Feitoto hana tena mahaba ya kuendelea kucheza Yanga

Feitoto hana tena mahaba ya kuendelea kucheza Yanga

Hapo atakaa tu mpaka mwakani mkataba unaisha anaondoka huku mnamlipa.
Ninachoshangaa kwa mashabiki wa Yanga ni kuwa timu yao ikiachwa ni kama laana. [emoji28]
Sasa uwezi kuwapangia namna ya kumtumia waajiri wake maana pesa ni za kwao ata wakimlipa bila kucheza we inakuuma nini? Asipocheza anaikomoa klabu au anajichimbia shimo mwenyewe, Timu gani itakusajili ukiwa chini ya kiwango kwa kukaa bila kucheza mwaka na nusu?
 
Wachukue mpunga upi labda? Kwani wanaomtaka washatuma ofa yao? Au unasemea mpunga upi? Tunachojua hao wahuni waliomuingiza chaka washaogopa ata kunusa pua zao pale jangwani kwakuwa washachafua hali ya hewa wanajua ata wakienda awatouziwa uyo feisal labda klabu toka nje ya nchi ndio imnunue na sio wahuni wahuni waliomvuruga kijana
HIvi zile hela zilizotumwa kweny akaunti zikarudishwa kwa Fei hivi kumbe hawakua na makubaliano mmwanzni kuwa awalipe ee?
 
Wakili Nduruma Majembe amebainisha msimamo wa mchezaji Faisal Salum juu ya sakata lake na waajiri wake, Yanga SC na kueleza kuwa nyota huyo hana tena mahaba ya kurudi na kuendelea kuitumikia klabu hiyo.

Feitoto alihojiwa na wajumbe wa kamati aliweka dhahiri kwamba hakuna uwezekano na hawezi tena kurudi kuichezea ile klabu.

“Mchezaji ameshasema hana mahaba na timu na hawezi kuitumikia" Nduruma Majembe wakili wa feitoto akizungumza kupitia #tbctaifa

Majembe ameongeza kuwa Uamuzi wa Kamati kutoa hukumu kuwa Feitoto arejee kuendelea kuitumikia klabu hiyo ni kitu kigumu kwa Feitoto na kubainisha kwamba labda kama atapatiwa msaada wa kisaikolojia wa kumuwezesha kutamani kurudi.

#KitengeSports
Kurudi kuitumikia Yanga siyo lazima,afuate taratibu aondoke.Huyo wakili naye ni kilaza tu,unawezaje ku argue basing on immaterial issue. Factum probandum hapo ni kufuatwa au kutofuatwa kwa taratibu mambo ya mahaba hayana maana hapa.Mke akikosa mahaba kwa mumewe akaamua kuondoka ndoa inaisha? Jibu ni kwamba haiishi mpaka taratibu zifiatwe.
 
Nimeona mwandiko kama una jazba hivi au macho yangu...
Kama sivyo basi Fei namuonea huruma maana hizi pilika pilika za makesi zitampotezea focus
Shida ya uyu dogo ajui anapambana na nani, kwa akili yake anajua anapambana na Eng.Hersi kumbe anapambana na dola🤣🤣 alishauliwa na watu wazito akae na waajiri wake wayamalize lakini dogo akadondokea mikononi mwa wahuni akajaa upepo sasa nguvu ya Timu ya wananchi inataka imuonyeshe ni kwa nini hii timu ilipigania uhuru wa Tanganyika💪💪💪💪
 
Igeni kwa wakubwa wenu Simba. Dejani aliposema haitaki timu wakamwachia.
Mwachieni Fei haitaki tena timu yenu.
Hata kama umefunga naye ndoa, mke akikuchoka na kuku kataa sio busara kumng'ang'ania.

Kama pesa yenu ya kimkataba kesha warudishia shida iko wapi ?
 
Back
Top Bottom