekezo kwa BoT kutothubutu kutoa fedha hizo.


Agizo hilo la POAC lilitokana na sababu kwamba fedha hizo zilikuwa ndani ya hesabu za Tanesco.
Akaunti ya ‘Tegeta escrow' ilifunguliwa kutokana na kuwapo kutoelewana kuhusiana na gharama halisi na halali za umeme unaozalishwa na IPTL na kuuzwa kwa Tanesco.
Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa (ICSID) katika uamuzi wake wa Februari, 2014 ilitoa hukumu kuonyesha kwamba Tanesco walitozwa kiwango cha juu zaidi ya kilichopaswa kulipwa kwa IPTL.


Kwa uamuzi huo ni dhahiri kwamba fedha zilizokuwa zimehifadiwa kwenye akaunti hiyo maalumu ya escrow zilipaswa kugawanywa kwa IPTL na Tanesco baada ya hesabu kufanyiwa marekebisho upya kwa viwango halali.

Hesabu za mwaka wa fedha ulioishia Disemba 2012 za Tanesco, zinaonesha wazi kwamba fedha hizo ni mali ya shirika hilo la umma linalomilikiwa na serikali kwa asilimia mia moja. Fedha za kampuni ni suala la kisheria kama inavyobainishwa katika sheria ya kampuni ya mwaka 2002.


Kwa maelezo hayo na hoja hizo, inakuaje serikali ianze kudai kwamba fedha hizo si mali ya umma? Hivi inawezekanaje kwa fedha za mtu binafsi zikaingizwa katika hesabu za shirika la umma linalomilikiwa na serikali kwa asilimia 100?
Ni lini fedha hizo zimekoma kuwa za umma? Je ni baada ya baadhi ya watendaji wa serikali kula njama za kuzichukua fedha hizo kwa kushirikiana na ‘mwekezaji' aliyechafuka kwa ufisadi duniani?


Serikali inadanganya waziwazi kudai kwamba fedha hizo si mali ya umma. Umma una haki ya kukumbushwa kwamba madai hayo yalitolewa pia katika lile sakata la ufisadi maarufu wa EPA unaofanana kwa kila hali na huu wa sasa wa ‘Tegeta Escrow'.



Hoja nyingine ni kwamba, mbunge Kafulila alisema kwamba Jaji Utamwa wa Mahakama Kuu ya Tanzania hakutoa uamuzi wa kuchukuliwa fedha kutoka akaunti ya ‘Tegeta Escrow'.


Nimepitia kwa makini hukumu ya Jaji Utamwa na kubaini kwamba hakuna popote alipotaja akaunti ya ‘Escrow'. Hata hivyo, nilipopitia muhstasari wa kikao kati ya Tanesco, IPTL na Wizara ya Nishati na Madini, ndipo kwa mara ya kwanza nikakuta wametafsiri uamuzi wa mahakama wakidai kwamba fedha zote za ‘Tegeta Escrow' zipewe kampuni ya PAP (inamilikiwa kwa asilimia 50 na Harbinder Singh na 50% na Simba Trust iliyosajiliwa Australia).


Hiki ndicho kikao kilichofanya maamuzi ya kuiba na kugawana wenyewe fedha hizo (Hukumu ya Jaji Utamwa na muhstasari wa kikao vinaambatanishwa).
Wote waliohudhuria kikao hicho kilichojipa mamlaka ya kutafsiri hukumu ya Mahakama Kuu, wanapaswa kuchunguzwa na kufikishwa mahakamani kwa mujibu wa sheria zilizopo.


Inawezekana vipi uamuzi wa mahakama ukatafsiriwa na kikao cha Wizara? Muhstasari wa kikao hicho ndio uliowasilishwa Benki Kuu (BoT) kuhalalisha madai kwamba fedha hizo lazima zitolewa kutoka akaunti ya Escrow.
Fedha zinazohusiana na akaunti ya Escrow ni dola za Marekani milioni 250, katia ya hizo dola milioni 122 zilizokuwa BoT zimeshatolewa na kiasi kilichosalia dola milioni 128 zitalipwa na Tanesco kutokana na fedha zake kwa madai ya kushindwa kulipa kwa wakati.


Fedha zilizolipwa ni zile ambazo zimetoka Wizara ya Nishati na Madini ambayo kisheria ndio walipaswa kulipia gharama za uzalishaji umeme (capacity charge) fedha zilizotoka kwa walipa kodi.
Ikumbukwe kwamba uhamishaji wa asilimia 70 ya hisa za IPTL kwenda PAP umeambatana na nyaraka za kughushi kutokana na kutokuwepo kabisa kwa uthibitisho wa cheti halisi cha hisa (share certificate) kutoka kampuni ya Mechmar kwenda kampuni ya Piperlink.


Nyaraka za TRA zinaonyesha kwamba hisa hizo (70%) ziliuzwa kwa shilingi za Kitanzania milioni sita (6) tu. Na bado hakuna ushahidi kuonyesha kwamba uhamishaji huo wa hisa ulipata baraka za mamlaka husika kama inavyotakiwa na sheria za nchi.

Wakati huyo anayejiita mmiliki mpya wa IPTL, aliposaini mkataba wa kuchukua fedha kutoka akaunti ya Escrow zilizokuwapo BoT, hakuwa mmiliki halali kisheria kwani kodi ililipwa siku moja baada ya wao kupokea fedha kutoka BoT.

Sheria inataka kutolewa kwa cheti na Kamishna wa TRA kama uthibitisho kwamba kodi yote imelipwa ipasavyo (Sheria ya Fedha ya 2012 kifungu cha 29).

Ni nani wamiliki wengine wa kampuni ya PAP? Uchunguzi ni muhimu ukawalenga vigogo na wanasiasa wakubwa wakiwamo watendaji waandamizi wa Wizara ya Nishati na Madini.

Inapaswa tutafakari kuona kwamba Harbinder Singh aliyechukua fedha za Escrow, anamiliki vitalu vya mafuta na gesi kupitia kampuni iitwayo HydroTanz ambayo nayo imesajiliwa nchini Australia, ikiwa na anwani sawa na ya kampuni ya Simba Trust.


Kitalu hicho cha mafuta kinaitwa ‘Mnazi Bay North', jirani kabisa na ugunduzi mkubwa wa hivi karibuni mkoani Mtwara.
Tunatarajia kwamba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), atafichua ukweli wa sakata hili na Takukuru itawafikisha mahakamani wahusika bila kujali nyadhifa zao serikalini.


Kauli ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, kwamba kuna watu waliokula rushwa na kwamba nyaraka zinazotajwa ni karatasi za kuuzia vitumbua, ni kauli zenye kuonyesha kutapatapa kwa watendaji serikalini.
Hakuna hata mahali pamoja ambapo nimemtaja mtu kuwa ni mwizi zaidi ya kuwasilisha hoja zinazohitaji majibu mwafaka na si matusi, vitisho na tuhuma za kuzusha.

Nyaraka za TRA haziwezi kuwa za kufungia maandazi kama ambavyo hukumu ya Jaji wa Mahakama Kuu haiwezi kuwa karatasi za kufungia maandazi na badala yake ni nyaraka halali zinazohitaji maelezo kutoka kwa viongozi na watendaji wa serikali badala ya kuropoka na kuporomosha matusi.

Hali kadhalika, Bunge lina kila sababu kupitia sheria yake ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kulinda hadhi yake kutoka kwa watendaji kama Maswi ambao wanatoa matamshi ya kuonyesha kwamba chombo hicho ni chombo cha watu wasiofaa na kwamba watu wanaofaa wanazungumza nje ya Bunge.


Maswi na wengine kama wana ushahidi wa rushwa dhidi ya mbunge ama yeyote hawapaswi kupayuka ovyo bali kwa nafasi zao wanaweza kuwasiliana na vyombo vya dola kama Takukuru na polisi ili wachunguze na kuchukua hatua kama ambavyo vinawachunguza wao.

Kauli ya Maswi kwamba "wanaume" hawazungumzi ndani ya Bunge si tu udhalilishaji wa chombo hicho bali pia inaashiria ugonjwa wa mfumo dume uliotawala miongoni mwa viongozi wetu kwa maana kwamba wanaume ndio wenye hadhi, uwezo na heshima na wanawake ni dhaifu na wasiostahili heshima.
Tufumbue macho tuone na tuondoe hisia binafsi zenye kubebwa na itikadi, chuki na misimamo yetu ya kisiasa. Tuwe wazalendo ili tuweze kusimamia utaifa.
 
Hadithi Hadithi;

Hadithi njo utamu kolea;

Pamoja na Seth kukubali kuchukua fedha hizo, alisema fedha zilizokuwamo ni Sh150 bilioni, huku akitetea hatua hiyo na ununuzi wa IPTL kwamba siyo kinyume cha sheria.



Kabla ya kuuzwa kwa PAP, IPTL ilikuwa inamilikiwa kwa ubia kati ya Mechmar Corporation ya Malaysia (asilimia 70) na VIP Engineering and Marketing Company Limited ya Tanzania iliyokuwa na asilimia 30.


PAP ni kampuni ya tatu katika mgogoro huo kujitokeza na kutoa ufafanuzi tangu habari zake zilipoanza kuandikwa. Kampuni ya kwanza ilikuwa ni VIP Engineering ya James Rugemalira na baadaye akaibuka Mwanasheria wa IPTL na wote walitetea mauzo hayo.


PAP ilivyonunua IPTL


Wakili wa PAP, Joseph Mwakandege alisema, kwa miaka mitano ya ITPL iliendeshwa bila kuwapo kwa mgogoro, lakini baadaye iliibuka mivutano miongoni mwa wanahisailiyosababisha kufunguliwa kwa akaunti ya Escrow.


Mwakandege alisema 2010, Sethi aliwasilisha nyaraka mahakamani kuonyesha kwamba alipewa mamlaka ya kusimamia mali zote za Mechmar hapa nchini.


Alisema, baadaye Sethi alinunua hisa zote ambazo awali Mechmar alikuwa ameuza kwa Piperlink na kuzihamishia PAP.


Kwa mujibu wa wakili huyo, Sethi baadaye alinunua asilimia 30 zilizosalia, na tayari mmiliki wa VIP, Rugemalira amekwishakiri kupokea Dola za Marekani 75 milioni (Sh120 bilioni) alizoziita kuwa ni fedha za ugoro.


Alisema baada ya mauzo hayo, VIP ilikwenda mahakamani na kuomba kesi zote zinazohusu kampuni hiyo na Mechmar zifutwe.


Septemba 5, mwaka jana, mahakama iliamua kufuta kesi hizo, hivyo PAP akapata haki ya kumiliki mali zote za IPTL, ikiwa ni pamoja na fedha zilizokuwa katika akaunti ya Escrow.


Mwakandege alisema baada ya uamuzi huo, PAP ilikubali kulipa madeni yote ya IPTL na ufilisi wa muda uliokuwa umewekwa kwa kampuni hiyo uliondolewa.


“Kutokana na hali hiyo, ilibidi kusainiwa mkataba kati ya IPTL na Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini…Ifahamike kwamba akaunti ya Escrow ilikuwa mali ya wanahisa wa IPTL, haikuwa na fedha za walipakodi wala fedha za Benki ya Standard Chartered ya Hong Kong (mkopeshaji wa IPTL),” alisema Mwakandege.


Alifafanua kuwa, Serikali iliitaka PAP kusaini makubaliano kwamba iwapo watatokea wadai wapya wa IPTL itawalipa. Alisema baada ya hapo Serikali iliandika barua kwa BoT kuitaka iruhusu fedha hizo zilipwe kwa PAP.
 
Hadithi Hadithi;

Hadithi njoo utamu kolea;

Pamoja na Seth kukubali kuchukua fedha hizo, alisema fedha zilizokuwamo ni Sh150 bilioni, huku akitetea hatua hiyo na ununuzi wa IPTL kwamba siyo kinyume cha sheria.



Kabla ya kuuzwa kwa PAP, IPTL ilikuwa inamilikiwa kwa ubia kati ya Mechmar Corporation ya Malaysia (asilimia 70) na VIP Engineering and Marketing Company Limited ya Tanzania iliyokuwa na asilimia 30.


PAP ni kampuni ya tatu katika mgogoro huo kujitokeza na kutoa ufafanuzi tangu habari zake zilipoanza kuandikwa. Kampuni ya kwanza ilikuwa ni VIP Engineering ya James Rugemalira na baadaye akaibuka Mwanasheria wa IPTL na wote walitetea mauzo hayo.


PAP ilivyonunua IPTL


Wakili wa PAP, Joseph Mwakandege alisema, kwa miaka mitano ya ITPL iliendeshwa bila kuwapo kwa mgogoro, lakini baadaye iliibuka mivutano miongoni mwa wanahisailiyosababisha kufunguliwa kwa akaunti ya Escrow.


Mwakandege alisema 2010, Sethi aliwasilisha nyaraka mahakamani kuonyesha kwamba alipewa mamlaka ya kusimamia mali zote za Mechmar hapa nchini.


Alisema, baadaye Sethi alinunua hisa zote ambazo awali Mechmar alikuwa ameuza kwa Piperlink na kuzihamishia PAP.


Kwa mujibu wa wakili huyo, Sethi baadaye alinunua asilimia 30 zilizosalia, na tayari mmiliki wa VIP, Rugemalira amekwishakiri kupokea Dola za Marekani 75 milioni (Sh120 bilioni) alizoziita kuwa ni fedha za ugoro.


Alisema baada ya mauzo hayo, VIP ilikwenda mahakamani na kuomba kesi zote zinazohusu kampuni hiyo na Mechmar zifutwe.


Septemba 5, mwaka jana, mahakama iliamua kufuta kesi hizo, hivyo PAP akapata haki ya kumiliki mali zote za IPTL, ikiwa ni pamoja na fedha zilizokuwa katika akaunti ya Escrow.


Mwakandege alisema baada ya uamuzi huo, PAP ilikubali kulipa madeni yote ya IPTL na ufilisi wa muda uliokuwa umewekwa kwa kampuni hiyo uliondolewa.


“Kutokana na hali hiyo, ilibidi kusainiwa mkataba kati ya IPTL na Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini…Ifahamike kwamba akaunti ya Escrow ilikuwa mali ya wanahisa wa IPTL, haikuwa na fedha za walipakodi wala fedha za Benki ya Standard Chartered ya Hong Kong (mkopeshaji wa IPTL),” alisema Mwakandege.


Alifafanua kuwa, Serikali iliitaka PAP kusaini makubaliano kwamba iwapo watatokea wadai wapya wa IPTL itawalipa. Alisema baada ya hapo Serikali iliandika barua kwa BoT kuitaka iruhusu fedha hizo zilipwe kwa PAP.
 
Zitto+px.gif

Na Zitto Kabwe, Mwananchi

KWA UFUPI
PAC haina sababu yoyote ya kufuatilia fedha za watu binafsi. Mwaka 2009 iliyokuwa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) ilitoa maelekezo kwa BoT kutothubutu kutoa fedha hizo. .


Kwa mara nyingine Serikali kupitia viongozi na watendaji wake, akiwamo Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), wamedai kwamba kiasi cha Dola 250 milioni za Kimarekani zilizopaswa kuendelea kuwapo kwenye ‘Tegeta Escrow Account' si mali ya Serikali na hivyo si mali ya umma.
Akaunti hiyo ilifunguliwa na Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) pamoja na kampuni ya Independent Power Limited (IPTL).

Kwa bahati mbaya sana viongozi wa Serikali wamekuwa wakiendelea kurudia kuueneza huo uongo kwamba fedha hizo si mali ya umma.

Inasikitisha pia kwamba vyombo vya habari vimekuwa navyo vikibeba na kusambaza huo uongo bila kuhoji na kuchunguza. Inashangaza sana pia asasi za kiraia nazo zimekaa kimya. Inatisha na kushangaza kuona wapinzani wakimwachia suala hili mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, pekee wakati mapambano dhidi ya rushwa ni ajenda kuu ya wapinzani.

Kafulila amekuwa akiendelea kuhoji suala hilo bungeni peke yake bila kuungwa mkono na kupewa msaada wa aina yoyote kutoka kwa wenzake wa kambi ya upinzani bungeni.

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ilielekeza kuwapo kwa ukaguzi maalumu kwenye akaunti hiyo ya escrow iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kuwa ndani yake kulikuwapo fedha za umma.

PAC haina sababu yoyote ya kufuatilia fedha za watu binafsi. Mwaka 2009 iliyokuwa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) ilitoa maelekezo kwa BoT kutothubutu kutoa fedha hizo. Agizo hilo la POAC lilitokana na sababu kwamba fedha hizo zilikuwa ndani ya hesabu za Tanesco.

Akaunti ya ‘Tegeta Escrow' ilifunguliwa kutokana na kuwapo kutoelewana kuhusiana na gharama halisi na halali za umeme unaozalishwa na IPTL na kuuzwa kwa Tanesco.

Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa (ICSID) katika uamuzi wake wa Februari, 2014 ilitoa hukumu kuonyesha kwamba Tanesco walitozwa kiwango cha juu zaidi ya kilichopaswa kulipwa kwa IPTL.

Kwa uamuzi huo ni dhahiri kwamba fedha zilizokuwa zimehifadiwa kwenye akaunti hiyo maalumu zilipaswa kugawanywa kwa IPTL na Tanesco baada ya hesabu kufanyiwa marekebisho upya kwa viwango halali.

Hesabu za mwaka wa fedha ulioishia Desemba 2012 za Tanesco, zinaonyesha wazi kwamba fedha hizo ni mali ya shirika hilo la umma linalomilikiwa na Serikali kwa asilimia mia moja.

Fedha za kampuni ni suala la kisheria kama inavyobainishwa katika sheria ya kampuni ya mwaka 2002.

Kwa maelezo hayo na hoja hizo, inakuwaje Serikali ianze kudai kwamba fedha hizo siyo mali ya umma? Hivi inawezekanaje fedha za mtu binafsi zikaingizwa katika hesabu za shirika la umma linalomilikiwa na Serikali kwa asilimia 100? Ni lini fedha hizo zimekoma kuwa za umma?

Serikali inadanganya waziwazi kudai kwamba fedha hizo siyo mali ya umma. Umma una haki ya kukumbushwa kwamba madai hayo yalitolewa pia katika lile sakata la ufisadi maarufu wa EPA unaofanana kwa kila hali na huu wa sasa wa ‘Tegeta Escrow Account'.

Fedha zinazohusiana na akaunti ya escrow ni Dola 250 milioni za Kimarekani, kati ya hizo Dola 122 milioni zilizokuwa BoT zimeshatolewa na kiasi kilichosalia Dola 128 milioni zitalipwa na Tanesco kutokana na fedha zake kwa madai ya kushindwa kulipa kwa wakati.

Zitto Kabwe ni mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).

Chanzo: Uongo kuhusu akaunti ya Tegeta Escrow uachwe - Maoni - Uchambuzi - mwananchi.co.tz



 
Kafulila ni mtu wa Zitto,na data zote zinatoka kwa Zitto,hapo utaelewa kwa nini upinzania hautoi sapoti
 
Watanzania tumelogwa. Zitto kaweka mambo hadharani, wewe unamwuliza "utetezi wa wanawake". Idiot. Maswi anauliza uchangiaji wa Zitto wizara ya madini akitaka kututoa kwenye hoja ili tumjadili Zitto na wewe unaingia mkenge. Hivi unalipwa au kuna share umenufaika nayo escrow?

Binafsi nina maswal kwa Zitto lakini anapokuja na hoja za kujenga nitazijadili hoja hizo si kuanza kutoa watu nje ya mada husika. la muhimu TUNATAKA HELA ZETU.

Kwa hili watanzania tuwe kitu kimoja bila kujali itikadi zetu. Shule, hospital, maji na huduma zungine zinapokuwa za hovyo hazibagui kwa kufuata vyama vyetu.

HALAFU tusikubali kuitwa TUMBILI tunapohoji pesa zetu. Kuna makaburu wenzetu aina ya Werema wanatuita tumbili ilhali ni weusi na wanafanana na tumbili kuliko hata kafulila. Ni tusi kubwa kumwita mtu tumbili au nyani. Angeita mzungu tungeandamana lakini tumbili mwenzetu katudhalilisha tunakenua.

Zitto, regardless what, kwa hili tuko pamoja.

Hapa tujenge hoja kwa kuuliza pesa zetu zimefanyiwa ni nini na siyo kumshambulia Zitto mana kinachozungumziwa hamkielewi acheni ushabiki kwenye masuala nyeti kama haya yanayogusa masilahi ya taifa
..
 
Sawa ZZK hajachangia hoja hiyo wizara toka 2011,sasa turudi kwenye point ya msingi hela zetu zinarudije toka kwa hawa wezi wa mchana??????Tusitoke nje ya mada!!!!!!!!
 
Tatizo letu watanzania ilimradi baba au ndugu kafaidika na mgao basi unakuja kuharibu mada nzuri kama hizi.Ni wakati muafaka wa kutoa tafakuri za maana kwa maslahi ya nchi yetu.Huu ujinga unaoendelea wa kuvuruga uchunguzi ili akina Sigh wasikamatwe pamoja na wakoloni weusi waliojazana bungeni na wizarani kutaipeleka nchi pabaya.Itafika siku watu watasema sasa basi SOMALIA itakuwa cha mtoto.
 
hili kaa la moto lazima liwatokee magamba makalioni safari hii. yaani hawana pa kutokea. uswisi imefanikiwa kuwawezesha kuficha fedha kwenye mabenki yao lakini uholanzi imewekalia kooni na kuzigandisha ?52 milioni walizoficha nchini humo, na bado!
 
Mkuu,
Karne hii bado unaamini uchawi?
Zitto ajibu hoja ya Maswi why hajachangia hoja wizara ya nishat na madini since 2011?

Tatizo yeye ni mpiga dili tu, anabiga kelele zen anapozwa. MASWI anamjua wote ni wale wale.

fact mkuu
 
Hatimaye gazet la majira la tar.27sept.2014 limeeleza kwamba fedha za escrow sio za umma na ni malipo halali yaliyopewa baraka na bot wizara ya fedha cag gavana na bunge. Akaunty hiyo ilifunguliwa kwa makubaliano kati ya iptl na serekali na bot ilichaguliwa kuwa kama wakala wa kutunza fedha.
Hali hiyo ilitokana na kuwapo kwa mgogoro kati ya wwabia wa iptl ambao ni vip ya rugemarila na mehmar kutoka malaysia ikimilik 70%x.
Nyaraka hizo zinaonyesha mahakama ilielekeza kuwa malipo hayo yahifadhiwe katika akaunt maalum mpaka mgogoro utakapoamliwa na mahakama ambapo wote walikubaliana kufungua akaunt na kuiita escrow.
Mbinu chafu za baadhi ya wagombea urais zilitaka kumtafutia uongo mmojawapo wa wasomi makini wenye uzoefu wa kitaifa na kimataifa kwa kutaka kumuhusisha na upotoshaji huu et alipewa msaada na mmoja wa wabia hao ambae alipewa pesa hizo kihalali jambo ambalo badala ya kumshusha kisiasa prof. Huyu makini prof. Anna Tibaijuka limempandisha mara dufu hasa pale umma na jamii ya kitanzania walipogundua kuiwa ilikuwa ni mbinu chafu ya kutaka kumpaka matope prof. Huyu anna tibaijuka baada ya kuona cv yake na utendaje wake ni wakiutukufu mara dufu.
Nae prof.juzi akiwa katika mahafali ya 12 ya shule ya wasichana babro dsm alisema basi inabidi bunge litunge sheria kali za kudhitibiti michango ikiwemo ya harusi kwan watu wanapokea michango bila kujua inatoka wapi.
Prof. Huyo wa uchumi alisisitiza kuwa alikuja nyumbani Tanzania ili ashirikiane na watanzania katika kuleta maendeleo ya wananchi na laa hasha hajaja tz kuganga njaa never ever.
Prof. Anna tibaijuka aliendelea kusema kwa muda wote alioishi ulaya na marekani amejifunza sana siasa za uwazi na ukweli kwani amejikuta kitu anachokijua kiunagaubaga anakitolea ufafanuzi bila woga wala kusita hata kama yupo mbali au kwakutumia cm ya mkonon.
Nimejifunza mengi kwa prof.huyo kwan nakumbuka gazet la raia mwema lilivompigiaga endrew chenge kuhusu sakata la iptl alijib yy yupo bize na hawez jib chochote. Unaona utofaut wa siasa za prof.za uwaz na ukweli na izi zetu za tz! Bravo pfor. And lo
 
We ni kifaranga tu... tunataka MAMA mtu ajitokeze aseme!! Hizo fedha hazijatoka mbinguni kwenda kwa hao unaowashadadia.. Fedha hizo ni kodi zetu sisi watanzania... TANESCO ni shrika la UMMA, linaendeshwa kwa kodi zetu.. Sasa mabwana zako wanashirikiana na hao wabia feki kuingia mikataba mibovu inayotafuna mamilioni yetu!!

Hizo fedha ni za umma, hazijatoka mbinuni!!! Nyama weee!!!!!!
 
unaposema inatokana na kodi zetu hebu tupe ufafanuzi ,Siku hizi BOT inafanya kazi za TRA,? na hiyo kodi ni ipi Vat au kitu,hebu tujuze ndugu usilete matusi na kashfa wengine tunafuatilia habari hii tupate ukweli
We ni kifaranga tu... tunataka MAMA mtu ajitokeze aseme!! Hizo fedha hazijatoka mbinguni kwenda kwa hao unaowashadadia.. Fedha hizo ni kodi zetu sisi watanzania... TANESCO ni shrika la UMMA, linaendeshwa kwa kodi zetu.. Sasa mabwana zako wanashirikiana na hao wabia feki kuingia mikataba mibovu inayotafuna mamilioni yetu!!

Hizo fedha ni za umma, hazijatoka mbinuni!!! Nyama weee!!!!!!

We ni kifaranga tu... tunataka MAMA mtu ajitokeze aseme!! Hizo fedha hazijatoka mbinguni kwenda kwa hao unaowashadadia.. Fedha hizo ni kodi zetu sisi watanzania... TANESCO ni shrika la UMMA, linaendeshwa kwa kodi zetu.. Sasa mabwana zako wanashirikiana na hao wabia feki kuingia mikataba mibovu inayotafuna mamilioni yetu!!

Hizo fedha ni za umma, hazijatoka mbinuni!!! Nyama weee!!!!!!
 
Back
Top Bottom