Ni mara chache mimi na wewe tunakubaliana and here is my two cents from the neighbouhood!
Na mimi natoa tahadhari kwa mwenyekiti wa Chadema FAM kwamba wapambe maslahi ni wa kuogopwa kama ukimwi.
Baba wa taifa alitaka kuachia uongozi mapema sana lakini wapambe maslahi hawakuwa tayari, walimlilia wakitaka aendelee kwa kudai hakuwepo mtu wa kuvaa viatu vyake.
Mwaka 1975 wapambe maslahi walimsihi aendelee wakidai haukuwa wakati muafaka wa kuachia madaraka kati kati ya chochoko za Idi Amin Dada wa Uganda zikiwa zimepamba moto.
Mwaka 1980, wapambe hao hao nuksi walimuomba aendelee tena wakidai ndiyo tumetoka vitani (vita vya Kagera) na hivyo uongozi wake bado ulihitajika kuliko wakati wowote ule!
Mwalimu alikubali lakini kwa sharti moja ingekuwa awamu yake ya mwisho na kweli mwaka 1985 aling'atuka baada ya kutembea nchi nzima akimnadi mrithi wake Hasan Mwinyi wa Zanzibar.
Sasa shuhudia lawama alizopewa Mwalimu baada ya kung'atuka madarakani alipopinga Mwinyi huyo huyo kuongezewa miaka mingine mitano baada ya kumaliza muda wake mwaka 1995!
Wapambe maslahi wa Mwinyi walimtaka Mwalimu akae kimya wakidai inakuwaje apinge wakati yeye mwenyewe aling'ang'ania madaraka kwa miaka zaidi ya ishirini bila kumpisha mtu!
Chama kile kile, wapambe wale wale...na sasa tunawashuhudia wapambe wa mwenyekiti wa chama mbadala Chadema wakiwa kazini wakifuata nyayo za wapambe wa CCM, hakuna cha ajabu!
Birds of a feather fly together...ndege wafananao huruka pamoja! Ni Lissu tu ndio mpaka sasa ameaonesha nia na ari ya kulikwamua taifa letu kutoka mikononi mwa walafi, wanafiki na wafuata nyayo!
Mbeba maboksi here I come with my two cents from a distance.
Nianze kwa kuwatakia heri ya Krismasi kwenu waumini wa Kristo.
Kwa wasio waumini, nanyi nawatakieni sikukuu njema na mapumziko mema.
Nimekuwa nikiifuatilia hii mijadala ya uchaguzi wa ndani wa CHADEMA kwa juu juu tu.
Sikuwa kabisa na raghba yoyote ile ya kunifanya niufuatilie kwa kina huo mchakato, hapo awali.
Jana ndo nikapata muda wa kusikiliza kidogo mjadala uliofanyika Clubhouse ambao Tundu Lissu alishiriki.
Nilifurahi zaidi nilipomsikia Bw. Lissu akikubaliana na mtazamo wangu kuhusu yale mazungumzo yao na CCM kuhusu maridhiano.
Kabla ya jana sikuwahi kumsikia Lissu akimkosoa Freeman Mbowe hadharani na kwa uwazi kiasi hicho.
Pamoja na kunifumbua masikio, huo mjadala ulizichochea fikra zangu na kupelekea kuwa na maswali mengi zaidi.
Inavyoelekea huko CHADEMA kuna mpasuko ambao ulikuwa unachemka kwa muda mrefu.
Sidhani kama kwenye miaka ya nyuma tokea Mbowe awe mwenyekiti, aliwahi kupewa changamoto kwenye hizo Chaguzi zao za ndani ya chama. Kama imewahi kutokea, mnaojua mtatujuza na kutukumbusha.
Sasa safari hii sijui ni kitu gani kilichomfanya Lissu naye kugombea hiyo nafasi ya uenyekiti wa chama.
Sijui huo uchaguzi wao utafanyika lini.
Na ukishafanyika na mshindi kujulikana, napata shida kuamini kuwa hali ndani ya chama itakuwa salama.
CHADEMA inaweza kutoka kwenye huo ikiwa ni dhoofu sana.
Atayeshindwa atakubali kuwa kashindwa kihalali na baada ya hapo atabaki kuendelea kukijenga chama?
Wakati mwingine napatwa na fikra za huenda Tundu Lissu katumia mwanya huo wa kumpa changamoto Mbowe ili aje kupata kisingizio cha kujitoa kwenye chama hapo mbeleni…
Kwa sasa tumewasikia hao wawili wakiwa hawako pamoja.
Ningependa sana kuona wanafanya mdahalo ili wapiga kura wao wapate fursa ya kuwaona wawili hao wakijinadi mbele zao.
Ila Mbowe naye…..dah. CHADEMA imesha plateau chini ya uongozi wake.
Kwa nini asijiuzulu tu awaachie na wenzie nao wakiongoze hicho chama?