Feitoto hana tena mahaba ya kuendelea kucheza Yanga

Hapo atakaa tu mpaka mwakani mkataba unaisha anaondoka huku mnamlipa.
Ninachoshangaa kwa mashabiki wa Yanga ni kuwa timu yao ikiachwa ni kama laana. [emoji28]
Sasa uwezi kuwapangia namna ya kumtumia waajiri wake maana pesa ni za kwao ata wakimlipa bila kucheza we inakuuma nini? Asipocheza anaikomoa klabu au anajichimbia shimo mwenyewe, Timu gani itakusajili ukiwa chini ya kiwango kwa kukaa bila kucheza mwaka na nusu?
 
HIvi zile hela zilizotumwa kweny akaunti zikarudishwa kwa Fei hivi kumbe hawakua na makubaliano mmwanzni kuwa awalipe ee?
 
Huyu mwanasheria gani? Nilitarajia aweke vifungu vya mkataba ambavyo vimekiukwa, anakuja kusema mambo ya huruma sijui mahaba
 
Kurudi kuitumikia Yanga siyo lazima,afuate taratibu aondoke.Huyo wakili naye ni kilaza tu,unawezaje ku argue basing on immaterial issue. Factum probandum hapo ni kufuatwa au kutofuatwa kwa taratibu mambo ya mahaba hayana maana hapa.Mke akikosa mahaba kwa mumewe akaamua kuondoka ndoa inaisha? Jibu ni kwamba haiishi mpaka taratibu zifiatwe.
 
Nimeona mwandiko kama una jazba hivi au macho yangu...
Kama sivyo basi Fei namuonea huruma maana hizi pilika pilika za makesi zitampotezea focus
Shida ya uyu dogo ajui anapambana na nani, kwa akili yake anajua anapambana na Eng.Hersi kumbe anapambana na dola🤣🤣 alishauliwa na watu wazito akae na waajiri wake wayamalize lakini dogo akadondokea mikononi mwa wahuni akajaa upepo sasa nguvu ya Timu ya wananchi inataka imuonyeshe ni kwa nini hii timu ilipigania uhuru wa Tanganyika💪💪💪💪
 
Igeni kwa wakubwa wenu Simba. Dejani aliposema haitaki timu wakamwachia.
Mwachieni Fei haitaki tena timu yenu.
Hata kama umefunga naye ndoa, mke akikuchoka na kuku kataa sio busara kumng'ang'ania.

Kama pesa yenu ya kimkataba kesha warudishia shida iko wapi ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…