Figisu dhidi ya CHADEMA zashika kasi, RC Mwanza apiga marufuku mikusanyiko

Upeo mdogo wa wateule wa Rais ndipo unapoishia.
 
Kwahiyo mechi ya Yanga vs Simba haitakuwepo?
Hii Nchi Mbona Tunakuwa Kama Si Binadamu wajameni.
WANASIASA nje ya kufanya shughuli za kisiasa mnataka wafanye nini?
Halafu mtasema vyama Ni vya msimu, havina ajenda, huku mnazizima ajenda zao. SAD!
 
Hio Virus havihusikii vinaogopa Simba na Yanga. Huyu RC akili zake hazina akili
Simba na Yanga,ni Kigoma sio Mwanza,alafu kasema Mpaka uombe kibari, hivo mikusanyiko inarusiwa ila mpaka kibari cha mkuu wa mkoa 😁😄😄😃😀
 
Kongamano Kama la chadema ,tumeona kila lilipo fanyika watu wamekua wakichukua hatua ,Sasa ACHA ajichanganye KWA kufuata mkumbo wa kutoa kauli, ipo kesho yake atakua yupo peke yake


Viongozi watambue mda unaenda kasi Sana, na kesho yetu hatujui bila kujali ni kiongonzi au la, nyakati Kama izi viongozi wanatakiwa kuwa makini, bora pale uonapo unacholazimishwa fanya KWA akili yako hakifai , piga chini KAZI, ili ukaishi na amani ya roho
 
Huu ni upuuzi vipi kusanyiko la misiba na ibada huko covid inapaogopa njoo na la maana Mzee vinginevyo hueleweki
 
Safi sana, Mbowe anamdharau mama. Wapelekwe Butimba hao naona hilo gereza hawajawahi kuingia
 
Ujumbe sahihi kabisa huu
 
Kama anafikiri anamsaidia Mama ajue ni kinyume chake. Hizi move za kipumbavu ndiyo zinazidi kuiharibia CCM.
 
Watakao tuingiza kwenye uhasama ni wale wasiofuata sheria.
Wanaishi kwa matamko
 
Mhu!
 
Mikusanyiko ni hatari sana hapo Mwanza sababu ya COVID imeenea sana, ikiwezekana kuwepo na lockdown anagalau ya wiki 1 kuepusha kusambaa kwa COVID.
Mbona mwenge haupigwi malufuku na leo umekesha Igunga?
 
Mbowe kama anataka mikusanyiko aanzie kwao huko Kilimanjaro kwanza,tuone kama atapata watu...

Kuna wimbi la tatu la Covid 19,kaka yake kafarik sasa anataka nani afe Ili azid kuamin kuwa huu ugonjwa haujitaji masihara
 
Najua CHADEMA wana vichwa nguli vya wanasheria, wakiamua wanaweza kuangalia kama Mkuu wa mkoa ana powers za kususpend haki za kikatiba za raia au la.

Pia wanasheria wa CHADEMA wanaweza kuangalia kama sheria inamruhusu mkuu wa mkoa kutangaza dharura za kiafya au hiyo ni kazi ya waziri

Serikali ya CCM wanandhani wana akili nyingi lakini mambo wanayoyafanya yakikutana na vichwa vinavyojua haki zao wanaonekana wamekurupuka!.

Hili agizo la Mkuu wa mkoa wa mwanza ni faida kisiasa kwa CHADEMA kwa sababu kuu mbili.

1. Moja, Watawala wamekosa kuzuia mikutano ya ndani kwa hoja za maagizo kutoka juu,au kukosa kibali, imewabidi sasa watafute excuse nyingine. Hii ni hatua kubwa kwa CHADEMA kwa sababu kama CCM wao watafanya mikutano kipindi hiki cha Korona basi hakuna reason ya kuwazuia CHADEMA

2. Inamuweka Samia kwenye wakati mgumu kwenye ishu ya Korona, maana raia wengi watatafsiri kuwa anatumia kisingizio cha Korona kuzuia mikutano ya CHADEMA tu, Na hapa CHADEMA wanaweza kuiplay hiyo mantra kuwa Samia hayuko serious kwenye vita dhidi ya Korona licha ya kujidai anaizungumzia, hapa itapelea raia wengi wamuone Samia hayuko serious na hivyo kupoteza mtaji wa kisiasa.

Hakuna sababu ya kuizuia CHADEMA kufanya siasa, ni haki yao ya kikatiba
 
Mbowe kama anataka mikusanyiko aanzie kwao huko Kilimanjaro kwanza,tuone kama atapata watu...

Kuna wimbi la tatu la Covid 19,kaka yake kafarik sasa anataka nani afe Ili azid kuamin kuwa huu ugonjwa haujitaji masihara
Mikusanyiko inazuiwa pale CHADEMA wanapotaka kufanya mikutano tu ila ya CCM haina shida?
 
Tunafuata maelekezo ya waatalamu kuzuia korona..ikiwamo kuzuia mikusanyiko isiyo ya lazima..hii kauli mbiu chadema mshaitosa? Si mlikuwaga hadi mnafanya vikao online sasa kwanini kongamano lisifanyike online pia?
 
Huyu mkuu wa Mkoa aliekuja kufungua kongamano la maelfu ya wafuasi wa Mwamposa hapo uwanja wa furahisha au ni mwingine? Kama ni yeye awajibishwe kwa kuweka maisha yetu rehani kwa kuruhusu na kushiriki kongamano la Mwamposa huku akijua Bugando mitungi ya gas haitoshi na Covid 19 bado ni tishio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…