diwan anatuhusu wengi kumbe?MI YANGU INAISHIA KUNUNUA MAVITU VYA JIKONI!mwe!\
aibu yangu aibu yangu!
yani hakuna kitu kinakula hela yangu kama shopping ya jikoni!cha
sijui nafanyaje walahi!
diwan anatuhusu wengi kumbe?
ila huu ni ujinga sana sana manake unakuta kwa mwez umekopa nguo za watoto hata pea 6 unashobokea kujaza yumba vitu vya jikoni bila mpango. halafu mwisho wa siku unajikuta hata huko jikon kwenyewe vinavunjika tu manake vinaonekana kama karakana
Nimeona aibu kama unanisema mimi, au unanijua nini ndio unanipa vijembe vya live live?
sijui nianzie wapi kujirekebisha maana najiona too late
Anza kwa kuandika kila unachinunua, kisha fanya tathmini kila wiki.
Mimi nilianza kuandika nikiwa mwaka wa kwanza chuo. Hatari ni kwamba unaweza kuwa bahili wa kupindukia. Baada ya miezi kadhaa kubana matumizi inakuwa sehemu ya tabia. Nakumbuka nilikuwa nakunywa chai na kiporo asubuhi, kisha pasi ndefu hadi nirudi gheto usiku wa saa nne, ndipo tupike tule. Ilifika wakati natumia Tsh. 350,000/- kwa semester nzima (kodi ya chumba, umeme, maji, chakula, stationeries, vocha n.k). Nilikuwa mchumi hata jamaa zangu wa karibu walilijua hilo, ila kwa kuwa ni mwanaume na ni Mchaga,hawakushtuka sana.
hiyo sasa ni zaidi ya kubana matumizi...vidonda vya tumbo vilikukwepa kweli!!?? God forbid kupata mwanaume wa design yako!!
sorry 2 say that! wadada wenye kipato kidogo ndio wanaospend sana, cjui kwa nini tu. angalia hata maofisini utaliona hili, wenye kipato cha chini wanalipuka na pamba kweli, wenye kipato cha juu wapo simple. angalia hata kwa wanasiasa Dr Rose migiro, Dr nagu, Dr Nkya wapo simple hakuna leswig wala makeup, afu angalia dada zangu wengine ambao hata CVs zao hazieleweki, utaona tofauti ni kubwa sana. ladies wenye kipato kikubwa (tsh 2M n above wapo busy kupeleka wtt shule nzuri (hata kama wanaume wao hawalipi fees), kuinvest na kusaidia family zao, ladies wenye kipato cha chini wapo busy na mapochi, viatu, designer clothes, outings etc. mi nafikiri ni akili ndogo tu za sie kina dada
ni kweli kabisa hapa ofisini kwetu wahudumu wanalipuka kuliko hata mabosi wao.
Habari yako mkubwa.Ni ujana, time will tell.