Feisal Salum 'Feitoto' arudi tena TFF na Wakili wa Msuva, aomba kuvunja mkataba na Yanga

So what?
Yanga ni waonezi tu, TFF ni makanjanja tu, mwacheni dogo aitafute haki yake hadi uajemi
Mbona kama una hasira. Yanga wanakuwaje waonezi kwa mchezaji waliye mlea kwa miaka chungu nzima! Mchezaji ambaye alikuja akiwa underground, na leo amekuwa star kiasi cha kutamaniwa na kila timu ya ligi kuu ndani ya nchi?

Afuate tu utaratibu ili aondoke bila mushkeli. Hata huyo Jasmini na misifa yake, ataishia tu kuangukia pua. Time will tell. Nimekaa pale 👉 🧔 nasubiria matokeo.
 
Mkataba hauwezi kuvunjwa kwa matakwa ya Yanga.
Utavunjwa kulingana na thamani halisi ya mkataba.
Nani atahakikisha mkataba unavunjwa ipasavyo kama sio TFF?

Ulikuwa unamlipa million nne, afu uje uwaambie watu mchezaji anauzwa Billion?
 
Simba hawakulifumbia macho, usipotoshe watu.View attachment 2539203
Sawaa ila kilichofuata ni nini? Pande zote mbili zililimaliza na maisha yakaendelea. Hilo ndilo post ile inauliza, kinachozuia pande hizi mbili kulimaliza suala lao ni nini?

Yanga hawawezi kuendelea milele kujificha kwenye kivuli cha "aje mezani tuongee". Mkataba umekiukwa, dogo hataki kuendelea kucheza, nini kinafuata? Je akitangaza kustaafu kucheza soka akavue pweza mtaendelea kumtumia mshahara wake?
 
Feisal Salum “Feitoto” atinga tena TFF akiwa na aliyemsaidia Saimon Msuva kushinda kesi CAS. Mara hii amewasilisha barua ya maombi kwa TFF akitaka kuvunja mkataba wake na klabu yake ya YANGA

View attachment 2539157
Hili ndio lilikuwa limebaki, kuna watu wanaona kijana hajui anachofanya mimi naona yuko sawa, kaanza na hatua ya kutingisha timu ya yanga kama wanamuweza ameona ngoma ngumu sasa anataka kuvunja aondoke
 
Mkataba hauwezi kuvunjwa kwa matakwa ya Yanga.
Utavunjwa kulingana na thamani halisi ya mkataba.
Nani atahakikisha mkataba unavunjwa ipasavyo kama sio TFF?

Ulikuwa unamlipa million nne, afu uje uwaambie watu mchezaji anauzwa Billion?
Nani amekwambia Fei anauzwa Billion? au magezeti ya udaku unayosoma kutwa ndio yanakufanya ujione unazijua sana za ndani.
 
Hili ndio lilikuwa limebaki, kuna watu wanaona kijana hajui anachofanya mimi naona yuko sawa, kaanza na hatua ya kutingisha timu ya yanga kama wanamuweza ameona ngoma ngumu sasa anataka kuvunja aondoke
Kuvunja mkataba sio rahisi kama unavyodhani.
 
Aliyekuwa anakula ugali kwa sukari anaweza kweli kumlipa wakili?
amekopa akiwa na uhakika zitarudi na atalipa. Kukopa akiwa anachezea Yanga hakuwa na uhakika wa kulipa, ndo akaamua tu ale ugali na sukari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…