Iliandikwa kuwa ataweka uadui Kati ya huyu Mwanamke na Joka,
Ndio kinachoendelea hapa,
Shetani kikawaida akija Kwa mwanamke huja Kwa mbinu ya kutaka kumsaidia kwenye tatizo Fulani,
Mfano, Hawa wakati anadanganywa na Nyoka, Shetani anataka kumpa msaada Hawa/Eva afanane/awe Kama Mungu, hivyo ili awe Kama Mungu itampasa ale matunda aliyokatazwa asiyale.
Mwanzo 3:1
Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?
Mwanzo 3:2
Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula;
Mwanzo 3:3
lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa.
Mwanzo 3:4
Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,
Mwanzo 3:5
kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.
Mbinu hiyo inatumiwa na watu wote wajanja pale wanapotaka kuwaingia Wanawake.
Ukitaka mwanamke umpige kirahisi mwambie utamsaidia kumuwezesha afanane na Mungu, Kwani Mungu anafananaje,
Kuwa na mamlaka na utawala, ajiongoze, ajitegemee na kumsaidia watoto.
Feminist wamejitahidi kuwa-empower wanawake Kwa lengo la kuzorotesha taasisi ya ndoa ili jamii zisiwe na nguvu.
Kumbuka Mwanamke hata awe empoweed Kwa namna gani hawezi kuitiisha dunia,
Hata Wanawake waliotawala katika falme za nyuma wote walikuwa wanasapotiwa na kikundi Fulani cha wanaume
Lakini mwanamke kama Mwanamke Hana uwezo wa kutawala wanaume ambao hawataki kutawaliwa.
Lakini mwanaume anauwezo WA kutawala wanawake hata Kama hawataki kutawaliwa