Fei Toto ni mchezaji wa kigeni, Yanga ilifuata kanuni?

Fei Toto ni mchezaji wa kigeni, Yanga ilifuata kanuni?

Leo KMKM ya nchi ya Zanzibar ilikuwa inacheza na timu ya Al Ahli Tripoli kwenye Mashindano sawa na Simba na Yanga. Kimantiki Zanzibar ina hadhi sawa na TFF kwenye mashindano haya ya CAF na uanachama wa CAF.

Kwa ivo Ligi iliyoitoa KMKM ndiyo ligi aliyokuwa anacheza Feisal Salum, kwa CAF, Ligi ya Tanganyika na Zanzibar ni Ligi mbili tofauti.

Jee Yanga ilifuata Kanuni za kuhamisha wachezaji wa kimataifa?
Kiufupi ni muungano wa kulazimishana ndo unapeleka haya.
 
Na hii nadhani itavihusu vile vilabu vyenye wachezaji wa nchi ya Zanzibar kweny vilabu vyetu, je Ile idadi ya wachezaji 12 wakigeni inahusisha na hawa wa nchi ya Zanzibar? Maana naona timu zimesajili wachezaji 12 kutoka mataifa yakigeni huku wakisahau kama wale wazanzibar pia ni wachezaji wakigeni.. Mbona timbwili ni kubwa sana hili mkuu
 
Na hili ni kosa la kuchukulia mambo kikawaida (For Granted). TFF wanaidharau ZFF nakuona kwamba ni kama chama cha mpira cha mkoa. Lakini mbele ya CAF, TFF na ZFF zote zina hadhi sawa!!
 
Feisal Salum Mchezaji wa Yanga leo nimegundua kumbe alikuwa anacheza kwenye Ligi ya Nchi ya Zanzibar ambayo pia ni mwanachama wa CAF. Kwa mujibu wa Kanuni za CAF mchezaji anapotoka Ligi ya nchi moja kwenda ligi ya nchi nyingine, hutakiwa kuwa na uhamisho wa Kamataifa kwa mchezaji kama huyo.

Jee Yanga ilimhamisha Feisal Salum kimataifa na kuijulisha CAF kwamba mchezaji huyo alikuwa anacheza kwenye Ligi ya nchi ya Zanzibar?
Kimenuka !!
 
Mkuu ushauri wangu, baada ya game ya marudiano la Yanga, wasiliana na timu inayopangwa kucheza na Yanga hatua inayofuata uwape ushauri wa kisheria.

Wanaweza kupita hiyo round bila kucheza nao na unaweza kupiga pesa ya kutosha kwa kuwaokolea gharama. Nchi hii tupo nyakati inabidi ujiangalie mwenyewe tu na utafaidikaje na suala zima.
 
Ha! Ha! Ha! Ha! Ha!

Mzee umeiona Fursa!!
 
Timu zilizoko kwenye Ligi ya Zanzibar Msimu wa 2022/2023

1. Malindi

2. Chipukizi FC

3. Dullah Boys

4. Jamhuri Sports Club

5. JKU

6. Kipanga

7. KMKM

8. Kundemba

9. KVZ

10. Mfunzo

11. Mlandege

12. Polisi

13. Taifa Jang'ombe

14. Uhamiaji

15. Zimamoto

16. Black Sailors.
 
Timu zinazoshiriki Ligi ya Tanganyika msimu wa 2022/2023.

1. Yanga

2. Simba

3 Azam

4. Mtibwa Sugar

5. Singida Big Stars

6. Mbeya City

7. Namungo

8. Tanzania Prisons

9. Coastal Union

10 Ruvu Shooting

11. Kinondoni Municipal Council

12. Polisi Tanzania

13. Geita Gold

14. Kagera Sugar

15. Dodoma F.C

16. Ihefu FC
 
Kwa utofauti huo wa Ligi, ni sahihi kwa Yanga kumsajili Fei toto bila ya kufuata utaratibu wa kuhamisha mchezaji toka ligi moja kwenda nyingine??
 
Maelezo ya FIFA kuhusu Uhamisho.

For the purpose of these regulations, the terms set out below are defined as follows:

1. Former association: the association to which the former club is affiliated. (ZFF)

2. Former club: the club that the player is leaving. (JKU)

3. New association: the association to which the new club is affiliated. (TFF)

4. New club: the club that the player is joining. (YANGA)
 
Mkuu unahangaika sana na mjadala wako ila kwa kifupi humu uwezi pata jibu.

We nenda TFF pale na hii hoja yako utapata majibu sahihi ila humu utaleta kila maelezo na hautapata ufafanuzi.
 
Mkuu unahangaika sana na mjadala wako ila kwa kifupi humu uwezi pata jibu.

We nenda TFF pale na hii hoja yako utapata majibu sahihi ila humu utaleta kila maelezo na hautapata ufafanuzi.
Hoja nyingi fikirishi na za maana katika nchi hii huanziaga hapa JF. Na hii tutakomaa nayo hadi kieleweke,tuache kufanya mambo kwa mazoea,lazima sheria na kanuni zifuatwe. Hao TFF hawezi kutoa jibu kwani na wenyewe wamechemsha,hili tunalifikisha CAF ndiyo watanyoosha maelezo na kutoa mwongozo

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Mkuu unahangaika sana na mjadala wako ila kwa kifupi humu uwezi pata jibu.

We nenda TFF pale na hii hoja yako utapata majibu sahihi ila humu utaleta kila maelezo na hautapata ufafanuzi.
Nashukuru kwa ushauri wako.

Niko darasani najifunza kama Fei Toto alihamishwa kihalali toka kwenye Ligi ya Zanzibar.

Halafu hapa sihangaiki kwa kuwa hakuna juhudi ya ziada ninayotumia kuandika hiki ninachoandika. Is Just for Leisure!!
 
Hoja nyingi fikirishi na za maana katika nchi hii huanziaga hapa JF. Na hii tutakomaa nayo hadi kieleweke,tuache kufanya mambo kwa mazoea,lazima sheria na kanuni zifuatwe

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
Kuna mambo yaki muungano hayapo sawa na tatizo halipo kwa Yanga bali tatizo linaanzia kwenye katiba yetu kisha inakuja mpaka kwa TFF.

  • mtu kutoka Zanzibar ni ruksa kuja Tanzania kufanya kazi ya aina yoyote ile bila kibali
  • Ni ruksa kumiliki ardhi bila ya kuwa sharti lolote
  • Ni ruksa kuwa raia wa Tanzania bara ili mradi tu upo Tanzania bara.
Ni ruksa ruksa tu,

Wakati upande wa Zanzibar wametuwekea sheria kali watu wa Tanzania bara a.k.a machogo.

Hili ni kosa la kikatiba, na sio Yanga tu bali ni timu zote zinazoshiriki ligi kuu Tanzania bara hakuna mchezaji wa Zanzibar aliyekatiwa kibali. Simba wana Ally Salim pia, shida ni mfumo wetu wa katiba imewachukulia kama wazanzibar kama ni sehemu yetu japo wao wazanzibar hilo ujinga kwa nchini kwao hawataki kuusikia.

TFF nao ikaja kuchukua mfumo huo huo wa mapungufu ya kikatiba hivyo imebariki huo muingiliano wa wachezaji kutoka Zanzibar kutokana na hali ile ile iliyokuwepo kikatiba.
 
Hoja nyingi fikirishi na za maana katika nchi hii huanziaga hapa JF. Na hii tutakomaa nayo hadi kieleweke,tuache kufanya mambo kwa mazoea,lazima sheria na kanuni zifuatwe. Hao TFF hawezi kutoa jibu kwani na wenyewe wamechemsha,hili tunalifikisha CAF ndiyo watanyoosha maelezo na kutoa mwongozo

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
Sawa ila una uhakika Zanzibar ni mwanachama wa CAF?

Maana inafikirisha kwa upande wa vilabu kupewa nafasi ya kushiriki michuano inayosimamiwa na CAF huku timu yao ya Taifa ikinyimwa nafasi
 
Back
Top Bottom