FIFA Women's World Cup 2023 | Kombe la Dunia kwa Wanawake

FIFA Women's World Cup 2023 | Kombe la Dunia kwa Wanawake

Mchezo wa mwisho kwa leo ulikuwa baina ya Jamaica na Panama. Kitu cha kushangaza, mchezo huu ulikuwa na mvuto wa hali ya juu kuliko ilivyotegemewa na wafuatiliaji wa michezo hii. Mshambuliaji Allyson Swaby wa Jamaica aliipatia timu yake goli la pekee na la ushindi kunako dakika ya 56 baada ya kosa kosa nyingi sana kwa pande zote mbili.



Naona nikumbushe watu hapa kuwa huyu Allyson Swaby aliyeifungia Jamaica ni mmarekani aliyezaliwa Connecticut. Timu ya Jamaica ina wamerakani wasiopungua wanne, wakati timu ya Panama nayo ilikuwa na wamerakani wasiopungua wanne pia. Timu ambayo ina wamarekani wengi sana nje ya Marekani yenyewe ni ile ya Phillipines kwani ina wamerakani 16
 
Mchezo kati ya South Korea na Morocco ndipo umeanza dakika hii. Kwa walio macho nitawajaulilsha maendeleo yake pole pole; ninaishabikia Morocco kwa vile ni waafrika wenzagu japo wa kiarabu.

Dakika ya sita Morocco ilipata goli la kwanza kwa kichwa cha Ibtissam, hivyo hadi muda huu Morcoco ndiyo inayoongoza kwenye mtanange huu. Bado kuna dakika zaidi ya themanini; tuendelee kusubiri.

Hadi dakika ya Mwisho matokeo hayakubadilika. Morocco illibuka kidedea kwa 1-0 baada ya kuwa imefungwa mabao mengi sana na Ujerumani. Kwa jumla Morocco leo ilicheza vizuri sana kuliko ilivyocheza dhidi ya Ujerumani

 
Nadhani mchezo ulionishtua sana ni huu baina ya Colombia na Ujerumani. Nilifungua TV nikiamini kuwa Colombia ni kichwa cha mwendawazimu mbele ya Ujerumani. Ila Colombia ilinishangaza ilivyocheza kwa ufundi wa hali ya juu na kutawala mchezo wote kiasi kuwa Ujerumani ilikuwa inaomba mchezo uishe haraka sana. Hadi dakika ya mwisho Colombia ilishinda kwa 2-1. Highlights za mchezo ni hizi hapa chini

 
Niwe mkweli nilisikitishwa sana mechi baina ya Norway na Phillipines kwenye Group A. Sitaongea lolote kwa nini nimesikitishwa na matokeo hayo ila jionee mwenyewe. Wachezaji 16 wa Phillipines akiwemo yule aliyepewa red card ni Wamerakani

 
New Zealand na Switzerland walimaliza mchezo wao bila kufungana. Ninawapa sifa zaidi magolikipa wa timu zote mbili waliokoa mashambulizi mengi japo hatakuwa makali sana.

 
Germany
emoji91.png
emoji91.png
emoji91.png
emoji91.png
BINGWA
Leo wamechezea za uso, na pengine watakosa kuingia 16 bora...
 
Dada zetu wa Zambia kama wenzao wa Morocco na wamechoka kuwa kichwa cha mwendawazimu baada ya kufungwa michezo miwili ya kwanza mabao mengi leo wamamua kuwasulubu wenzao wa Costa Rica jumla ya mabao 3-1.

 
Kati ya michezo iliyonifurahisa sana ni ule wa Japan na Spain leo. Kwenye timu ya Japan kuna mchezaji anaitwa hasegawa, jina la aliyekuwa mpenzi wangu ningali kijana, kwa hiyo nilikuwa naishabikia Japan kwa sababu ya Hasegawa, na kweli hawakuniangusha. Wameibamiza spain mabao 4-0. Mshambulaiji mmoja wa Japan anyeitwa Miyazawa anacheza kama Mayelle kabisa.

 
Kuna michezo miwili inayoendelea kwa pamoja wakati huu. Nadhani FIFA wamefanya makosa kuchezeasha micehzo miwili katika muda mmoja kwani imenilazimu kuhamisha TV nyingine kutoka ukumbi wa chini kuileta ukumbi wa juu kusudi nie na TV mbili kuweza kuangalia michezo yote. Ninaangalia Nigeria Vs. Ireland, na Canada Vs Australia. Nitaleta updates michezo hiyo ikiisha; ila hadi sasa Nigeria Vs Ireland bado wako suluhu 0-0 wakati Australia inaingoza Canada 2-0. Ni jambo la ajabu sana kwa Canada kwani nadhani ndiyo bingwa wa Olympic hadi wakati huu.
 
Mpaka sasa wachezaji wenye talents zilizonivutia:

Linda Caicedo 🇨🇴
Eugénie Le Sommer 🇫🇷
Sakina Karchaoui 🇫🇷
Kerly Théus 🇭🇹
Mary Earps 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿
Lauren James 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿
Alessia Russo 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿
Kim Hye-Ri 🇰🇷
Alexandra Popp 🇩🇪
Ramona Bachmann 🇨🇭
 
Mchezo baina ya Nigeria na Ireland umekwisha kwa droo ya 0-0. Nigeria walijitahidi sana lakini bahati haikuwa yao. Nitaleta video baadaye kidogo Fox wakishaipandisha.

Video yenyewe hiyo hapo
 
Mpaka sasa wachezaji wenye talents zilizonivutia:

Linda Caicedo 🇨🇴
Eugénie Le Sommer 🇫🇷
Sakina Karchaoui 🇫🇷
Kerly Théus 🇭🇹
Mary Earps 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿
Lauren James 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿
Alessia Russo 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿
Kim Hye-Ri 🇰🇷
Alexandra Popp 🇩🇪
Ramona Bachmann 🇨🇭
Vipi Miyazawa, Rose Lavelle na Lindsey Horan?
 
Mchezo baina ya Canada na Australia nao umekwisha kwa Australia kuwabamiza Canada mabao 4-0. Leo Canad ilicheza mcvehazo hafifu sana kulinganisha na ilivyocheza wakati wa Olympic kule Tokyo. Nitaleta viodeo baadaye kidogo zikishapatikana hewani.


 
Mpira wa wanawake ni mzuri sana; nawasikitikia ambao hawapati kuangalia mashindano haya kwani yanasisimua sana.
 
Mpira wa wanawake ni mzuri sana; nawasikitikia ambao hawapati kuangalia mashindano haya kwani yanasisimua sana.
Wanawake wanacheza kandanda safi sana. Wapenda football mechi yoyote tunaangalia cha muhimu entertainment na kujifunza mengi zaidi kwenye mchezo huu pendwa.
 
Mpaka sasa wachezaji wenye talents zilizonivutia:

Linda Caicedo 🇨🇴
Eugénie Le Sommer 🇫🇷
Sakina Karchaoui 🇫🇷
Kerly Théus 🇭🇹
Mary Earps 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿
Lauren James 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿
Alessia Russo 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿
Kim Hye-Ri 🇰🇷
Alexandra Popp 🇩🇪
Ramona Bachmann 🇨🇭
Hatimaye Alessia Russo kapata goli lake la kwanza.

Lauren James kambani tena.

Manchester United walifanya makosa makubwa sana kuwaachia hawa wachezaji.
 
Mpira wa wanawake ni mzuri sana; nawasikitikia ambao hawapati kuangalia mashindano haya kwani yanasisimua sana.
Uko sahihi wanacheza kwa utulivu mkubwa na wenye urahisi kwa mtazamaji kufatilia
Binafsi nafatilia hapa Azam Hawa cecafa maana hao world cup hakuna mahali pa kuangalia ila huwa najua ni Raha sana kuungalia
 
Back
Top Bottom