FIFA inatakiwa kuwaondoa Senegal World Cup kwa mchezo mchafu dhidi ya Egypt

Johnny Sack

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2017
Posts
8,984
Reaction score
19,288
Nimetizama mpira kati ya Senegal vs Egypt, licha ya mchezo mzuri ulioonyeshwa na timu zote lakini mashabiki wa Senegal wametia aibu

Walikuwa wakiwalenga machoni wachezaji wa Egypt na mwanga mkali wa laser kipindi wanacheza na walipokuwa wakipiga penalti

Hili limewaathiri sana wachezaji wa Egypt hasa kwenye upigaji penalti. FIFA haipaswi kuruhusu uhuni huu, Senegal waondolewe au mechi irudiwe bila mashabiki ili kukomesha tabia hii chafu

Yaani leo uwanjani kulikuwa hivi...Dunia nzima imeshangaa

 
Waarabu🤪🤪🤪
 
Wameleta malalamiko kwako?
 
Nikusaidie tu kwa Kukuambia kuwa hakuna Nchi ambayo ndiyo Walimu Wazuri na Waanzilishi wa Fitina zote na Umafia wote ( Kitaalam inaitwa 4-4-2 ) katika Soka la Afrika kama Misri ( Egypt ) na hata hicho ambacho unakiona wamekifanya hao Raia wa Senegal na chenyewe pia Wamejifunza na Kukiiga kutoka kwa Mafarao ( Wamisri ) Wenyewe.

Mkisikia Muosha Huoshwa muelewe!!!!!
 
We jamaa hebu angalia gemu iliyopita japo youtube. Mnapenda kuongea pumba na mnakera kweli kweli. Hicho kitendo walikianzisha misri kule kwao game ya mwanzo. Senegal ni kama wamelipiza kisasi tu. Hata mimi nilihisi fifa wataliongelea hili suala kwenye game ya mwanzo lakini walinyamaza kimya
 

Inasikitisha sana....hapa nacheki game ya Algeria na cameroon, penalty mbili za wazi kwa Algeria
 

Sawa , waandikie FIFA barua , maana hapa JF hutopata msaada wa malalamiko yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…