"Niliambiwa na viongozi wa Yanga kuwa nauza mechi iliniuma sana na nikipokuwa nawapigia simu hao viongozi waliokuwa wanatamka hayo maneno hawapokei simu yangu.
"Viongozi walikua wanamtukana mama yangu na kutoa matusi ya kumnyanyasa hata ingekua ni wewe ndugu mwandishi usingekubali kutukaniwa mzazi"
"Kula ugali kwa sukari sikula saivi nilikula kipindi kile timu bado ilikua ipo chini kiuchumi na Kuna muda tulicheleweshewa mishahara lakini Mama aliniambia vumilia mwanangu maana alikua ni mpenz wa mkubwa wa Yanga.
"Mama Kuna muda mwingine alinipa pesa yake tulipokua tumecheleweshewa mshahara."
Mwandishi : tueleze umepitia manyanyaso gani??
"Naambiwa nauza mechi, viongozi wananitukana na nikiwaambia familia wanasema nivumilie.
"Mama yangu alikuja dar wakamtukana na kuanza kumpa maneno ya kejeri."
"Huyo huyo Raisi anatuma watu wamtukane mama yangu wanamuita mama yangu andazi "
Wanitukane Mimi lakini siyo mama yangu maana mama yangu ni pepo yangu"
"Nimekaa masaa sita na Engineer hers kuwa hapa nilipofikia nataka niachane na Yanga na hers alisema kuwa bado anahitaji huduma yangu"
Raisi : anampigia simu mama na mama aliniambia niende kusaini mkataba na mama alimwambia mpe fei mkataba wa miaka miwili"
Hers aliongeza mwaka mmoja badala ya miaka miwili"
"Mimi sijui kiingereza walinipa mkataba wa miaka mitatu"
"Signing fee sijapewa kwa wakati nilipewa kidogo kidogo Tena kwa kutumiana meseji za vitisho"