Sidhani kama kuna 'idea' mpya kabisa kabisa Msanii anaweza kuja nayo ili awaridhishe watu wa sampuli yako.
Hata nyimbo za wasanii wakubwa duniani, tayari zilishawahi kuimbwa na wasanii wengine kabla yao, tena wao wamepita mulemule -- bora hata ya Fid Q anayeleta mawazo yake kutoka katika 'quotes' za watu -- lakini bado hakimiliki ni zao.
Mifano halisi ni hii michache:
1. Wimbo YOUNG FOREVER wa msanii mkongwe wa Hip Hop nchini Marekani, JAY-Z ulishawahi kuimbwa miaka ya '80 na msanii NASHVILLE, na ukiusikiliza, Jigga amepita mulemule, lakini bado dunia imemtambua SHAWN CARTER @ JAY-Z kwa ngoma yake hiyo.
2. Wimbo maarufu wa MAD WORLD ulioimbwa na msanii GARY JULES ulishaimbwa na SHADE OF TEARS miaka ya nyuma, na ni vilevile 90%. Kwahiyo ni suala la kawaida kabisa.
Kwa hapa Bongo kuna nyimbo kama Siwema, Sina Makosa, nk. zimekuwa 'severely sampled,' NI SUALA LA KAWAIDA KABISA.
Kwahiyo FID Q is still a genious.