DSTV wamepandisha Fainali hizi kwenye vifurushi vya juu, ni mashaka tu kwenye vifurushi vya chini, ambapo inakubidi kusubiri zaidi ya saa moja baada ya mechi ili kiona marudio au pengine highlight....
Leo saa 5 asubuhi (saa za Tanzania) kutakuwa na mashindano ya kuwania mshindi wa tatu baina ya Sweden na Australia. Ingawa haya mashindano hayana mvutoa kama mashindano ya kesho ya kumtafuta bingwa, bado nitatoa summary yake kadri nitakavyoweza
Nilikaa mbele ya TV na kusahau kuja kupost updates. Mpira ni mzuri, timu zote zinacheza vizuri sana na zinashambuliana kwa kasi. Hata hivyo kwenye dakika ya 29 hivi Sweden walipata penalty na kufunga bao la kuongoza. Hadi sasa Sweden inaongoza 1-0; hata hivyo kwa jumla Matildas (Australia) wanacheza mpira mzuri sana kuliko Sweden.
Sasa hivi ni ndani ya dakika za majeruhi za kipindi cha kwanza
Kipindi cha pili kimeanza pole pole
Naona kama Matildas hawana moto kama wa huko nyuma. Swedena inacheza kulinda goli lao huku Matildas hawafany mashambulizi ya nguvu, kwa hiyo mpira uko katikati ya uwanja sana
Matilidas wamefungwa bao la pili na sidhani kama watapata pumzi tena.
Mchezo umekwisha kwa ushindi wa Sweden 2-0. Video zitakuja baada ya Fox kuzirusha
Mpira kati ya Uingereza na Spain I umeshaanza. Wanawake hawa wanacheza kwa kasi na ufundi sana. Spain wanashambulia kwa nguvu sana huku Uingereza nayo inajibu mapigo
Mpira ulisimama kidogo wana usalama wako Gia uwanjani. Nadhani kuna stability alikuwa kavamia uwanja. TV haikumulika huko walikuwa wana kwenda hao wanaulinzi
Uingereza hawa na ball control nzuri. Pass zao nyingi zinapotea. Halafu wanarudia makosa yaliyofanywa na Australia ya kurudisha mipira kwenye lango Lao wenyewe.
Hawa spain wanataka matani yote makubwa ya wanawake wakamate wao, u17 wao wabingwa u20 wao mabingwa sasa na hili kubwa wanataka kubeba....kweli wamejipanga vizuri