Samahani kidogo nilijasahau kuwa mimi ni modereta wa thread hii nikaishia kwenye nyama za kuchoma, bia na TV tu. Sasa nimerudi kwenye meza yangu
Mpaka kipindi hiki cha pili, mceazo kati ya Spain na Uhloanzi bao wako suluhu ya 0-0. Hata hivyo Spain imekuwa ineaielemea sana Uhloanzi kwa mashambuliz mengi na makali sana. Uholazi inabebewa vizuri sana na defence line yao ikiongoza na golikipa wao.
Kuna wakati Spain walifunga bao lakini likakataliwa
Kuanzia sasa nitakuwa kwenye keyboard hii kuleta updates kadri ninavyozipata.
Mshambuliaji wa Uholanzi amefanyiwa faulo kwenye box, kwa hiyo wanaelekea kupata penalty. Hapana, penalty hiyo imekataliwa baada ya kupitia VAR.
Mchezo ni mgumu sana ila Spain wamewalemea sana uholanzi kwa msambuliz. Goli la Uholanzi halina amani hata kidogo.
Spain wamepata penalty na kujipatia goli la kuongoza. hadi sasa matokea ni kuwa Spain ineongoza kwa 1-0 na zimebakti kama dakika nane tu pamoja na zile za majeruhi ili mchezo uishe. Mashinadno haya yana maajabu sana kuwa timu zilizotegemea sana ndizo zimeondolewa au kupata wakati mgumu sana. Inaelekea Uholanzi sasa hivi ni kwishney.
Zimebaki kama dakaika tatu na nawaona Uholazi wameshakata tamaa wala hawajishughulishi kufanya mashambuliz yoyote. Katika mcehzo wote Uholazi walikuwa wanauzia tu, hawakuwa washambuliaji kabisa, jambo lililonishangaza sana kulingana na kuwa walikuwa wanapewa uwezeiakno mkuba. Labda wamekula hela za makampuni ya kamari.
Mchezo uko kwenye dakika za mejeruhi sasa, na Spain wameimarisha ulizi wao sana ukizingatia kuwa hata fowardline ya Uholanzi ni dhaifu sana.
Astaghfirullah! Uholanzi wamesawazisha ndani ya dakika za majeruhi; sikuamini hivyo. Sasa ngoje nilete bia zaidi kujiandaa na dakika nyingine 30 za burudani ingawa Uholanzi hawachezi vizuri.
Haya sasa; dakia 90 official pamoja na zile za majeruihi ndiyo zimekwisha, na msimamo bado ni 1-1 ingawa marefa waliweka dakika nyingi sana za mejeruhi (zaidi ya robo saa) nadhani wakitegemea timu moja itaibuka kidedea lakini wapi. Ngoja sasa tusibiri muda wa nyongeza.
Wachezaji wamepewa muda kidogo wa mapumziko na kusikiliza mafundisho ya mbinu kutoka kwa waalimu wao kabla ya kuanza ngwe ya inayofuata.
Haya jamani; ngwe ya lala salama imeanza. Timu zote mbili zina tension kubwa sana ila naona Spain wameanza kwa kuwaheshimu Uholazi. Ile spidi waliyokuwa nayo kipindi cha kwanza imepungua sana, au labda wameishiwa petroli. Ila mashindano ya mwaka huu hayatabiliki hadi kipenga cha mwisho.
SPain imeanza tena kukiwasha lakini siyo kwa spidi ile ya kipindi cha kwanza.
Time zote zimefanya subs. Nilisoma kuwa Uholanzi ilimwondoa Damari na kuwemka Katarina kwenye safu ya Ulinzi. Spain nayo walimwondoa Eva na kuweka Esta kwenye safu ya ushambuliaji; Spain pia imefanya mabadiliko mengine ambayo majina ya wahusika ni ya kizungu sikuweza kuyakumbuka.
Sasa hivi dakika 15 za kwanza kwenye kipindi cha nyongeza zimekwisha; wachezaji wote wanapumzika dakika tano. Bado matokeo ni 1-1.
Kipindi cha pili cha dakika za nyongeza kimeanza; uholanzi ilfanya subsa za watu wenye majina ya kizungu tu. kwa hiyo timu zote mbile zimefanya subs mbili mbili.
Spain wanapata goli la pili kutokea kwa Salma aliyeingia kama sub kwenye kipindi cha pili. Mpaka sasa Spain inaongoza 2-1
Zimbeaki dakika tatu official pamoja na zile za mejeruhi.
Tuko kwenye dakika za majeruhi na matokeo hayajabadilika.
Mchezo umekiwasha Spain kaibuka kidedea kwa 2-1. Fox wakishaleta video nitazishare hapa. Mchezo ulikuwa mzuri sana kwangu hasa kwa vile nilikuwa sishabikii timu yoyote niliufurahia sana.