Fei Toto kukata rufaa rasmi CAS aomba mchango wa pesa kwa Watanzania

Fei Toto kukata rufaa rasmi CAS aomba mchango wa pesa kwa Watanzania

Nafikiria kwa namna tofauti. Kwanza kwanini TFF wameshindwa kumpatia haki yake ndugu Feisal ( Yawezekana kuna vipengele havipo sawa...???). 2.Kama CAS mahakamani ya usuluhishi ya mpira ndugu Feisal anaamini itampatia haki yake,kwanini asiwaombe wao wampunguzie au wamtolee gharama zote za kufungua jalada (Mfano Watz wakamchangia uko CAS alafu bado ikaonekana TFF wapo sawa kwa maamuzi yao...).
 
WATANZANIA NAOMBA MNICHANGIE - FEISAL

Kupitia mtandao wa instagram mchezaji wa Yanga Feisal Salum amepost akiomba wapenda soka Nchini kumchangia ili apate fedha zakufungua kesi Mahakama ya kimichezo CAS dhidi ya klabu yake ya Yanga

Kiasi kinachohitajika ni zaiai ya milioni 55View attachment 2634537
Acha nimchangie hii hele yangu niliayotaka kumpa mhindi
 
Inawezekana swali la ulitoa wapi pesa wanaomwezesha hawataki aulizwe.🙂

Sasa Yanga wangesema wanataka Tsh ngapi watu wangepima wachange kwa ajili ya kesi au wailipe Yanga.
 
0F783C7B-9343-492E-A10E-728F0AA9A446.jpeg
 
"KUTOKA KWA SHABIKI"

Sitachanga ila siwapangii watu pa kupeleka pesa zao. Mtu katafuta pesa yake kwa shida kwanini nimpangie? Achange tu. Kila mtu apambane na hali yake. Kwani Fei angebaki Yanga kwa adabu na nidhamu kingeongezeka nini kwenye akaunti yangu mpaka nifanye kampeni asichangiwe? Tukutane fainali, Mpira burudani.
 
Aliyekimbia mshahara wa mil 4 anawaomba walala hoi wa instagram wamchangie pesa za kupeleka kesi CAS;

===

View attachment 2634845
Picha: Feisal Salum (Fei Toto)

Feisal Salum katika ukurasa wake rasmi wa Instagram ameandika ujumbe ufuatao:

Ndugu zangu Watanzania na familia yote ya soka kwa Bara na visiwani. Mimi kijana wenu ambaye kwa miaka yote nimekua na nidhamu nje na ndani ya uwanja na kwa dhati nimeitumikia klabu ya Yanga na Timu ya Taifa ya Tanzania na Zanzibar Heros.

Utiifu wangu umekua shubiri ya maisha yangu ya soka, nimevumilia nimeshindwa, sitamani tena mama yangu kutukanwa. TFF imeshindwa kunisaidia kupata haki yangu ya Kuvunja mkataba na Yanga hivyo nimeamua Kwenda Mahakama ya michezo CAS.

Nahitaji Mchango wa kila Mtanzania mpenda haki na maendeleo ya wachezaji wa Kitanzania ambao wamekua kimya na woga juu ya maslahi, Heshima na Haki zao. Naomba unichangie kadiri utakavyoweza ili niweze kupata pesa ya Kulipia gharama za kufungua Jalada la kesi yangu CAS ili kupata Haki yangu ya Kuondoka Yanga kwa kuvunja mkataba.

Tafadhali naomba unichangie ili nipate haki yangu itakayoniwezesha kutumikia kipaji changu na Timu za Taifa (Tanzania na Zanzibar) katika namna tofauti kwa manufaa yangu na Taifa. Shangazi Fatma Karume na wanasheria wengine watafanya kazi Bure.
SOMENI KUHUSU TOFAUTI YA 'uncertainty VS. uncertainty inherent'
 
Yeye achangiwe tu aende CAS na huko tutamnyoosha, safari hii tunataka aje na walimu wake amewashikilia mikono atwambie kuwa hawa ndiwo wanaonipotosha.
 
Maaskini Makolo

Maaskini Fei Toto

Mbona mnahangaika sana?
 
Back
Top Bottom