Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
- Thread starter
- #21
Wewe umesoma kiupandupande. Najua hayo mambo na najua kuwa ZFA iliomba tena kwa bidii kuwa mwanachama wa FIFA na ikakataliwa kwa kigezo kwamba si nchi inayotambulika kimataifa kwa kuwa na mipaka yake.Ungeanza kwanza kwa kuwa na uelewa mpana juu ya hali ya uanachama wa Zanzibar katika shirikisho la soka Africa ndipo ungekuja na hii mada. Sasa tunajadili nini wakati hujui hata kwanini Zanzibar timu yao ya taifa haishiriki kombe la dunia wala AFCON. Unashindwa kwanini Feitoto huyo huyo yupo kwenye timu ya taifa inayosimamiwa na TFF badala ya ZFA
Zanzibar inatambuliwa CAF kama mwanachama mshirika na ingawa haina sifa kama Tanzania (kwa Timu za Taifa) lakini ligi yake ya vilabu ina sifa kama Ligi ya vilabu ya Tanganyika. Kwa ivo linapokuja suala la Ligi ya vilabu, Zanzibar inajitegemea.
Kujitegemea kwake ndiyo maana zile nafasi mbili za Klabu Bingwa (Simba na Yanga ) na zile mbili za Shirikisho (Azam na Geita Gold FC), haziwahusu Zanzibar bali zinazihusu timu za Tanganyika Pekee. Leo KMKM ikiongeza nafasi zitakuwa ni za Zanzibar peke yake, Tanganyika haitahusika.
Yanga ilifuata Kanuni?