Artifact Collector
JF-Expert Member
- Mar 7, 2019
- 6,617
- 10,205
Maamuzi aliyoyafanya feisal december muda ndo unatuonyesha yalikua yakijinga sana
- Feisal ni kweli analipwa mshahara mdogo ila ni ukweli uliowazi ukitaka kuondoka kihuni vile ni timu chache zinaweza kama angekua ni mtu anayeona mbali angelinda kiwango chake na kukiongeza ili hata mkataba wake ukiisha mwakan anauhakika wa kusign mkataba mnono kulikua hakuna haja ya papara
- Hakuna watu wabaya kama washauri hasa ukiwa kwenye mafanikio- aliyemshauri feisal ni mtu mbaya sana na anatakiwa akemewe kuna muda unaweza jiuliza sisi watanzania tuna gundu nin sababu haiwezekani unaenda hatua muhimu anatokea mtu anakushauri ujinga vile, aliyemshauri feisal ni mtu ambaye ana upeo mdogo na mbinafsi kupindukia
- Yanga hajafuzu nusu fainal ila mpaka sasa hivi ananafasi kubwa sana kwa matokeo aliyoyapata kule Nigeria ila ukiangalia feisal hayupo hii ndo ilikua nafasi yake ya yeye kuonekana lakin hayupo inaumiza sana, watu wanaituhumu Yanga lakini swali la kujiuliza leo Yanga akikubali kirahisi kumwachia feisal eti sababu haipendi Yanga, kuwa na uhakika kesho kutwa atatokea mchezaj mwingine atatumia mbinu zile zile za Feisal