Feisal ndiyo amewaharibia zaidi wachezaji Wazawa

Mimi ni yanga kabisa. Ila kwenye issue ya Feisal naomba wanayanga wenzangu tuwe watulivu. Tuwe professional.... Tusiwe na mihemko ya kishabiki. Kama mchezaji anaona maslahi yamepatikana sehemu mwache akajitafutie.
Pesa ndo kila ndoto ya mcjezaji(refer CR7).
 
Morrison alipozingua akakimbilia simba akidhani anatukomoa tuliwapata wachezaji waliotufanya tuyasahau madhila aliyotufanyia. So hata Feisal anatoa fursa kwa wachezaji wengine wazuri zaid kuja yanga.
#daima mbele nyuma mwiko!!!
 
Hapo ndo mnapo waharibu wachezaji mkuu ..asicheze ILI kufurahisha watu wakati mpira ni mchezo wa furaha
Kwa hiyo Azam haina mashabiki wa kufurahia soka lake huku na yy akitengeneza maisha yake...
 
Tatizo hapa hakuna anayemwonea dongo Feisal. Shida ni namna anavyotoka na utaratibu alioutumia sio sahihi. Kumtafuta good pasture ni halali yake. Na wabongo tunatereza hapo tunapenda sana shortcuts. Ukiwa mtu wa kufuata taratibu utaheshimika vinginevyo unadharaurika na kuonekana wa hovyo tu.
 
Dunduka fc aka kolo ulivyokosa akili eti wanamdhurumu.kwani ule mkataba ulimsainisha wewe?
 
Kumbe na ww ni kilaza
 
Kati ya morisoniii na feisal nani mswahili?
Vilabu viheshimu wazawa wanaonyesha ubora pasi na shaka.
Sifikiri n muda wa kumlaumu feisali n muda wa kuboresha mazingira ya kazi kwa wazawa pia
 
Fei anadhulumiwa kivip?

Analipwa kulingana na mkataba. Huwez kulipwa kulingana na kiwango chako uwanjani Bali unalipwa kulingana na mkataba
 
sio sahihi kwa misingi ya ubongo wako mdogo ama mkataba waliosaini~toa mwiko uwe na akili
 
Fei anadhulumiwa kivip?

Analipwa kulingana na mkataba. Huwez kulipwa kulingana na kiwango chako uwanjani Bali unalipwa kulingana na mkataba
haya kaacha kazi kwa mujib wa mkataba,sasa wewe mbelemwikonyumamwiko unajichokonoa nini?
 
Vipi lile suala la Motisson na Yanga lilipandisha heshima na hadhi ya wachezaji wa kigenii??
Yanga acheni kutapatapa mwanzo mlisema atakuwa anawaharibia wanzibar wenzake nashangaa juzi tu mmemtambulisha Mudathir Yahaya na Ninja amerudi kikosini.
 
Fei ni mchezaji wa kawaida sana,kilichokuwa kinambeba ni vile vishoot vyake vya kubahatisha
 
Yanga siyo baba yake wala mama yake. Feisal lazima aangalie Maisha yake ya sasa na baadae. Siku Maisha yakimuendea kombo kwa kuendekeza unazi kwa Yanga wewe mwenyewe utakuwa wa kwanza kumchekelea.

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…