FIFA Women's World Cup 2023 | Kombe la Dunia kwa Wanawake

FIFA Women's World Cup 2023 | Kombe la Dunia kwa Wanawake

Nimeona Wachina wakichezea kichapo murua kabisa...
Leo wachina wamecheza kichapo cha mbwa koko mabao 6-1 na hivyo kutolewa nje ya mashindano kwa vile kwenye group lao sasa ni England na Denmark ndio wanaosonga mbele kwenye round ya 16. Bao moja walilipata la penalty ambayo ilikuwa ya mauzauza tu. England likuwa inafunga mabao mazuri sana.

 
Marekani imelazimishwa droo ya 0-0 dhidi ya Ureno. Forward line ya Marekani mwaka huu ni dhaifu sana kwa vile ilikuwa inashindwa kumalizia mipira ya wazi kabisa. Nimeshaikatia tamaa kabisa timu ya Marekani mwaka huu ingawa kwenye grupu lake imeshika nafasi ya pili na hivyo itaendelea katika round of 16 pamoja na Uholanzi. Inaonyesha kuwa wakati mwalimu alipokuwa mwanamke (Jill Ellis) timu ilipanda sana, lakini tangu mwalimu awe mwnaume (Vlatko Andonovski) naona timu imerudi nyuma sana; wachezaji wake wengi walipewa Yellow cards ambapo Rose Ravelle kapewa Yellow card ya pili kwa hiyo atakosa mechi ya kwanza kwenye group of 16. Nadhani wanawake wanajua kuongea na kuwafundisha wanawake wenzao vizuri ya wanaume.



Haya sasa wapinga ushoga eleweni kuwa Jill ameoana na mwanamke mwenzake Betsy Stephenson. Kwa nchi za kwetu, uwezo wake wa kufundisha mpira hadi kupata makombe mengio ya world cup ungetepwa jalalani akanyongwa kama sheria ya Uganda invyosema.
1690929562145.png
 
Transgender kibao hapo hamna wanawake ukifuatilia ni midume ime left gr
 
Mcehazo wa Mwisho ulikuwa baina ya Denmark na Haiti. Ilitarajiwa kuwa Haiti itafungwa tu kwani ndiyo timu dhaifu kiwenye grupu lao; hato hivyo waweka mchezo mgumu sana dhid ya Denmark ingawa walitolewa kwa mabao 2-0

 
Timu za kuangaliwa sana mwaka huu ni Sweden, England, France na Netherlands. Canada imeshatolewa nje, na USA haina makali yake yale ya miaka ya nyuma, nadhani USA itaweza kutolewa kwenye group of 16 isipobadili mbinu za mchezo. Kuna wasiwasi isifike hata robo fainali
 
Mcehzo mwingine wa leo ulikuwa baina ya Uholanzi na Vietnam. ambapo Uholanzi ilitoa kipigo cha kufa mtu kwa kuifunga Vietnam 7-0. Netherlands (Uholanzi) itakuwa ni timu ya kuangaliwa sana kwenye mashindano haya. Inaweza kuwa bingwa.

 
Mchezo wa leo baina ya South Africa (Banyana Banyana) na Italy ni wa muhimu sana kuangalia kwani South Afrika ikiifunga Italy bao moja tu, inakuwa aimeifungashia Itally virago vyake na yenyewe kuendelea kwenye round of 16. Kwa mchezo walioonyesha dhidi ya Sweden na Argentina, sina wasiwasi South Afrika wataendele mbele wakikaka buti kidogo.
 
Kwa bahati mbaya Banyana Banyana wameshafungwa 1-0 mpaka dakika hii ya 30 ninapoandika. Sasa watatakiwa waifunge Italy bao mbili; ngonja niendelee kutazama na kuwaombera dada zetu wavuke waingine kwanye round ya 16.

Update: Nimerudi kwenye TV mara baada ya kuandika hapo juu nikakuta Banyana Banyan wameshaswazisha. Sasa ni mbao 1-1.
 
Hatimaye South Africa waingia round ya pili baada ya ushindi wa 3 -2 dhiidi ya Italy
 
Hatimaye South Africa waingia round ya pili baada ya ushindi wa 3 -2 dhiidi ya Italy
Mchezo wa S.Africa ulinifurahisha sana kwani nilipata matokeo niyokuwa napenda. Ingawa Itally nao walicheza vizuri sana, ni wazi kuwa S.Afrika iliwaelemea zaidi. Italy walijifunga bao ambalo liliwaongezea nguvu sana S.Africa.

 
Mchezo wa pili ambkwa leo ambao ulikuwa ni wa kumalizia ratiba tu kwani matokeo yalikuwa hayaathir msimamo wa ligi ni ule baina ya Argentina na Sweden. Ingawa katika kipindi cha kwanza Argentina ilikuwa imeweka ngumu sana, ilipofika round ya pili walilainika na kufungwa mabao 2-0



Sasa Sweden itapambana na Marekani ambapo South Afrika itapambana na Uholanzi.
 
Bingwa, Sweden, US, au Brazil

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Brazil imeshatolewa labda ifanikiwe kupata goli la dakika za mwisho mwishoni. Mpaka sasa wamekaliwa koo na Jamaika bado wako 0-0 na kuifanya Jamaika iwe ya pili kwenye kundi lao. Hadi naandika post hii zimebaki kama dakika 10 tu mpira uishe. Brazili ikipata goli moja basi yenyewe ndiyo itakuwa ya pili ili kuendelea kwenye kundi la 16.

UPDATES: Mpira Umekwisha na Brazil imeshatolewa kwa kutoka suluhu. Nasubiri Video kutoka Fox niiweke



US ya mwaka huu ni goigoi sana kwenye ufungaji; labda wabadilishe mfumo kuanzia sasa. Inawezekana US ikatolewa na Sweden kwenye round of 16
 
Back
Top Bottom