Feitoto akwama tena TFF, arudishwa Yanga

Kwa hapa ilipo fikia kijana anatakiwa atumie busara ya kawaida tu, akubali kurudi Yanga.
Baada ya hapo, akaongeze bidii na ajinoe vya kutosha ili akafanye maajabu. Maana muda uliobaki ni mchache na pengine hii inaenda kumpa nafasi ya kutazamwa kwa umakini hata kwa tum za nje.
Kijana anatakiwa sasa akalitangaze jina lake kwa kufanya maajabu, na atakua amejipaisha zaidi kisoko, kisoka na uthamani.
 
Wengine Tangu siku ya Kwanza tuliweka ushabiki pembeni na kumshauri afuate sheria. Lakini Mabushlawyer wa Jf na Wachambuzi mchongo wakamkomaza kichwa eti ataahinda. Matokeo yake amebaki kuzurura tu na mwisho amerudishwa huko huko.
 
kiburi si maungwana
yanga wamempa option tatu: 1. kurejea kuitumikia yanga huku mkataba wake ukiboreshwa, 2. kukaa mezani na yanga na kuvunja mkataba, 3. timu inayomtaka kuifuata yanga officially. yote haya hayataki!!! kiburi si maungwana
 
Dogo wamuangalie kwa karibu huyo. Atakunywa sumu ili ajiue
 
Mi ningetafuta sehemu nikae nitulie maana mshahara wananilipa
 
Sheria za mpira wakati fulani ni za kikatili sana... inamaana ukishaingia mkataba na timu hakuna namna tena ya kuvunja mkataba hata kama hutendewi mema au hujapenda mazingira ya timu..... au kwa sababu ya TFF imejaa uoga inapokabiliana na yunga..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…