FIFA irudishe sheria ya kuchomekea, vijana kwenye mpira wamekuwa wahudi sana

Machame Juu

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2013
Posts
1,514
Reaction score
3,363
Kuchomekea shati au tu kochomekea tu ni ishara ya udhanifu na heshima duniani kote. Hilo linafahamika wazi.

Ukiangalia wachezaji wa mpira kabla 2005 kurudi chini walikuwa na heshima, dhanifu sana kwasababu walikuwa wanachomekea jezi.


Lakini baada ya 2005 FIFA walipoivunja sheria ya kuchomekea na kuruhusu wachezaji kutochomekea vijana wachezaji wamekaa kuhuni huni tu hadi hawafanyi vizuri.

FIFA waliangalie hili. FIFA walikataza pia kuvaa herini, mkufu chain hata wrist band na pete. Kabla ya hapo wachezaji walivaa hivi vitu.


Mchezaji pekee maarufu aliyesalia kuchomekea jezi wakati wote ni Rodri wa Manchester city.

 
Sawa Sawa Warudi Tena Kama Zamani Kuchomekea Jezi Ndiyo Wanapendeza Sana
FIFA wamebadilisha sheria nyingi sana. Zamani mchezaji aliweza kumrudishia kipa wake mpira kwa miguu ndani ya 18 akaudaka. Lakini sasa hivi ukifanya hivyo ni free kick. Sheria inaruhusu tu kipa kuudaka kwa kumrudishia kwa kichwa, kifua, goti, paja, mgongo na tako.

Pia zamani kipa aliweza kuudaka kwa mkono mpira nje ya 18. Lakini sheria ikabadilishwa akifanya hivyo ni straight red card.

Zamani makocha waliruhusiwa kuvuta sigara ndani ya uwanja.
 
Joto la dunia limeongezeka, zamani Dar hazikuwepo baa za kukaa nje, zilikuwa ndani na nyingine vyumbani, lakini kwa kuwa kiwango cha joto kilikuwa chini haikuwa shida, ujue hazikuwa na feni, usibishe. Siku hizi hata hapo nje bado hapakaliki sasa mchezaji anayetamani avue jezi unataka achomekee! Mlima Kilimanjaro ile barakashia imelika imebaki utosini kama ya muuza madafu.
 

Dhanifu ni nini?
Halafu hebu leta kifungu cha hizo sheria za FIFA kinachokataza mchezaji kuchomekea kwa sasa!
Ikibidi ulete reference ya kifungu cha sheria kabla ya mabadiliko 2005 kilichoeleza mchezaji anaruhusiwa kuchomekea pia!

Na kama sheria kwa sasa inakataza iweje Rodri aendelee kuchomekea bila kuchukuliwa hatua?
 
Mkuu hapana FIFA haikatazi mchezaji kuchomekea kwasasa l. Ila kabla hapo ilikuwa inakataza mchezaji kutochomekea. Lakini baada ya 2005 ikaruhusu mchezaji anaweza kuchomekea ama kutochomekea. Sasa baada iyo sheria wachezaji wote hawachomekei.
 
Katika mifano yako umemsahau mwamba huyu hapa, Peter Shalulile. Huyu naye anaendeleza utamaduni uliosahaulika.

Ni kweli mchezaji anayechomekea katika zama hizi anaonekana tofauti sana na ni nzuri katika branding yako hasa kama kiwango chako ni kizuri. Iachwe tu uwe uamuzi binafsi maana marefa walikuwa na kazi za ziada kuwaadhibu wasiochomekea kama vile walimu wa shule za msingi.



Juzi juzi nilimuona Clatous Chama amechomekea mazoezini. Pia Augustine Okrah naye mara kwa mara nimemuona akichomekea.
 
Mkuu hapana FIFA haikatazi mchezaji kuchomekea kwasasa l. Ila kabla hapo ilikuwa inakataza mchezaji kutochomekea. Lakini baada ya 2005 ikaruhusu mchezaji anaweza kuchomekea ama kutochomekea. Sasa baada iyo sheria wachezaji wote hawachomekei.

Hivi hili jambo unalozungumzia, limeezwa kwenye sheria 17 za FIFA?
Kama ndio naomba hicho kifungu cha sheria za FIFA kilichokuwa kinakataza kutokuchomekea kabla ya 2005!
Lakini pia ingekuwa vyema ukaleta hicho kipengele kinachoelezea kutokuwa na ulazima wa kutochekea kwa sasa!
 
Sasa huyu shaulile na hili umbo lake hafai kuchomekea, cheki sasa hips na tako zote ziko bampaaaaa,

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Aaaaahaaaa
 
Imechangiwa wachezaji wengi kuvaa milegezo wakina Wawa ,Nyingi ,Diara ,Rojo nk
 
Sasa huyu shaulile na hili umbo lake hafai kuchomekea, cheki sasa hips na tako zote ziko bampaaaaa,

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
πŸ€£πŸ˜‚πŸ€£πŸ˜‚ anapenda nguo zinazobana ili ajihisi anacheza akiwa mtupu πŸ€£πŸ˜‚πŸ€£
 
Sasa huyu shaulile na hili umbo lake hafai kuchomekea, cheki sasa hips na tako zote ziko bampaaaaa,

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
We ndo kitu umeona? Unamtamani?
 
Hii picha ni muhimu katika huu uzi
Shalulile anaujua mpira ..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…