Feisal achana na magenge ya wahuni utapotezwa kwenye ramani ya soka, rudi njia kuu

Feisal achana na magenge ya wahuni utapotezwa kwenye ramani ya soka, rudi njia kuu

Mtanzanias

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2021
Posts
1,747
Reaction score
3,725
Kwa akili tu ya kawaida hii kesi ya Feisal ilikuwa wazi sana ata kwa mtu asiyejua sheria na miongozo ya Fifa kwenye mikataba ya wachezaji angeweza kuiamua bila shida.

Ni kichekesho sana unaingia mkataba kulipwa shingi 100 na unasaini mkataba alafu baada ya muda unamuona mwenzako analipwa shingi 300 unaruka kuvunja mkataba ukitaka na wewe ulipwe kama mwenzako🤣🤣🤣 pasipo kufata utaratibu wowote ule ni ajabu sana, Mwajiri wako uwezi kumlazimisha akuongeze malipo kienyeji wakati mkataba uliosaini unakubana, Apo unatakiwa ujilaumu wewe na yule anayekusimamia kipindi mnakubaliana masuala ya malipo, Yule anaelipwa shingi 300 alisimamiwa vyema kwenye maslai yake ndio maana analipwa iyo 300 tofauti na wewe.

Kilichotakiwa ni kuomba mwajiri kama anaweza mkae kuuboresha mkataba husika na sio kumlazimisha kufanya ivyo kwakuwa yeye ndiye aliyeshika mpini na wewe umeshika makali, Sasa kijana feisal aliingia mkenge akakutana na genge la wahuni wanataka wamdake kwa gharama ndogo na yeye bila kufikiria akaingia chaka, Kamati imeamua vyema kwa maana iyo Yanga ndiye atakaeamua imuuze ama laah.

Timu zinazomtaka ziende mezani kwa yanga watajiwe dau lake biashara ifanyike na sio kufanya mambo ya kihuni kihuni kama ayo, Ingekuwa ivyo mpira usingechezeka ingekuwa kila mchezaji anavunja mkataba anavyoweza anasepa anakokujua
 
Weka Aya mkuu ,mbona upo speed sana?

Fei ana wazazi na ndugu zake wanamtegemea.
 
Uyu Feisal madalali wamesha mvuruga, anahitaji ushauri nasaha Ili akae sawa.
Wakifanya utani anaweza asiweze kufikia kiwango alicho kifikia Sasa.

Majamaa yaliyo mvuruga yata mfariji sikumbili tatu na kusepa.
Wazazi na Ndugu wanatakiwa wawe makini sana na kijana wao amesha lishwa maneno mengi sana.
Maneno ni sumu kubwa, ajizuie ku post chochote mitandaoni anaweza jikuta anaharibu mustakbali wake katika soka.
 
Kwaiyo wakimtegemea ndio asifate utaratibu?
Kama anataka kuwa huru sana basi akauze karanga lakin ukitaka kuajiriwa lazima ufate taratibu
Wakati anatia sahihi huo mkataba hayo ya ndugu na wazazi hakuyajua? Hebu punguzeni uchawa wenu.
Si aliwalipa maboss wake kiasi kinachotajwa ktk kipengele cha kuvunja mkataba wakakirudisha?

Angekuwa anaomba kuondoka bila malipo mngemsumbua sana lkn ametekeleza masharti ya mkataba wake.

Muacheni aondoke hana expectations yoyote na taasisi yenu.
 
Uyu Feisal madalali wamesha mvuruga, anahitaji ushauri nasaha Ili akae sawa.
Wakifanya utani anaweza asiweze kufikia kiwango alicho kifikia Sasa.

Majamaa yaliyo mvuruga yata mfariji sikumbili tatu na kusepa.
Wazazi na Ndugu wanatakiwa wawe makini sana na kijana wao amesha lishwa maneno mengi sana.
Maneno ni sumu kubwa.
Wale waliompa zile milioni 112 za kuvunja mkataba awarudishie pesa zao ili wazikusanye waongeza milioni 800 nyingine waje wauziwe feisal kiroho safi waache mambo ya kihuni kwenye soka
 
Wale waliompa zile milioni 112 za kuvunja mkataba awarudishie pesa zao ili wazikusanye waongeza milioni 800 nyingine waje wauziwe feisal kiroho safi waache mambo ya kihuni kwenye soka
Biashara ya samaki hiyo sio mpira wa bongo
 
Si aliwalipa maboss wake kiasi kinachotajwa ktk kipengele cha kuvunja mkataba wakakirudisha?

Angekuwa anaomba kuondoka bila malipo mngemsumbua sana lkn ametekeleza masharti ya mkataba wake.

Muacheni aondoke hana expectations yoyote na taasisi yenu.
Sasa kama alifata matakwa ya kimkataba imekuwaje ameshindwa kesi?
 
Kwa akili tu ya kawaida hii kesi ya Feisal ilikuwa wazi sana ata kwa mtu asiyejua sheria na miongozo ya Fifa kwenye mikataba ya wachezaji angeweza kuiamua bila shida, Ni kichekesho sana unaingia mkataba kulipwa shingi 100 na unasaini mkataba alafu baada ya muda unamuona mwenzako analipwa shingi 300 unaruka kuvunja mkataba ukitaka na wewe ulipwe kama mwenzako🤣🤣🤣 pasipo kufata utaratibu wowote ule ni ajabu sana, Mwajiri wako uwezi kumlazimisha akuongeze malipo kienyeji wakati mkataba uliosaini unakubana, Apo unatakiwa ujilaumu wewe na yule anayekusimamia kipindi mnakubaliana masuala ya malipo, Yule anaelipwa shingi 300 alisimamiwa vyema kwenye maslai yake ndio maana analipwa iyo 300 tofauti na wewe, Kilichotakiwa ni kuomba mwajiri kama anaweza mkae kuuboresha mkataba husika na sio kumlazimisha kufanya ivyo kwakuwa yeye ndiye aliyeshika mpini na wewe umeshika makali, Sasa kijana feisal aliingia mkenge akakutana na genge la wahuni wanataka wamdake kwa gharama ndogo na yeye bila kufikiria akaingia chaka, Kamati imeamua vyema kwa maana iyo Yanga ndiye atakaeamua imuuze ama laah, Timu zinazomtaka ziende mezani kwa yanga watajiwe dau lake biashara ifanyike na sio kufanya mambo ya kihuni kihuni kama ayo, Ingekuwa ivyo mpira usingechezeka ingekuwa kila mchezaji anavunja mkataba anavyoweza anasepa anakokujua
Mimi mwenyewe na tamani auzwe tu cha msingi timu inayo mtaka ifuate taratibu.
 
Si aliwalipa maboss wake kiasi kinachotajwa ktk kipengele cha kuvunja mkataba wakakirudisha?

Angekuwa anaomba kuondoka bila malipo mngemsumbua sana lkn ametekeleza masharti ya mkataba wake.

Muacheni aondoke hana expectations yoyote na taasisi yenu.
Kwa hiyo Ana expectation na Makolo fc waliomtanguliza Dubai? Ama kweli aliyezoea vya kunyonga kamwe kuchinja kwake mwiko. Always anavizia kunyonga tu
 
Back
Top Bottom