Fei Toto ni mchezaji wa kigeni, Yanga ilifuata kanuni?

Feisal Salum Mchezaji wa Yanga leo nimegundua kumbe alikuwa anacheza kwenye Ligi ya Nchi ya Zanzibar ambayo pia ni mwanachama wa CAF. Kwa mujibu wa Kanuni za CAF mchezaji anapotoka Ligi ya nchi moja kwenda ligi ya nchi nyingine, hutakiwa kuwa na uhamisho wa Kamataifa kwa mchezaji kama huyo.

Jee Yanga ilimhamisha Feisal Salum kimataifa na kuijulisha CAF kwamba mchezaji huyo alikuwa anacheza kwenye Ligi ya nchi ya Zanzibar?
Kahoji pia wachezaji wanaocheza pale Azam kama walifanyiwa uhamisho wa kimataifa kutoka zanzibar ina maana umemuona fei toto peke yake? Amekufanyaje uyo fei toto mpaka umempoint yeye tu
 
Feisal Salum Mchezaji wa Yanga leo nimegundua kumbe alikuwa anacheza kwenye Ligi ya Nchi ya Zanzibar ambayo pia ni mwanachama wa CAF. Kwa mujibu wa Kanuni za CAF mchezaji anapotoka Ligi ya nchi moja kwenda ligi ya nchi nyingine, hutakiwa kuwa na uhamisho wa Kamataifa kwa mchezaji kama huyo.

Jee Yanga ilimhamisha Feisal Salum kimataifa na kuijulisha CAF kwamba mchezaji huyo alikuwa anacheza kwenye Ligi ya nchi ya Zanzibar?
Usichanganyikiwe,[emoji16][emoji1787]

Zanzibar sio Nchi mbele ya TANZANIA

ni Nchi kama kutakuwa na Tanganyika...

ZFA mbele ya TFF ni sawa na DRFA

Kwa Tanzania ligi ya Zanzibar ni kama ligi ya Mkoa..

Zanzibar haina mamlaka kamili, mbele ya Tz...
 
Ngoja nijibu maelezo yako kwa swali.

Jee TFF inapofanya uchaguzi wake huwa kuna wajumbe toka ZFF wanaoshiriki kwenye Uchaguzi wa TFF?

Hapa tunazungumzia Ligi na siyo mamlaka ya kiinchi. Kwa mfano si sawa kwa Feisali Salum kuombewa kibali cha kufanya kazi kwa kuwa yeye ni Mtanzania, lakini Tanzania kuna Ligi mbili zinazoendeshwa na vyama viwili tofauti vyenye mamlaka Kamili kwenye maeneo yao.

Siyo Kweli kwamba ZFF na DRFA ni sawa. DRFA inaweza kutoa timu ikaenda kwenye mashindano ya CAF kama Klabu Bingwa au Shirikisho?

Kusema Zanzibar ni nchi kama kutakuwa kuna Tanganyika, kwani Tanganyika haipo? Kama Tanganyika haipo Waziri Mkuu anafanya kazi kwa niaba ya nani?
 
Kimpira Zanzibar haitambuliki kama nchi inayojitegemea. Na ndio maana FIFA iliwanyima uanachama, sio kwamba haiwezekani kupewa uanachama hapana inawezekana ila ni TFF ndio wanaopaswa kuwapa mamlaka kamili ZFA katika shirikisho la soka FIFA. Likishafanyika hilo ndipo utaona ulichokisema kitafanikiwa kikanuni na kisheria. Ila kwasasa ZFA haitambuliki FIFA bali inayotambulika ni TFF kama ndiyo iliyoibeba Tanzania kwa ujumla.
 
Katiba ya TFF ibara ya 12, imetaja wanachama wake kama ifuatavyo;

1. Vyama vya Mpira vya mikoa

2. Vilabu vya Ligi Kuu ya Tanzania (Ikimaanishwa Tanganyika)

3. Chama cha Mpira wa miguu kwa wanawake.

4. Chama cha wacheza mpira Tanzania (SPUTANZA).

5. Chama cha makocha Tanzania (TAFCA)

6. Chama cha marefarii Tanzania (FRAT)

7. Chama cha utabibu michezoni (TASMA)

Hao ndiyo wanachama wa TFF.
 
Kimpira Zanzibar haitambuliki kama nchi inayojitegemea. Na ndio maana FIFA iliwanyima uanachama, sio kwamba haiwezekani kupewa uanachama hapana inawezekana ila ni TFF ndio wanaopaswa kuwapa mamlaka kamili ZFA katika shirikisho la soka FIFA. Likishafanyika hilo ndipo utaona ulichokisema kitafanikiwa kikanuni na kisheria. Ila kwasasa ZFA haitambuliki FIFA bali inayotambulika ni TFF kama ndiyo iliyoibeba Tanzania kwa ujumla.
Kwanza hapa naona unachanganya madesa. Nazungumzia uanachama wa Zanzibar CAF na siyo FIFA. nchi zote za Afrika zinatakiwa kuwa wanachama wa CAF ambayo yenyewe ni mwanachama wa moja kwa moja wa FIFA.

Kimantiki Ligi ya Zanzibar inatakiwa itambuliwe na CAF na siyo FIFA. CAF wanaitambua Ligi ya Zanzibar kwamba ni tofauti na Ligi ya Tanganyika na ndiyo maana wameamua kuipa Zanzibar uwakilishi kwenye mashindano yake.

Kama kuna Ligi mbili tofauti zinazotambuliwa na CAF basi bila shaka hizo Ligi si moja. Kwa mfano Wawa na Kagere wote si watanzania, lakini kuhama kwao toka Simba kwenda Singida Big Stars hakukuhitaji uhamisho wa kimataifa kwa kuwa bado wamo kwenye Ligi ile ile waliyokuwemo wakati wakiwa Simba.

Kwa Kagere na Wawa watasimama kucheza kama vibali vyao vya kufanya kazi vikiisha muda wake kwa kuwa wao si watanzania. Lakini Feisal Salum yeye haitaji kibali cha kufanya kazi kwa kuwa ni Mtanzania. Kinachotakiwa ni yeye kuhamishwa toka Ligi ya Zanzibar kuja Tanganyika.

Yanga ilifuata huo utaratibu?
 
Mkuu kwani Yanga wamemsajili feitoto kutoka ligi ya Zanzibar? Au wamemsajili kutoka humu humu kwenye ligi ya Tanganyika?
 
Mtu kashiba makande huko anakuja kuandika upopoma hapa JF kisa tu ana uhuru wa kuandika anachojiskia
 
Wewe sasa tunaongea Lugha moja. Kwamba mchezaji akisajiliwa toka Ligi ya Zanzibar anahitaji uhamisho wa kimataifa. Kwa kuwa Feisal Salum alisajiliwa na Yanga toka timu ya Jeshi la Uchumi Zanzibar ( JKU ) basi anahitaji uhamisho wa kimataifa.

Yanga ilifuata utaratibu huo??
 
Mtu kashiba makande huko anakuja kuandika upopoma hapa JF kisa tu ana uhuru wa kuandika anachojiskia
Kwa nini ni upopoma ndugu yangu. Huwezi kusema Kichina siyo Lugha kwa tu wewe hukijui. Huu upopoma nimeanza kuandika toka jana mpaka leo jibu halijapatikana.

Yanga ilifuata taratibu za CAF kumhamisha Feisali Salum toka Ligi ya Zanzibar??
 
Wewe sasa tunaongea Lugha moja. Kwamba mchezaji akisajiliwa toka Ligi ya Zanzibar anahitaji usajili wa kimataifa. Kwa kuwa Feisal Salum alisajiliwa na Yanga toka timu ya Jeshi la Uchumi Zanzibar ( JKU ) basi anahitaji uhamisho wa kimataifa.

Yanga ilifuata utaratibu huo??
Mkuu mbona naskia Singida United ndio walimsaini uyo feitoto kutoka JKU Kisha wakawazawadia Yanga huyo mchezaji..
 
Singida haikuwahi kumsajili Fei toto bali walitangaza kumsajili Fei Toto. Meneja wa Fei toto, Mohammed Kombo alikataa Feisal asisajiliwe Singida kwa kuwa hawakufuata taratibu. Feisal Salum hakuwahi kusajiliwa na singida United.
 
Oook.. kwaio mkuu ikionekana Yanga hawakufata taratibu za kumuhamisha huyu mchezaji wa nchi ya Zanzibar, kanuni za caf zinasemaje?? Zalan wapewe point zao na Yanga wanatakiwa wafungiwe kushiriki michuano ya caf Kwa kipindi gani??
 
Kwa nini ni upopoma ndugu yangu. Huwezi kusema Kichina siyo Lugha kwa tu wewe hukijui. Huu upopoma nimeanza kuandika toka jana mpaka leo jibu halijapatikana.

Yanga ilifuata taratibu za CAF kumhamisha Feisali Salum toka Ligi ya Zanzibar??
Yanga haikufuata utaratibu wa CAF kwa sababu haukuwepo huo utaratibu wa kufuatwa kutokana na u peculiar wa kesi yenyewe.
Huyo Feisal Salum ingetokea kusajiliwa na timu ya nje ya Tanzania akitokea JKU ya Zanzibar bila shaka TFF ndio ingehusika na hiyo transfer pamoja na kwamba alikuwa hachezi kwenye ligi inayoisimamia.
Ni mtazamo tu lakini.
 
Oook.. kwaio mkuu ikionekana Yanga hawakufata taratibu za kumuhamisha huyu mchezaji wa nchi ya Zanzibar, kanuni za caf zinasemaje?? Zalan wapewe point zao na Yanga wanatakiwa wafungiwe kushiriki michuano ya caf Kwa kipindi gani??
Tuwaache kidogo utopolo wasonge mbele kidogo halafu tuwachome 🤣😂
 
Oook.. kwaio mkuu ikionekana Yanga hawakufata taratibu za kumuhamisha huyu mchezaji wa nchi ya Zanzibar, kanuni za caf zinasemaje?? Zalan wapewe point zao na Yanga wanatakiwa wafungiwe kushiriki michuano ya caf Kwa kipindi gani??
Utata utaanza kwanza kuangalia, inakuwaje kwenye Taifa moja (Nation) kuna ligi mbili zinazotambuliwa na CAF. Maana Zanzibar ni nchi lakini siyo Taifa.

Utata wa pili ni Taifa la Tanzania kwa nini lina ligi ambayo nchi ya Zanzibar haishiriki? Halafu itaangaliwa ni kwa nini wachezaji watoke Ligi moja kwenda ligi nyingine bila ya Uhamisho wa kimataifa.

Mwisho ni lazima CAF itoe maelekezo ya kuweka taratibu za kimataifa za kuhamisha wachezaji toka ligi moja kwenda nyingine. Au inawezekana pia CAF ikaiondolea kwa mara nyingine tena ZFF sifa ya kuwa mwanachama wake.
 
Yanga haikufuata utaratibu wa CAF kwa sababu haukuwepo huo utaratibu wa kufuatwa kutokana na u peculiar wa kesi yenyewe.
Huyo Feisal Salum ingetokea kusajiliwa na timu ya nje ya Tanzania akitokea JKU ya Zanzibar bila shaka TFF ndio ingehusika na hiyo transfer pamoja na kwamba alikuwa hachezi kwenye ligi inayoisimamia.
Ni mtazamo tu lakini.
"Peculiarity" ya kesi yenyewe ikoje kwani? Maana ZFF si mwanachama wa TFF ni kwa nini TFF basi isimamie mambo ya Ligi ya Zanzibar?

Yaani TFF isimamie maslahi ya Mchezaji ambaye hachezi kwenye ligi yake, KWA NINI?
 
Nimekuuliza swali kama Zanzibar ni mwanachama kamili wa CAF kwanini timu ya taifa haushiriki michuano ya Afcon wala kombe la dunia?
Na kwanini Feitoto awepo kwenye timu ya taifa ya Tanzania ambapo timu hiyo huwa ipo chini ya TFF?
Taifa Stars - zenji na tz bara

Kilimanjaro stars/boys - kama sikosei hii ndio ilikuwa ya Tanganyika tu, Zanzibar walikuwa wanashiriki pia michuano ya kimataifa

Utata utaanza kwanza kuangalia, inakuwaje kwenye Taifa moja (Nation) kuna ligi mbili zinazotambuliwa na CAF. Maana Zanzibar ni nchi lakini siyo Taifa.

Utata wa pili ni Taifa la Tanzania kwa nini lina ligi ambayo nchi ya Zanzibar haishiriki? Halafu itaangaliwa ni kwa nini wachezaji watoke Ligi moja kwenda ligi nyingine bila ya Uhamisho wa kimataifa.

Mwisho ni lazima CAF itoe maelekezo ya kuweka taratibu za kimataifa za kuhamisha wachezaji toka ligi moja kwenda nyingine. Au inawezekana pia CAF ikaiondolea kwa mara nyingine tena ZFF sifa ya kuwa mwanachama wake.
Kwa maelezo yako nadhani TFF ndio Wana majibu zaidi kwenye hili kuliko Yanga maana wamewezaji kumsajili mchezaji kweny system yao kama mchezaji wa ndani wakati katoka kwenye ligi ya nchi nyingine??
Kilichofanyika kupeleka majina caf ni formality tu kutokana na ambacho tayari kimefanyika kwenye system ya usajili wa TFF
 
Na CAF kwenye kanuni ya Kumi ya Leseni kwa vilabu Africa, wanasisitiza kuwa mtoa Leseni (Licensor) Kwa Klabu, ambavyo ni vyama vya mipira vya nchi husika, vina wajibu wa kutoa Leseni kwa wapewa Leseni (Licensee) baada ya kujiridhisha kwamba wanastahili.

TFF walijiridhisha kwamba Yanga imetimiza vigezo vya kumtoa Feisal Salum JKU?
 
Back
Top Bottom