Kuna mambo yaki muungano hayapo sawa na tatizo halipo kwa Yanga bali tatizo linaanzia kwenye katiba yetu kisha inakuja mpaka kwa TFF.
- mtu kutoka Zanzibar ni ruksa kuja Tanzania kufanya kazi ya aina yoyote ile bila kibali
- Ni ruksa kumiliki ardhi bila ya kuwa sharti lolote
- Ni ruksa kuwa raia wa Tanzania bara ili mradi tu upo Tanzania bara.
Ni ruksa ruksa tu,
Wakati upande wa Zanzibar wametuwekea sheria kali watu wa Tanzania bara a.k.a machogo.
Hili ni kosa la kikatiba, na sio Yanga tu bali ni timu zote zinazoshiriki ligi kuu Tanzania bara hakuna mchezaji wa Zanzibar aliyekatiwa kibali. Simba wana Ally Salim pia, shida ni mfumo wetu wa katiba imewachukulia kama wazanzibar kama ni sehemu yetu japo wao wazanzibar hilo ujinga kwa nchini kwao hawataki kuusikia.
TFF nao ikaja kuchukua mfumo huo huo wa mapungufu ya kikatiba hivyo imebariki huo muingiliano wa wachezaji kutoka Zanzibar kutokana na hali ile ile iliyokuwepo kikatiba.