Feisal Salumu: Nimeondoka Yanga kutokana na manyanyaso, nilizungumza na Rais wa Yanga kwa saa 6, nikamwambia nataka kuondoka

Feisal Salumu: Nimeondoka Yanga kutokana na manyanyaso, nilizungumza na Rais wa Yanga kwa saa 6, nikamwambia nataka kuondoka

Nipo upande wake lakini hapo kwenye kutokujua mkataba unasemaje sababu ni wa kingeleza namlaumu. Kwanini asaini dili kubwa kama hii bila kuwa na mtalamu wa hata mambo
bongo wachezaji wengi sana hili linawakuta....
wao huwa wanaamini maneno waliyoambiwa, hawasomi mikataba au hawajui kusoma kingereza (au lugha ya kisheria),
umefika wakati wachezaji waanze kuwa na wawakilishi wao, maana kwa sasa ligi yetu ina pesa!
 
Nipo upande wake lakini hapo kwenye kutokujua mkataba unasemaje sababu ni wa kingeleza namlaumu. Kwanini asaini dili kubwa kama hii bila kuwa na mtalamu wa hata mambo
Ina maana meneja wake hakuusoma mkataba wake??
Sidhani kama aliitwa asaini oeke yake, lazima meneja wake aliupitia kwanza mkataba. Aache wongo.
 

"Niliambiwa na viongozi wa Yanga kuwa nauza mechi iliniuma sana na nikipokuwa nawapigia simu hao viongozi waliokuwa wanatamka hayo maneno hawapokei simu yangu.

"Viongozi walikua wanamtukana mama yangu na kutoa matusi ya kumnyanyasa hata ingekua ni wewe ndugu mwandishi usingekubali kutukaniwa mzazi"


"Kula ugali kwa sukari sikula saivi nilikula kipindi kile timu bado ilikua ipo chini kiuchumi na Kuna muda tulicheleweshewa mishahara lakini Mama aliniambia vumilia mwanangu maana alikua ni mpenz wa mkubwa wa Yanga.

"Mama Kuna muda mwingine alinipa pesa yake tulipokua tumecheleweshewa mshahara."

Mwandishi : tueleze umepitia manyanyaso gani??

"Naambiwa nauza mechi, viongozi wananitukana na nikiwaambia familia wanasema nivumilie.

"Mama yangu alikuja dar wakamtukana na kuanza kumpa maneno ya kejeri."

"Huyo huyo Raisi anatuma watu wamtukane mama yangu wanamuita mama yangu andazi "

Wanitukane Mimi lakini siyo mama yangu maana mama yangu ni pepo yangu"

"Nimekaa masaa sita na Engineer hers kuwa hapa nilipofikia nataka niachane na Yanga na hers alisema kuwa bado anahitaji huduma yangu"

Raisi : anampigia simu mama na mama aliniambia niende kusaini mkataba na mama alimwambia mpe fei mkataba wa miaka miwili"

Hers aliongeza mwaka mmoja badala ya miaka miwili"

"Mimi sijui kiingereza walinipa mkataba wa miaka mitatu"

"Signing fee sijapewa kwa wakati nilipewa kidogo kidogo Tena kwa kutumiana meseji za vitisho"


Huyu dogo boga kabisa, kunakuwaje na connection kati ya Mama yako na Yanga? Ina maana huwezi jisimamia au
 
Walishaongea kabla ya kusaini mkataba kwanza, kwahivyo yale mazungumzo Faisal ndo akayapeleka kwenye mkataba ambapo baadaye yaliyotokea ni kwa Hersi miaka mitatu na kwa Feisal ni miaka miwili.

Alikariri mazungumzo waliongea kabla ya kusaini mkataba wa Kingereza.
Kwahiyo Hersi kamzunguka kijana ama??!!
 
Kwa jinsi dogo anavyozungumza ni wazi kua ana msongo wa mawazo, kina fatma hawakumpanga kuzungumza vizuri lakini pia hamna la maana aliloongea. Sijui hao wanaomsimamia wanafeli wapi
 
Kutokujua sheria, Sio excuse kwako, maana umesaini pasipo kushurutishwa....

Kabla ya kusaini mkataba wowote ule achilia mbali ya michezo.....unakuwa na zaidi ya saa 24 za kusoma mkataba, uuelewe na uridhie kwa hiyari.....

Una haki ya kuchukua mkataba kabla hujausaini na kwenda nao nyumbani ukausoma na uuelewe kisha kesho yake ukaenda kusaini....

SHIDA YETU KUU NI NJAA....!!!!.....kipengele muhimu tunachokiangalia ni Gross pay na Nett pay tu....tunaanguka signature...

Kwa umri wangu mdogo kabisa katika ajira yangu ya kwanza early 2005 kwenye intake ya watu 10....tukiitwa mmoja mmoja Kwa HR kusaini........

Nilimwambia HR aniruhusu nikausome mkataba then nitausaini kesho yake baada ya kuuelewa...

Alitoa copy na akanipa nikaja kusaini kesho yake....
 
Back
Top Bottom