FIFA Women's World Cup 2023 | Kombe la Dunia kwa Wanawake

FIFA Women's World Cup 2023 | Kombe la Dunia kwa Wanawake

#TeamFrance imetolewa... " Ni masikitiko kwangu"

Sasa wacha nifikilie timu ya kuisupport....

By the way natumai nipo ndani ya wakati kupata bia...😄 Kichuguu
 
#TeamFrance imetolewa... " Ni masikitiko kwangu"

Sasa wacha nifikilie timu ya kuisupport....

By the way natumai nipo ndani ya wakati kupata bia...😄 Kichuguu
Kuna roli liko njiani kukuletea kinywaji. Wakati wa ujana wangu niliwahi kushi sehemu nyingi sana duniani ikiwa Ufaransa, Australia, New zealand na Japan. Siri ninayojua kuhusu wasichana wa sehemu hizo hasa Ufaransa, Australia na Japan walikuwa ni wapenda ngono sana. Kwa hiyo uwanja wa leo ulikuwa na watu wenye kufanana kitabia.
 
Kipindi cha pili England na Colombia kimeshaanza. Timu zote zimeaanza pole pole sana.

England imekuwa inashambulia sana langoni mwa Colombia; golikipa wa Colombia yuko fit sana.

England imepata goli la pili. Sasa hivi wanaongoza 2-1

Baada ya kufunga bao la kuongoza England imeanza kuelemea sana Colombia

Timu zote zinacheza kwa ufundi sana lakini England wanapata advantage kubwa sana kwenye mashambulizi; wako vizuri sana huko.

Colombia iliamka kujaribu kufanya mashambulizi dhidi ya goli la England lakini wamekutana na askari wa zimamoto wazuri sana kutoka england.

Tunaenda dakika za lala salama na Colombia wamekuwa wakali sana lakini England wanasema mtu hafiki kwenye goli lao.

Haya tunaingia dakika za majeruhi sasa. England bado inaongoza kwa 2-1

Hizi dakika za mwisho kweli Colombia imefanya mashambulizi ya kutisha sana lakini Egland wameweka ukuta imara sana


Mchezo umekwisha na England wameibuka kidedea kwa 2-1. Ila timu zote zilicheza vizuri sana wala sikuwa najua kuwa Colombia itaweka ushindani mgumu kama huu, Muda mwingi England ilikuwa inacheza kujilinda tu.

 
Kuna roli liko njiani kukuletea kinywaji. Wakati wa ujana wangu niliwahi kushi sehemu nyingi sana duniani ikiwa Ufaransa, Australia, New zealand na Japan. Siri ninayojua kuhusu wasichana wa sehemu hizo hasa Ufaransa, Australia na Japan walikuwa ni wapenda ngono sana. Kwa hiyo uwanja wa leo ulikuwa na watu wenye kufanana kitabia.
Comment yakusisimua sana hii bila shaka umeipeperusha vyema bendera yamama samia huko
 
weekend hii ni mapumziko kwa wachezaji. Nusu fainali zinaanza tena Jumanne saa 5 asubuhi (saa za Tanzania) baina ya Spain na Sweden. Kwenye mchezo huo Sweden ni Giant na Spain ni Underdog. Lakini kama tulivyoona kwenye mashindano haya, underdogs wamekuwa wanafanya vizuri sana kuliko giants. Kwa hiyo tutegemee Spain iwafedheheshe Sweden?
 
Nakumbusha tena kuwa ndani ya saa tano zijazo, yaani ikifika saa tano asibuhi hii litachewa kabumbu la kukata shoka baina ya Sweden na Spain

Unaweza kuuona mchezo huo live kwa kutumia simu yako; lakini hakikisha una sign up mapema.


Nililtetewa link hiyo na rafiki yangu mmoja kutoka India; meijaribu inaonyesha kuwa unatakiwa kiulipia dola moja (TSh 2500) Sijui kama ni ya kuaminika. Try at your own risk.
 
Zimebaki dakika 30. Tayari nimeshandaa vitu hivi vya kutosha. Ukitaka tuungane kuuangalia mtanange huu
1692084793678.png
1692084962651.png


Vinginevyo, sema nikutumie kwa email.

Haya sasa: timu zimeshingia uwanjani na kubadilishana bendera pamoja na kupeana mikono
 
Spain vs Sweden; kipenga cha kwanza kimepulizwa na mchezo umeanza.

Katika dakika hizi za mwanzo mwanzo Spain wameonekana kuwaelemea Sweden kidogo.

Sina timu ninayoshabikia hapa ila Spain wanaonekana kuwaelemea sana Sweden labda upepo uubadilike huko mbeleni. Sweden walinitoa raha kwa kuiondoa Team USA kwenye mashindano haya kwa technicalities.

Pamoja na Spain kuilemea Sweden, bado timu zote hazishambuliani kabisa. Yaani Spain wanamiliki mpira sana lakini hawashambulii pia.

Mchezo bado haujasisimua kabisa

Umedoda sana. Sweden hawajafika kwenye goli la Spain na Spain nayo imefika golini kwa Sweden labda mara u mbili tu tena kwa udhaifu sana.

Dakika 45 za kwanza zimekwisha sasa tuko kwenye dakika za majeruhi.

Kipindi cha kwanza kimekwisha wala hakikusisimua kabisa. Nia kama walikuwa wanaogopana vile.

Tumeaza kipindi cha pili sasa

Sijaweka updates kwa vile mcehzo umedumaa sana inga ni hivi karibuni tu wameanza kushambuliana lakini siyo kwa nguvu sana.

Spain ilijaribu kusmabulia sana lakini kicks zake zote zilikuwa zinakwenda nje.

Spain wamepata goli la kuongoza. Kuna mcheazji wa Spain anitwa Slam ndiye amefunga bao hilo; watangazaji wanasema ndioye pial aliyewafunga Uholanzi, kwa hiyo anaonekana ni star wa magoli sana.

Sweden wamesawazisha mara moja; haikukuchukua hata dakika tano kwa Sweden kusawazisha.

ndani ya muda mfupi, Spain wameongza bao jingine la kuongoza. Sasa hivi tuko kwenye dakika za mejeruhi. Mpira umependeza sana dakika hizi za mwishoni. Mpaka sasa Spain inaongoza 2-1.

Katika dakika hizi za mejuri, husu Spain ikiongoza, imeamua kuimarisha sana ulinzi langoni mwake. Sweden watapata muda mgumu sana kupenya na zimebaki kama dakika nne tu.

Spain imeshinda; dakika hizi za mwisho mpira ulisismua sana kwani wanwake wa pande zote mbili walianza kushambuliana kwa nguvu sana. Hata hivyo Sweden ambayo nayo ilikuwa mojawapo mwa vigo wa mashindano haya ameatolewa. Sasa hivi amebaki kigogo mmoja tu-England. Wengine wote ni underdogs : Spain, Australia, na kigogo England


View: https://www.youtube.com/watch?v=h7Mlf7chPJs
 
Mchezo wa pili wa nusu fainali ni kesho saa 7 mchana za Tanzania kati ya Australia na England. Nitaleta bia na nyma za kuchoma ili tushirikiane.
 
Timu zote zimeshaingia uwanjani, kupena bendera na kusalimiana. Sasa wameanza kujipanga kwenye nafasi zao. Muda wowote kuanzia sasa mchezo unaanza.

Mpira umeshaanza

Uingereza imeaza kwa kumiliki mpira sana, lakini timu zote hazijaanza kushambuliana.

Uingereza imeanza masmabulizi sasa; imeshipiga hodi kwenye lango la Australia wakati Australia haijafika kwenye lango la Uingereza
 
Uingereza imepata nao la kwanza. Australia inafanya kosa la kurudisha mipira langoni kwao sana

Baada ya nao la kwanza mchezo imeanza kuwaka

Mpira unakuwa kwenye upande wa Australia sana kwa vile wanamrudishia golikipa wao mno

Halftime sasa

Kipindi cha pili kumeshaanza

Australia wanajaribu kushambulia lakini wanapoteza sana pasi

Kosa kosa bao la pili kwa Uingereza inakuwa kona

Kuna winga wa kushoto wa Australia anatomy krosi nzuri sana lakini langoni hakuna mfungaji

Australia amepata bao la kusawazisha kwa shuti la mbali

Baada ya kusawazisha Australia wameongeza sana kasi ya mashambulizi

Pande zote zimeongeza kasi sasa; mpira unakwenda haraka haraka na Uingereza inapata bao la pili. Hadi sasa Uingereza inaongoza 2-1

Australia imekosa ambao mawili ya waziwazi

Australia ina kosa bao jingine la wazi
 
Uingereza imepata bao la tatu na kuwakatisha Matildas tamaa kabisa. Timu ya Australia inajulikana kama Matildas
 
Back
Top Bottom