Feisal achana na magenge ya wahuni utapotezwa kwenye ramani ya soka, rudi njia kuu

Feisal achana na magenge ya wahuni utapotezwa kwenye ramani ya soka, rudi njia kuu

Nimeanza kukusoma tu mpaka pale unapodai hata mtu asiyejua sheria anaweza kuiamua hii kesi, nikajua kumbe huwa nawaelekeza mapoyoyo wasiojua chochote, nikaishia hapo.
 
Alichokifanya fifa walishapiga marufuku, hivi ww kwa mfano yanga waende wamshwishi phiri alafu wampe pesa za kuvunjia mkataba alafu phiri asifuate utaratib unaona tu kaweka hizo pesa kwenye account ya simba!!

Hivi unafikiria Alichokifanya fei ni ni sahihi ? Kama ndo hivo mpira usingechezeka duniani wenye pesa wangekuwa wanafanya tu hivo kirahis kupata wachezaji bora kupitia pesa zao. Fifa waligundua hili na ndomana walikataza.. nchi ina watu wajinga mno na ww ni miongoni mwao
😂😂😂😂
 
Nimeanza kukusoma tu mpaka pale unapodai hata mtu asiyejua sheria anaweza kuiamua hii kesi, nikajua kumbe huwa nawaelekeza mapoyoyo wasiojua chochote, nikaishia hapo.
Huwezi kuendelea maana huu uzi ni mchungu kwa makolo
 
Kwa akili tu ya kawaida hii kesi ya Feisal ilikuwa wazi sana ata kwa mtu asiyejua sheria na miongozo ya Fifa kwenye mikataba ya wachezaji angeweza kuiamua bila shida.

Ni kichekesho sana unaingia mkataba kulipwa shingi 100 na unasaini mkataba alafu baada ya muda unamuona mwenzako analipwa shingi 300 unaruka kuvunja mkataba ukitaka na wewe ulipwe kama mwenzako[emoji1787][emoji1787][emoji1787] pasipo kufata utaratibu wowote ule ni ajabu sana, Mwajiri wako uwezi kumlazimisha akuongeze malipo kienyeji wakati mkataba uliosaini unakubana, Apo unatakiwa ujilaumu wewe na yule anayekusimamia kipindi mnakubaliana masuala ya malipo, Yule anaelipwa shingi 300 alisimamiwa vyema kwenye maslai yake ndio maana analipwa iyo 300 tofauti na wewe.

Kilichotakiwa ni kuomba mwajiri kama anaweza mkae kuuboresha mkataba husika na sio kumlazimisha kufanya ivyo kwakuwa yeye ndiye aliyeshika mpini na wewe umeshika makali, Sasa kijana feisal aliingia mkenge akakutana na genge la wahuni wanataka wamdake kwa gharama ndogo na yeye bila kufikiria akaingia chaka, Kamati imeamua vyema kwa maana iyo Yanga ndiye atakaeamua imuuze ama laah.

Timu zinazomtaka ziende mezani kwa yanga watajiwe dau lake biashara ifanyike na sio kufanya mambo ya kihuni kihuni kama ayo, Ingekuwa ivyo mpira usingechezeka ingekuwa kila mchezaji anavunja mkataba anavyoweza anasepa anakokujua
umekula kande mbichi,pole.
 
Si aliwalipa maboss wake kiasi kinachotajwa ktk kipengele cha kuvunja mkataba wakakirudisha?

Angekuwa anaomba kuondoka bila malipo mngemsumbua sana lkn ametekeleza masharti ya mkataba wake.

Muacheni aondoke hana expectations yoyote na taasisi yenu.
umekula maharage ya wapi wewe?
 
Back
Top Bottom