Fei Toto ni mchezaji wa kigeni, Yanga ilifuata kanuni?

Fei Toto ni mchezaji wa kigeni, Yanga ilifuata kanuni?

Mkuu heshima yako, Zanzibar kwenye CAF ni associate member tu Hana ile full membership status na hii inatokana na kwamba Zanzibar haitambuliki kama nchi kamili bali nchi inayotambulika ni Tanzania

Hivyo Zanzibar kwenye CAF tunasema ni member ambae hana nguvu za moja Kwa moja ingawa ana shirikisho lake la mpira wa miguu ambalo linaitwa ZFA.

Sasa kinachofanya wachezaji wa Zanzibar kuwa huru kucheza Tanzania bara bila kuwa na uhamisho wa kimataifa ni

1. Sababu ya kiuanachama, CAF waligoma kuitambua Zanzibar kama nchi huru Kwa kutumia kigezo cha UN, sasa hii ikapelekea wao kulitambua shirikisho moja tu la mpira ambalo lina uanachama rasmi yaani TFF. Wakasema kwamba haiwezekani nchi moja yaani Tanzania iwe na uwakilishi wa mashirikisho mawili kwahiyo mchezaji kutoka Zanzibar ana Uhuru wa kucheza Tanzania bara bila uhamisho wa kimataifa coz Zanzibar bado haijapata full membership ingawa Wanapewa favour ya kushiriki Inter-club competitions

2. Sababu ya kisiasa, katiba yetu ya Jamhuri ya muungano inaruhusu mkaazi wa Zanzibar kufanya kazi, kumiliki ardhi, na kuishi eneo lolote la Tanzania bara bila kuwa na Vibali vya kwamba yeye ni raia wa kigeni. Hivyobasi katiba inawaruhusu wao kuwa watu huru kabisa wakiwa huku bara kama walivyo wabara wengine kama Wasukuma, Wajita, Wazaramo na makabila mengine mengi

Hivyo mchezaji kutoka Zanzibar ana Uhuru wa kucheza team yoyote Ile ya Tanzania bara bila kuwa na Vibali vya uhamisho kwani katiba inawatambua kama Watanzania na wapo huru kufanya kazi bara
 
Back
Top Bottom