Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
FIFA huwa hawaweki chochote mpaka baada ya mwezi mzima tangu mashindano yaiseh wakati mwingine inawachukua hata miezi miwili. Jaribu kugoogle "Bein TV" ndiyo mimi hutumia kuangalia mashindano ya CAF na ya UEFA bure. Link yake kutokea huku imeziba michezo inayopendwa na watu wa huku ikiwamo hiyo World CUP.
Ripoti ya leo ni nzuri sana... Masikitiko ni kwa Banyana Banyana.Mchezo baina ya Uholanzi na South Afrika umeshaanza ingawa hadi nakuja kwenye compyuta Uholanzi ilikuwa inaongoza kwa bao 1-0 lililofungwa dakika ya tisa tu. Hata hivyo ndiyo mchezo umeanza ngoja tuone utakwishaje. Katika dakika hizi za kwanza Uholanzi wamekuwa kwa spidi kubwa na wamemiliki mpira sana. Hatujui kama hiyo itakuwa ni nguivu ya soda tu kabla dada zetu Banyana Banyana hawakunjua makucha yao.
Banyana Banyana wameanza kukiwasha sasa. Naona wamanza kuwa masimba jike wenye njaa. wameanza kuwakamia Uholanzi kama nini ingawa bado uholanzi wanatawala mcheazo lakini wameanza kupoteza petroli.
Naona Uholanzi wameaza tena kuchoma mafuta tena na kuongeza mashambulizi kwenye lango la Banyana Banyana lakini bila madhara yoyote.
Hawa wasichana wa banyana Banyana kweli wanalijua boli. Pamoja na kufungwa wana-control mpira vizuri sana. Mambo yanaweza kugeukia upande wao wakati wowote ingawa Uholanzi imeweka ulinzi mkubwa sana langoni mwao baada ya kupata bao mapema.
Mpaka Half-time mabao bado ni 1-0 huku Uholanzi ikiongoza. Hata Hivyo dakika za mwisho Banyana Banyana walilishambulia sana lango la Uholanzi na walimiliki mpit=ra kwa kiwangu kikubwa sana kiasi kuwa kipindi cha pili kinaweza kuwa chao.
Nimeshaona wasichana hawa wa uholanzi wakimwomba refa amalize mpira mara moja. Inaonyesha kuwa kipindi cha pili Uholanzi watakuwa defensive sana, wanaelekea kucheza na walinzi wengi sana kulinda goli lao moja.
Kipindi cha lala salama kimeshaanza. Tuwaombee sana dada zetu wa Banyana Banyana; wameanza kwa masmabuliz makali sana dhidi ya Uholanzi.
Uholanzi wamepata goli la pili mwanzoni tu mwa kipindi cha pili. Matumaini ya Banyana Banyana yanaanza kupungua japo wameonyesha mchezo mzuri sana. Good news! Bao hilo limekataliwa
Banyana Banyana haonyeshi kukata tamaa na wameanza tena kwa nguvu ile ile.
Uholanzi imetoesha kidonda kwa kuongeza bao la pili. Sasa kazi itakuwa ngumu sana kwa Banyana Banyana.
Baada ya kupata goli la pili, wanawake wa uholanzi walikaza misuli sana kulilinda. Banyana Banyana wanapata wakati mgumu sana kupenyeza.
Tuko kwenye dakika za mejruhi na tayari Banyana banyana wameshaka tamaa. Ninachoogopa ni kwamba wasijekuruhusu goli la tatu kutokana na kukata tamaa. Ilivyofika dakaia ya tisini nilikaribia kupata heart attack kwa masikitiko ila nikavuta bia moja baridi nikapona.
Haya jamani, mpira umekwisha na Uholanzi wameibuka kidedea kama ambavyo wale akina Sheikh Yahya wa mchongo niliopost hapo juu walivotabiri. Nasubiri FOX wapandishe video za highlights niziweke hapa. Mchezo unaofuata ni baina ya Marekani na Sweden ambao utachezwa saa 6 mchana saa za Tanzania.
Siku njema!
Banyana Banyana wamecheza mchezo mzuri sana; muda wote kocha wa Netherlands alikuwa anasumbuliwa na presha kupanda na kushuka. Amemeza vidonge vingi sana kuponya maisha yake; ukimwambia mchezo urudiwe hatakubali kabisa.Ripoti ya leo ni nzuri sana... Masikitiko ni kwa Banyana Banyana.
Hapana shaka watakuwa wamepata uzoefu fulani kwa fainali hizi...