Felchesmi Mramba: Bwawa la JNHPP ni mara 10 ya bwawa la Kidatu lililojengwa kwa miaka 5

Kwenye ujenzi wowote ule hata kibanda umiza marekebisho ni jambo la kawaida na pengine ndiyo sababu Katibu Mkuu akatoa tahadhari na kwamba hakuna makusudi ya kuchelewesha mradi. Hata hivyo taarifa kwamba ujenzi umefikia asilimia 60 inaongeza matumaini. Tuache kuihukumu serikali kwa kuwa makini, tujaribu kuwa na akiba ya maneno.
 
Bwawa la mtera linaingia mara kumi? Mzee unalifahamu bwawa la mtera lakini??
bwawa la mtera linazalisha megawati ngapi na hilo linalojengwa litazalisha megawati ngapi tuanzie hapo kwanza ndo tujue lipi kubwa na linaingia mara ngapi kwa mwenzie
 

Viongozi waliopo na wanaokuja, wazingatie hili ulilolitoa kama angalizo.
 

unataka Mama akope matrillion? Nimeeleza hapo juu unaweza kopa unavyotaka tatizo miaka 10 ijayo utakua na madeni yaliyo zaidi ya Pato la taifa mtaanza tena kumlaumu ukopaji awamu ya 6? Je unadhani ni sustainable kukopa zaidi ya trillion 20+ ndani ya miaka 10 kwa ajili ya Miradi miwili tu? Hapo Bado tuna Mradi wa zaidi ya trillion 20 wa kuvuna gesi huko Lindi.

Upigaji unakujaje sasa? Kwanini wasihujumu Bomba la gesi maana ndio umeme ni 60% unategemea gesi? Yaani wahujumu 40% itasaidia nini? Kwanini tunapenda conspiracy theories? CCM ni majizi najua ila eti hawataki kukamilisha ujenzi eti Ili watoe mikataba kwa makampuni ya kufua umeme mbona haiingii akilini? Kwanini usiseme haukamiliki sababu wanakula Hela za Mradi?? It makes more sense. Yaani wasile matrillion ya Nyerere Dam ila waje kugawana billion vichache vya PAP??
Umezungumzia Dodoma mahali..., hiyo ni aina ya uthubutu ambayo imempambanua huyu kichaa aliyetokea kuwepo wakati huo, na hili kiukweli kalimaliza. Hutegemei tena serikali kurudi Dares Salaam hata wafanye nini hawa mashetani waliopo sasa hivi.
Issue ni uthubutu au matokeo? Kwahiyo Mama akikopa ajenge daraja kutokea Bagamoyo hadi Zanzibar mtamsifia sababu ya uthubutu pekee?? Dodoma hata airport haijajengwa Bado, ring roads hamna then unasema IMEKAMILIKA? Hivi kwanini nchi tunakosa vipaumbele wamehamia dodoma so what? Kuhamia dodoma Kuna umuhimu kuliko SGR au Nyerere Dam? Hayo Matrillion yaliyotumika kuhamia Dodoma si yangetumika kukamilisha kipande Cha Moro-Dom.

Let's be serious kama taifa
 
Yule alikuwa muongo Sana. Pale ubungo hakuna fyover, kile ni kidaraja cha juu. Flyover ni barabara ya juu yenye km 10 au zaidi.
Na alivowabomolea watu vitega uchumi vyao... Tukaoneshwa ramani tofauti kabisa na kilichojengwa!
Mungu alituamulia aisee!!
 
Matatizo tuliyonayo yanahitaji umakini wa wananchi katika kufanya overhaul ya system nzima!
Si mmeona kwa jiwe? Hamjifunzi tu? Ameenda na ukurupukaji wake nao umemfuata!
We need stronger policy systems not individuals!
 
All in all... JNHP is a mega project. It will take a while and cycles or do undo to finalize and commission!
 
Hawa watu magufuli aliwafukuza sasa samia kawarudisha wanajipanga kuhujumu kukamilika bwawa la nyerere ili waweze kuleta agenda zao za kuiba hela ya umma kwa kupendekeza dili zao za nishati mbadala.
Ratiba ya kumalizika ujenzi haikua imetayarishwa kwa kubahatisha. Tusisahau huyu mramba ni yule magufuli alimtimua kwa kuja na mpango kupandisha bei ya umeme na pia kushirikiana na wengine kuiongezea mkataba kampuni ya iptl kinyume na mpango wa kampuni hiyo kukabidhi mitambo yake tanesco baada ya mkataba wake kumalizika. Agizo la msgufuli lilikua kupunguzwa bei ya umeme kwa siku zijazo sio kuongeza.
Awamu hii ya mama samia imetekwa na wafanyabiashara ambao wanatanguliza maslahi yao binafsi. Bila shaka samia mwenyewe au familia yake ni wafanyabiashara wenye maslahi binafsi.
 
La ethipia sidhani kama project nzima imeisha .. nafikiri ndo kwanza wamejaza maji awamu ya kwanza na inaweza chukua zaidi ya 3 yrs . Hizi project si mchezo. Kujaza maji tu ni miaka achana na kujanga
Bora wewe umejielekeza vyema. Pro JPM wana macho lakini ni vipofu...hawaoni! Wana akili lakini hawazitumii ipasavyo!
Wanapaswa wajue kuwa miradi mikubwa ya umeme wa maji ni hatari zaidi kuliko comfort ya kubofya switch ya umeme.
Mradi ukikamilika sijui maji watayapata wapi kutosha kujaza bwawa ukizingatia kuwa upstream kwenye mito na vijito tayari kina ni changamoto. Na je wakiyaelekeza maji bwawani... national food basket - the Rufiji basin maisha yatakuwaje? Tayari ni magumu within Great Ruaha River ecosystem bila bwawa. Je, bwawa likiwepo maji yatatosheleza mahitaji?
Na kutokana na haya mabadiliko ya tabianchi... ipo siku kutatokea mafuriko ya hatari... watalazimika kufungulia JNHP kuruhusu free flow ya maji... Sasa sijuhi watu wa down stream kama watabaki salama!

Nilimuelewa sana Dr. Slaa... kwamba JPM alijua hana muda mrefu kwa hiyo alijicommit kufanya vitu vingi kwa haraka kusaka legacy. Lakini vingi alivyofanya ni mzigo kwa taifa!
 
1.Kikwete aliacha deni ni trillion 35 so whatever limeongezeka ni la JPM Kiufupi Ame double deni la taifa in less than 6 years!!!

2. Madeni ya private sector hayapo kwenye deni la taifa. Deni la ndani ni kama trillion 20, deni la nje ni zaidi ya trillion 40!! So serikali inadaiwa trillion zaidi ya 60.

3. Unadai madeni/mikopo ya watangulizi. Kama mlirithi Miradi kama Kuhamisha maji ya ziwa Victoria, Upanuzi wa airport, lami nchi nzima, Bomba la gesi na Kinyerezi 1 and 2, mwendokasi n.k basi muwe tayari kurithi na madeni sio mafanikio mnajifanya kuchukua credit afu madeni mnajifanya lawama ni kwa awamu zilizopita.

4.kumbe mnatambua mabadiliko ya thamani ya fedha na inflation? Mbona mlikua mnajisifia mara sijui bajeti imepanda kuliko awamu zote, mara Miradi inayojengwa imezidi uwekezaji wa awamu zote, makusanyo ya TRA yamezidi awamu zote n.k kwani mlikua hamjui kwamba thamani ya pesa enzi za JK au Mwinyi ni tofauti na sasa?? Acheni unafiki aisee.

5. Aliwaletea maji lakini haibadili ukweli kwamba alikopa sana hivyo inaua sustainability ya uchumi wetu maana makusanyo yanaishia kulipa mishahara na riba za madeni. So msijifiche kwenye maji kujustify mikopo ya trillion 30 ambayo mlidai ni pesa za ndani kumbe mnakopa!!!
 
Hapa mchezo huko hivi; pesa tuongeze kwenye mishahara na marupurupu mengine, pia tukamirishe miundo mingine ili tuoneka tunapiga kazi!
Lakini kiukweli watu kufanya kazi kwa ajiri ya vizazi vijavyo hatuna mtizamo huo!
Huyu anayesema bwawa dogo lilitengenezwa ndani ya miaka mitano, hili kubwa haiwezekani likatengenezwa kwa muda mfupi! Ni mwongo sana huyu
 
Hakuna cha ufuasi, hapa ni usimamizi na kukitumia vizuri kinachopatikana, akili zetu ni mgando na kuaminishwa kuwa vitu fulanifulani mpaka wajomba watusaidie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…