FIFA Women's World Cup 2023 | Kombe la Dunia kwa Wanawake

FIFA Women's World Cup 2023 | Kombe la Dunia kwa Wanawake

Mchezo unaofuata ni kati ya Japan na Sweden ambao utaaza saa 4:30 asubuhi za Tanzania. Nikifanikiwa, nitaleta updates minute by minute kwani ninaupenda sana na ninaishabikia Japan.
 
Kipindi cha kwanza kati ya Sweden na Japan

Mpaka sasa bado Sweden na Japan wanacheza kwa kuogopana ingawa Sweden inaonekana kumiliki mpira kwa wingi, lakini mchezo wote uko katikati ya uwanja, hawashambuliani sana.

Sweden walipata nafasi ya kupiga kick na hiyo ikageuka kuwa bao lao la kwanza; hivyo katika dakika hii ya 33, Sweden wanaongoza 1-0.

Baada ya kufunga bao la kwanza sasa Sweden wamekuwa na confidence sana na wameanza kulishambulia lango la Japan kwa kasi sana; Japana hawajasmabulia goli la Sweden kias cha kuridhisha.

Mpaka sasa hivi Sweden imetawala mchezo huo kwa kiasi kikubwa sana. Sijaona jaribio lolote la japan kuingia golini mwa Sweden.

Tunakwenda halftime sasa na hadi wakati huu Japan haijfanya jaribio lolote kwenye lango la Sweden huku Sweden ikiwa imeshashambuli mara nyingi sana.

Kipindi cha pili kinaendelea hapo chini kwa vile kuna post zilifanyka hapa katikati kabla ya mchezo kuisha na hivyo kuvuruga mtililiko.
 
Mpira wa wanawake unavutia sana kuliko mpira wa wanaume. Kwanza wana spidi sana na wanatumia ufundi mwingi mno; hawatumia maguvu kama wanaume. Kama unapenda burudani ya mpira, basi lazima vigezo vyako viwe spidi na mbinu. Ndiyo maana huwa nayafuatilia mashindano haya kwa uzito sawa na yale ya wanaume. Hata mwaka 2019 nilijaribu kuyafuatlia kwa karibu na kuweka record zake hapa 2019 FIFA Women's World Cup
Ha ha ha ha Acha maskhara Mkuu.
Mpira wa wanawake unafurahisha kutokana na makosa wanayofanya na kusababisha magoli. Mfano game ya juzi ya 16 bora beki alivyomrudishia kipa mpira ukaingia moja kwa moja nyavuni halafu kwenye mashindano makubwa kama haya.

Mimi sana sana mle naangalia watoto wazuri tu.

Japo kuna vidada vinakimbiza kabumbu sio Poa.
 
Ha ha ha ha Acha maskhara Mkuu.
Mpira wa wanawake unafurahisha kutokana na makosa wanayofanya na kusababisha magoli. Mfano game ya juzi ya 16 bora beki alivyomrudishia kipa mpira ukaingia moja kwa moja nyavuni halafu kwenye mashindano makubwa kama haya.

Mimi sana sana mle naangalia watoto wazuri tu.

Japo kuna vidada vinakimbiza kabumbu sio Poa.
Kujifunga wenyewe kumetokea mara mbili tu tangu mashindano haya yaanze. na huwa inatokea pia kwa wanaume. Kama unakumbuka kwenye fainali kati ya France na Croatia kule Urusi mwaka 2018, Croatia walijifunga bao la kwa kwanza halafu France nao wakajifunga bao la pili, tena hiyo ilikuwa ni fainali.
 
Kipindi cha pili cha mcehzo kati ya Japan na Sweden kimeanza.

Sweden imanza kwa kasi na nguvu sana. Sidhani kama Japan watapona hapa; bado dakika 41, ngoja tusubiri.

Sweden wamepata bao la pili kwa njia ya penalty na kuzima kabisa ndoto za Japan; Sweden inaongoza 2-0. Japan hawashambulii kabisa goli la Sweden. Golikipa wa Sweden yuko vacation Sheraton.

Japan wana wakati mgumu sana kwani tangu mpira uanaze hawajashambulia goli la Sweden hata kwa kupiga nje tu.

Mpira umekosa msisimko ingawa Japan imeanza kushambulia kidogo kidogo lakini mchezo wote umepooza sana.

Tuko kwenya dakika za 80 na matokeo bado hayajabadilika. Japan ilifanya majaribio kadhaa langoni mwa Sweden lakini yalikuwa majaribio hafifu sana; karibu yote yalikwenda nje na yaliyolenga golini yalikuwa mepesi tu ambayo golikipa angeweza hata kuyapuliza tu yakarudi yanakotoka.

Japan imekosa penalty

Dakika za mwisho wa kipindi cha pili Japan wanapata goli la kwanza, sasa matokeo ni 2-1 kwa upande wa Sweden.

Tumeanza dakika za majeruhi ya kipindi cha pili sasa. Mpira utakwisha wakati wowote kuanzia sasa. Yaania mwishoni mwa mchezo ndipo japa ilipoamka na kuanza mashambuliz sana. Nadhani itakuwa ni too late kwao.

Mchezo umekwisha. Sweden anasonga mbele kwa ushindi wa 2-1.Japan wameniudhio sana kukosa penalty ile. Nimesikita sana kuwa kila timu niliyokuwa nashabikia imekuwa inatolewa kwa makosa ya kujitakia. Sasa hivi imebaki Australia tu.

Nitaleta video FOX wakishaipandisha

 
Mchezo unaofuata ni kati ya Uingereza na Colombia ukaochezwa kesho saa 7.30 mchana saa za Tanzania. Sina utabiri hapo kwani ingawa najua Uingereza ni timu yenye uzoefu na wachezaji wenye majina yao, Colombia imekuwa inazifedhesha timu zenye majina sana kwenye mashindano haya na kutokana na kutokutabilika kwa matokeo haya, ninasubiri mwisho wa dakika tisini tu.
 
Mpira wa Australia na France nimechelewa sehemu kubwa ya kipindi cha kwanza nitaiangalia baadaye kwa vile ilirekodiwa. Mpaka sasa wako half time na bado hawajafungana. Mtangazaji anasema wamepambana nguvu sawa pande zote mbili.

Kipindi cha pili kimeshaanza.

Bado mpira unachezewa katikati tu kama nilivyoukuta kipindi cha kwanza; hashambuliani sana. Nafikiri wanategeana.

Australia imeanza kuwaelemea wafaransa kidogo lakini bado kama 50-50 tu.

Mpira unaelekea kuwa mgumu kwa upande wa Ufaransa sasa. Naona Ufaransa wameanza kuelemewa; ila mchezo huu huwa hautabiriki; meza zinaweza kugeuzwa wakati wowote.

Wanawake hawa wamekabana makoo kweli kweli. Tumebakiza kama dakika nane tu kumaliza zile 90 na sioni wakishambuliana sana; bado mpira unachezewa katika kati ingawa kuna wakati Australiwa walikuwa wakishambulia lakini naona mwamerudishwa tena katikati.

Tuko kwenye dakika za majeruhi; bado dimba ni 0-0.

Official time imekwisha, sasa wanapewa mapumziko kidogo ili waongezewa dakika nyingine 30. Mbape wa kike wa Ufaransa leo alidhibitiwa sana na hao wanawake wa "Austwalia"

1691830606386.png



Kipindi cha kwanza cha dakika za ziada kimeanza. Naona mchezaji mmoja wa Australia kapewa yellow card.

Naona ufaransa walianza kwa kasi kidogo lakini gesi imeanza kupungua tena

Mpira huu ni mzuri sana kwa wanaoutazama na neutral eye. Ila mimi kapuku ninayetaka Australia ishinde ndiye ninapata pressure ya bure sana. Kwa juma timu zote ni ngomu na wanawake wote wanacheza kwa ufundi sana.

Tumeingia kwenye dakika za majeruhi ya kipindi cha kwanza cha nyongeza.

Kipindi cha kwanza kimekwisha

Kipindi cha pili cha dakika za nyongeza kimeanza; hakuna mabadiliko makubwa kwa timu zote mbili.

Ufaransa ilifanya shambulio kali sana golini mwa Australia lakini halikuwa na madhara.

Ufaransa imeoangeza sana mashambulizi upande wa Australia.

Naona mcehazo huu pia utaamuliwa kwa matuta. Mpaka sasa tuko kwenye dakika za majeruhi ya kipindi cha pili cha ziada, na mpira utakiwasha wakati wowote. Kipindi hiki France ilijitahidi kufanya masmabulizi sana lakini yote hayakuwa na madhara yoyote.

Muda official umekwisha sasa ni penalty kicks. Bado wanafanya modalities za nani atapiga penalty kwa pande zote husika. Imeamriwa kuwa Ufaransa ndiyo itakayokuwa ya kwanza kupiga penalty.

Ufaransa imekosa penalty yao ya kwanza.

Asutralia wanapata penalty yao ya kwanza.

Zamu ya Ufaransa sasa: Ufaransa wamepata penalty yao ya pili (Diani)

Zamu ya Australia: Australia wamekosa penalty yao ya pili

Zamu ya Ufaransa: Ufaransa wamepat penaly yao ya tatu (Wendy)

Zamu ya Australia: Australia nao wamepata penaly yao ya tatu

Zamu ya Ufaransa: Ufaransa wamepata penalty yao ya nne (Eugenie)

Zamu ya Australia: Australia pia wamepata penalty uyao ya nne

Zamu ya Ufaransa: Ufaransa wanakosa penalty yao ya tano

Zamu ya Australia: Australia nao wanakosa penalty yao ya tano.

Kipindi cha penalty tano official kimekwisha na timu bado zimelingana kwa 3-3. Sasa tunaingia kipindi cha the first lead.

Grace anaifungia Ufaransa bao la kuongoza

Katarina anaifungia Australia bao la kusawazisha

Sakina anaifungia ufaransa bao la kuongoza

Tameika anaifungia Australia bao la kusawazisha

Mayelle anaifungia Ufaransa bao la kuongoza

Elia anaifungia Australia bao la kusawazisha

Hapo hajapatikana mshindi.

Kenza wa Ufaransa anapoteza penalty

Australia wanasita katika kumchagua mtu wa kupiga penalty inayofuata

Clara wa Australia naye anakosa penalty yake

Inaelekea timu zote zimeanza kukosa wapigaji wa penalty. Wanajishauri sana nani akapige.

Vicki wa Ufaransa amekosa penalty

Cortney wa Australia amepata penalty yake na mchezo umekwisha kwa ushindi wa Australia dhidi ya Ufaransa 0-0(7-6)

Hongera zenu rafiki zangu wa Australia.

Ngoja tuwasubiri FOX watuletee video. Mchezo ulikuwa na msisimkuoa sana na pressure kubwa sana kwa wapenzi kama mimi. Kinachoonekana hapa ni kuwa timu vigogo wamwkuwa wang'olewa mmoja mmoja: Canada, USA, China, Japan, Netherlands na leo France. Sasa ngoja tusubiri England ambaye pamoja na sweden tu ndio vigogo waliobaki.





 
Mchezo unafuata ndani ya robo saa ijayo ni kati ya Colombia na England. Kama huna bia niambie nikulee hapo ulipo, kwani mashindano baina ya vigogo na undergos yamekuwa yanavutia sana. England ni kigogo, lakini Colombia nao ni no pusher underdogs kwa hiyo tunategema burudani safi sana. Kuna wacheazji kadhaa wazuri wa Uingereza hawamo kwenye timu kutokana ama na majeraha au kuwa na kadi za njano na nyekundu
 
Mchezo baina ya England na Colombia uneanza. Kaa mkao wa kula, nitakupakulia minyama yote.

Colombia wameanza kwa nguvu sana.

England imeanza kugeuza meza
 
Mcheazo unafuata ndani ya robo saa ijayo ni kati hya Colombia na England. Kama huna bia niambie nikulee hapo ulipo, kwani mashindano baina ya vigo na undergos yamekuwa yanavutia sana. England ni kigogo, lakini Colombian nao ni no pusher underdogs kwa hiyo tunategema burudani safi sana. Kuna wacheazji kadhaa wazuri wa Uingereza hamao kwenye timu kutokana ama na majeraha au kuwa na kadi za njano na nyekundu
Mkuu mbona umenitamanisha sn,ningepata ofa yako ya kili kubwa 4 tu hii game ningeipata kwa uzuuuri
 
Mchezo huu (England Vs Colombia) hauna kasi ila umejaa mbinu sana kwa pande zote mbili ingawa uingereza inaonyesha ukomavu sana.

Mpaka sasa mchezo uko katikati tu hawashambuliani sana,. Ni kama wanategeana lakini pia timu zote zinaonyesha kuwa na ulinzi mzuri.

Colombia wameshawararua vigogo England bao moja.

Bila subira England nao wamesawazisha. Sasa sehemu ya mchezo uliobaki utakuwa wa nguvu sana. Tunaingia kipindi cha mapumziko sema nikuletee bia kabla kipindi cha pili hakijaanza. Order baada ya mchezo kuanza haikubaliki.
 
Back
Top Bottom