FIFA Women's World Cup 2023 | Kombe la Dunia kwa Wanawake

FIFA Women's World Cup 2023 | Kombe la Dunia kwa Wanawake

Kwa wanaoikumbuka timu ya Jamaica mwaka 2019 ilivyoichakza Australia bila huruma. Kwenye mchezo wao wa kwanza mwaka huu dhidi ya timu mchachari ya Ufaransa ya akina Kadidiatou Diani (Mbape wa Kike), Eugénie Sommer (Mayele wa Kike) na wafaransa wengine machachari wa kike wamebanana na kutoka droo 0-0. Kisiwa cha Jamaika kwenye upande wa michezo kiko vizuri sana; kinalingana ukubwa na mkoa wa Morogoro.



Ufaransa leo hawakuwa na golikpia wao mdaka mishale Sarah Bouhaddi kwa sababu inasemekena alianza maisha ya kulea familia kuanzia mwaka 2020; ametunza maisha ya familia yake binafsi haiandikwi hovyo mitandaoni.
1690146948196.png
 
Haya jamani, dada zetu wa Morocco leo wamechezea kichapo cha mbwa koko. Tatizo kubwa sana la Morocco lilikuwa kwenye ngome ya ulinzi pamoja na golikipa walikuwa wanapwaya sana. Walifanya makosa mengi yaliyoirahisishia Ujerumani kuwafgunga jumla ya mabao 6-0 ambapo magoli mawili walijifunga wenyewe. Mororcco0 ndiyo timu iliyofungwa mabao mengi zaidi katika mchezo mmoja tu ikifuatiwa na Zambia ambayo ilifungwa 5

 
Mchuano kati ya Italy na argentina ulikuwa ni wa vuta nikuvute kweli kweli. Itaslly walikuwa wakilishambulia sana lango la Argentina ingawa mbabo yao mawili yalikataliwa kwa ni ya kuotea, mojapoa halikuwa la kuota baada ya playback ya makini lakini ingawa uamuzi ulikuwa umeshatoka. Dakatika za mwisho mwisho Itally ikapata goli moja na hivyo kumaliza mcehzo kwa ushindi wa 1-0

 
Zaidi ya Morocco, timu nyingine iliyotembezewa kichapo cha mbwa koko na Panama ilipopambana na Brazili. Kwa Ujumla timu ya Brazi iliielemea Panama sana ingawa mashambuliaji maarufu wa Brazil namba kumi ajulikanaye kama Marta kutocheza kipindi choate cha kwanza, bado Brazili iliichapa Panama mabao 4-0. Iwapo Marta angecheza vipindi vyote viwili (ana miaka 39 sasa) inawezekana Panama ingefungwa zaidi ya hayo mabao manne.

 
Mchezo baina ya Colombia na South Korea ulikuwa wa kasi sana na wachgeazji wengi walikuwa watoto wadogo kwa pande zote mbili. Colombia walikuwa wanalishambulia lango la Korea kwa kasi isiyokuwa na kipimo ingawa Korea nao walikuwa wanashambulia lango la Colombia vivyo hivyo. Golikipa wa Colombia alikuwa ukuta kweli kweli na kusababisha Korea isifunge bao hata moja. Matokeo ya Mwisho Colombia ilishinda bao 2-0

 
Kama mnakumbuka kwenye round ya kwanza Philipines ilicheza mchezo mzuri sana dhini ya Switzerlnad lakini bado ikasihia kufungwa. Nadhani kwenye round ya pili kocha wao alijifunza makosa waliyofanya kwenye round ya kwanza na kuyfanyia kazi. Mchezo wa dihdi ya New Zeaknda kwenye round ya pili waliidhihiriosha dunia kuwa Philipnes siyo timu ya kuangaliwa hivi hivi baada ya kwachapa New Zealanda ambao wenyeji wa mashindano hayo kwa bao 1-0

 
Kwa bahati mbaya mchezo baina ya Switzerland na Norway ni kati ya michezo ambayo haikusisimua sana kwenye raundi hii ya pili inayoendelea. Sehemu kubwa ya mpira ulikuwa katikati ya uwanja na mashambulizi langoni yalikuwa machache sana. ambapo washambuiliaji walikuwa ndio wanafanya makosa kushindwa kutumia nafasi hizo Mwisho wote walishia kutoka droo ya 0-0

 
Dada zetu wa Zambia wameendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu baada ya kufungwa mabao 5-0 na wenzao wa Spain. Hii ni baada ya kuwa wamefundwa 5-0 na japan wakati michezo ya round ya kwanza.Kwa mwendelezo huu, nawashauri watafute sababu yoyote ya kujitoa kwenye mshindano hayo kuliko kuendelea kubebeshwa mbao matano matano.

 
Japan wameendeleza ubabe wao kwa kuwafunga Costa Rica bao 2-0. Kwa sasa hivi naona Costa Rica na Zambia wanaaza kusogelea mlango wa kutoka kwenye mashindano haya wakiwaachia Spain na Japan waendeleze kundi lao.

Ikumbukwe pia kuwa kwenye mashindano kama haya kwa wanaume huko Qatar, Costa Rica ndio walioifunga Japan 1-0

 
Mchezo bain ya Canada na Ireland ulikuwa mgumu kwa pande zote mbili ila Canada walitumia sana uzoiefu wao katika mashindano haya na kuwabonyeza Ireland mabao 2-1. Kwa ujumla mchezo ulikuwa mzuri sana.
 
Kwa mnaokumbuka mwaka 2019, fainali ya kombe hili iliwakutanisha USA na Uholanzi. Sasa leo hao miamba hawa walikuwa wanakutana klwenye makundi roundi ya pili na hadi ninaaza kuandika post hii bado wanamenyana ila zimebaki kama dakika tisa tu ( + dakika za majeruhi) mchezo kuisha. Mchezo huu ulikuwa mgumu sana kwa Marekani kwani Uholanzi walipopata goli la mapema sana walicheza mchezo wa kulilinda goli lile kwa nguvu sana kiasi kuwa japokuwa Marekani walitawala mchezo na walishambulia sana goli la Uholanzi, ngome ya Uholanzi ilikuwa imara sana jambo lililowakatisha sana tamaa wachezaji wa Marekani hadi pale mfungaji bora wa marekani mwaka huu Lindsey Horan alipopata bao la kusawazisha kwenye dakika ya 62 kutokana na pasi ya mpiga chenga matata Rose Ravelle (aliyefunga bao la kusiliba ushindi mwaka 2019). Hata hivyo muda mfupi baadaye Rose Ravelle alipewa yellow card. Hadi wakati huu kwenye dakika za majeruhi, presha bado inapanda na kushuka kwa pande zote mbili na haijulikani nani ataibuka na ushindi, ngoja nisubiri kipenga cha mwisho ndipo nipinge kongole la Post Reply.

Basi kipenga kimepulizwa na imeishia kuwa droo ya 1-1. Nitaleta video baada ya Fox kuipandisha. Mchezo huu ulikuwa ni kama mchezo wa fainali kwa vile ulijaa mbinu za kiufundi sana na mitego mingi ya kila aina.


 
Hii michuano mwaka huu imekosa mvuto hasa kwa afica kitokana na muda zinachezwa mechi, mechi zinachezwa alfajiri mara asbhi.
 
Mchezo wa leo baina ya Nigeria na Australia nadhani ni kati ya michezo iliyonisisimua sana. Ingawa kipindi cha kwanza kilikuwa na sintofahamu nyingi na Australia wakafanikiwa kupata goli la kwanza katika kipindi cha dakika za majeruhi ya kipindi hicho, mambo yalibadilika sana kipindi cha pili. Dada zetu wa Nigeria walitawala sana mchezo ule katika kipindi cha pili hadi kufikia dakika ya 90 Nigeria ilikuwa inaongoza kwa mabao 3-1; hata hivyo kunako dakika ya 99 ndani ya muda wa majeruhi ndipo Australia wakapata goli la pili na hadi kipenga cha Miwsho Nigeria iliongoza mashindano yake kwa mabao 3-2.

Golikipa wa Nigeria apewe maua yake kwani aliokoa mashambulizi mengi sana.

 
Mchezo baina ya Argentina na South Africa ulikuwa mgumu sana kwa upande wa Argentina, ingawa pia walitumia offside tricks mara kadhaa kuzuia South Africa isifunge magoli. Hadi dakika ya 70 south Africa ilikuwa inaongoza kwa mabo 2-0; hata hivyo baada ya dakika ya 74 Argentina iliweza kuyarudisha magoli yote mawili ndani ya dakika tano tu na mwisho mchezo ukaishia droo ya 2-2

 
Mchezo baina ya Ureno na Vietnam haukuwa na mashamsham sana. Nilisahahu kuleta link yake kwa sababu hiyo ila Ureno ilishanda kwa mabao 2-0

 
Mechi iliyowakutanisha China na Hait ilikuwa mbaya sana kwani China walikuwa wanacheza rafu sana hadi mcheazaii wao mmoja akatolewa kwa kadi nyekundu. Hata hivyo China walipata penalty iliyowapatia ushindi wa 1-0. China walihitaji sana uchindi huo ili wasitolewa kwenye kundi baada ya kuwa wameashafungwa mchezo wa kwanza. Bahati haikuwa upande wa haiti ingawa walichezao mcehzo mzuri sana.

 
Mchezo baina ya uingereza (England) na Denmark ulikuwa na mbwembwe sana na timu zote zilionyeshana umahiri. Hata hivyo goli la mapema lilifungwa na Lauren James dakika ya sita kipindi cha kwanza liliwahahakishia Uingereza ushindi.

 
Matokeo yaliyoshangaza wengi ni kwenye mchezo baina ya Sweden na Italy. Ilitegemewa kuwa mchezo utakuwa mgumu kwa pande zote lakini jambo la kushangaza Italy iligeuka kichwa cha mwendawazimu kwa kufungwa mbao 5-0

 
Mchezo uliokuwa unasubiriwa kwa hamu na watazamaji wengi ni kati ya France na Brazil. Kweli mchezo huu ulikuwa mzuri sana kwani ulijaa ufundi na mbinu za hali ya juu sana. Ufaransa ilipata bao la kwanza mapema sana kunako dakika ya 17 kupitia mshambuliaje wake Eugenie. Hata hivyo mwanzoni mwa kipindi cha pili Deborah akaipatia timu yake ya Brazil bao la kusawazisha hali iliyofanya mchezo uwe tense sana kwa pande zote mbili. Kunako dakika ya 80, Wendie ambaye ni mchezaji mrefu sana kuliko nadhani wachezajei wote kwenye mashindao hayo, aliipatia Ufaransa goli la kichwa kutokana na mpira wa kona na kusababisha mchezo kuisha kwa Ufaransa kushinda 2-1

 
Back
Top Bottom