FIFA waja na sheria mpya ya Offside, je hili litavuruga soka au ni bora?

FIFA waja na sheria mpya ya Offside, je hili litavuruga soka au ni bora?

TFF wafanye majaribio kwa kuwa na mechi 3 msimu ujao zisiwe na offside. Wazichague hizo mechi randomly, ila ikitokea debi imechaguliwa sijui itakuwaje.

Mpira wetu kivyetuvyetu.
Hivi huoni hata kwa akili ya kawaida tu hilo haliwezekani?mpira utachezwaje hapo?
Si wachezaji karibu wote watang'ang'ania kwenye lango la mpinzani!
 
Hivi huoni hata kwa akili ya kawaida tu hilo haliwezekani?mpira utachezwaje hapo?
Si wachezaji karibu wote watang'ang'ania kwenye lango la mpinzani!
Timu ipi ndio itang'ang'ania na ipi haitang'ang'ania? Huoni kama uwezo wa timu ndio unafanya timu ing'ang'anie langoni Kwa mpinzani na wala haihusiani na offside? Vile vile ni ngumu Wachezaji wote wa timu moja kung'ang'ania langoni Kwa timu nyingine bila mahesabu sababu itakuwa ni raisi wao kufungwa.
 
Bora tu waondoe off side. Itafanya mpira uchangamke na mechi ziwe na Magoli ya kutosha
Mimi pia huwa siwezi kuelewa logic ya offside!! Kazi ya mabeki ni kumkaba mshambuliaji!! Kama wanaona mshambuliaji anasogea mbele zaidi, ni juu yao kumfuata na kumkaba na siyo kumkimbia ili awe offside!! Na mimi ningependa sheria ya offside ifutwe kabisa!! Inatunyima utamu sana!
 
Back
Top Bottom