Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
FIFA World Cup 2026 imeidhinisha mgawanyo wa fedha wa dola milioni 727 (Tsh. Trilioni 1.9) kwa ajili ya mashindano hayo, ambao ni mkubwa zaidi katika historia ya michuano hiyo.
Kati ya kiasi hicho, dola milioni 655 zitatolewa kama zawadi kwa timu 48 zitakazoshiriki, ikiwa ni ongezeko la asilimia 50 ikilinganishwa na Kombe la Dunia lililopita. Bingwa wa 2026 atapokea zawadi ya dola milioni 50.
Aidha, kila taifa litakalofuzu litapokea dola milioni 1.5 kama fedha za maandalizi, hivyo kila shirikisho linaloshiriki litahakikishiwa angalau dola milioni 10.5 kwa ajili ya kushiriki kwenye mashindano hayo.
Uamuzi huo uliidhinishwa na Baraza la FIFA katika mkutano wake uliofanyika Doha, Qatar, kabla ya fainali ya FIFA Intercontinental Cup, huku maandalizi ya Kombe la Dunia la mataifa 48 yakiendelea kwa ajili ya michuano itakayofanyika Marekani, Kanada na Mexico kuanzia Juni 11, 2026.