Sijaona tatizo lolote lile kwa yeye kusoma vitabu na kurahisisha yale anayoyapata humo kwa njia ya mistari, nilishawahi kumsikia kwenye interview moja akisema yeye anapenda sana kusoma vitabu, ningeshauri na wasanii wengine wajisomee vitabu ili waimbe vitu vinavyoeleweka, pia nikukumbushe mdau, kusoma kitabu au vitabu ni jambo moja na ule ufundi wa kuunganisha hayo mawazo katika mtitiriko unaoeleweka na yakaimbika ni jambo jingine, hivyo tusiwabembeze wasanii wanaojisomea kaka, sijajua pia kama ulitaka kila mwisho wa wimbo pawe na references na ziwekweje.