Fei Toto ni mchezaji wa kigeni, Yanga ilifuata kanuni?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Feisal Salum Mchezaji wa Yanga leo nimegundua kumbe alikuwa anacheza kwenye Ligi ya Nchi ya Zanzibar ambayo pia ni mwanachama wa CAF. Kwa mujibu wa Kanuni za CAF mchezaji anapotoka Ligi ya nchi moja kwenda ligi ya nchi nyingine, hutakiwa kuwa na uhamisho wa Kamataifa kwa mchezaji kama huyo.

Jee Yanga ilimhamisha Feisal Salum kimataifa na kuijulisha CAF kwamba mchezaji huyo alikuwa anacheza kwenye Ligi ya nchi ya Zanzibar?
 
Namimi naomba kuongezea kwa kukuuliza je lini uliona timu ya taifa ya Zanzibar ikishiriki michuano ya Afcon? kwanini tusianzie na timu ya taifa stars ambayo inamchezesha Fei toto ambae ni raia wa kigeni kwenye michuano ya Afcon?
 
Acha uchochezi

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
Leo KMKM ya nchi ya Zanzibar ilikuwa inacheza na timu ya Al Ahli Tripoli kwenye Mashindano sawa na Simba na Yanga. Kimantiki Zanzibar ina hadhi sawa na TFF kwenye mashindano haya ya CAF na uanachama wa CAF.

Kwa ivo Ligi iliyoitoa KMKM ndiyo ligi aliyokuwa anacheza Feisal Salum, kwa CAF, Ligi ya Tanganyika na Zanzibar ni Ligi mbili tofauti.

Jee Yanga ilifuata Kanuni za kuhamisha wachezaji wa kimataifa?
 
Namimi naomba kuongezea kwa kukuuliza je lini uliona timu ya taifa ya Zanzibar ikishiriki michuano ya Afcon? kwanini tusianzie na timu ya taifa stars ambayo inachezesha raia wa kigeni kwenye michuano ya Afcon?
KMKM inashiriki Ligi ya mabingwa kutokana na Ligi inayoendeshwa na TFF? TFF na ZFA ni vyama viwili tofauti vya mpira na ligi zao ziko tofauti na vilabu tofauti na kanuni za kuziendesha ligi hizo ni tofauti.
 
Nimekuuliza swali kama Zanzibar ni mwanachama kamili wa CAF kwanini timu ya taifa haushiriki michuano ya Afcon wala kombe la dunia?
Na kwanini Feitoto awepo kwenye timu ya taifa ya Tanzania ambapo timu hiyo huwa ipo chini ya TFF?
 
Sina uelewa na timu za taifa. Ila kwa vilabu mchezaji ni lazima anapotoka Ligi ya nchi moja kwenda nchi nyingine ni lazima afanyiwe uhamisho wa kimataifa.

Hivi Zanzibar hawana timu ya Taifa na huwa inashiriki mashindano gani? Nilishawahi kuona Timu ya Zanzibar inacheza na timu ya Tanganyika. Ikicheza Tanganyika na Zanzibar Fei toto anaweza kucheza Tanganyika?
 
Punguza stress

Sent from my CPH2059 using JamiiForums mobile app
 
Nilijua migogoro na kero za Muungano zipo kwenye siasa tu, kumbe Hadi kwenye soka?
Aisee!! Hii nayo kumbe ni Kero??

Zanzibar wana ligi yao na Tanganyika wana ligi yao. Ligi ya kule mwiko kudhaminiwa na makampuni ya pombe huku kwetu TBL ilishawahi kuwa mdhamini mkuu wa Ligi ya Tanganyika. Kwa ivo Yanga ilifuata Kanuni?
 
Sina uelewa na timu za taifa. Ila kwa vilabu mchezaji ni lazima anapotoka Ligi ya nchi moja kwenda nchi nyingine ni lazima afanyiwe uhamisho wa kimataifa.

Hivi Zanzibar hawana timu ya Taifa na huwa inashiriki mashindano gani? Nilishawahi kuona Timu ya Zanzibar inacheza na timu ya Tanganyika. Ikicheza Tanganyika na Zanzibar Fei toto anaweza kucheza Tanganyika?
Ungeanza kwanza kwa kuwa na uelewa mpana juu ya hali ya uanachama wa Zanzibar katika shirikisho la soka Africa ndipo ungekuja na hii mada. Sasa tunajadili nini wakati hujui hata kwanini Zanzibar timu yao ya taifa haishiriki kombe la dunia wala AFCON. Unashindwa kwanini Feitoto huyo huyo yupo kwenye timu ya taifa inayosimamiwa na TFF badala ya ZFA
 
HHu
Feisal Salum Mchezaji wa Yanga leo nimegundua kumbe alikuwa anacheza kwenye Ligi ya Nchi ya Zanzibar ambayo pia ni mwanachama wa CAF. Kwa mujibu wa Kanuni za CAF mchezaji anapotoka Ligi ya nchi moja kwenda ligi ya nchi nyingine, hutakiwa kuwa na uhamisho wa Kamataifa kwa mchezaji kama huyo.

Jee Yanga ilimhamisha Feisal Salum kimataifa na kuijulisha CAF kwamba mchezaji huyo alikuwa anacheza kwenye Ligi ya nchi za Zanzibar?
Huyu huenda akawa bin kazumari, eti umakoloni anategenewa na ni mbeba maono wao.
 
Aisee!! Hii nayo kumbe ni Kero??

Zanzibar wana ligi yao na Tanganyika wana ligi yao. Ligi ya kule mwiko kudhaminiwa na makampuni ya pombe huku kwetu TBL ilishawahi kuwa mdhamini mkuu wa Ligi ya Tanganyika. Kwa ivo Yanga ilifuata Kanuni?

Sijajua unatafsiri vipi keto, nilimaanisha baadhi ya mambo yenye utata kuhusu Muungano nilijua yanapigiwa kelele tu, kumbe hata kwenye soka napo Kuna sintofaham?

Kila kitu kungekua sawa, huu uzi usingekuwepo
 
Nilikuelewa ilikuwa namna ya kuchagiza tu. Ni KERO na watu wanataka ionekane ni sawa. Ligi ziko mbili na zinasimamiwa na vyama viwili vya mpira. Mgao unaoliliwa ni wa FIFA siyo CAF.
 
Back
Top Bottom