FIFA waja na sheria mpya ya Offside, je hili litavuruga soka au ni bora?

Shirikisho la soka la Kimataifa (FIFA) wamekuja na sheria mpya ya offside ambayo ili mchezaji ahesabiwe alikuwa offside ni lazima awe amempita mchezaji wa timu pinzani kwa mwili wake wote


View attachment 2675466
Safi sana. Hivi ndio inatakiwa sio mtu kazidi kisigino eti offside.

Offside iwe kama ya mpira kuingia golini lazima mpira uvuke mstari.
 
inaharibu ladha ya mpira sheria ilitakiwa ibaki ileile ukizidi hata kidole kibendera kiwe juu, wachezaji wanaovizia wanaharibu sana ladha ya mpira, sheria ya awali iliwafanya wachezaji wawe wabunifu na kujituma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…