Kujiuzulu siku zote ni hiyari ya mtu sio haki ya mmoja kuidai dhidi ya mwingine unless huyo .mtu hayuko timamu kichwani.Mbeba maboksi here I come with my two cents from a distance.
Nianze kwa kuwatakia heri ya Krismasi kwenu waumini wa Kristo.
Kwa wasio waumini, nanyi nawatakieni sikukuu njema na mapumziko mema.
Nimekuwa nikiifuatilia hii mijadala ya uchaguzi wa ndani wa CHADEMA kwa juu juu tu.
Sikuwa kabisa na raghba yoyote ile ya kunifanya niufuatilie kwa kina huo mchakato, hapo awali.
Jana ndo nikapata muda wa kusikiliza kidogo mjadala uliofanyika Clubhouse ambao Tundu Lissu alishiriki.
Nilifurahi zaidi nilipomsikia Bw. Lissu akikubaliana na mtazamo wangu kuhusu yale mazungumzo yao na CCM kuhusu maridhiano.
Kabla ya jana sikuwahi kumsikia Lissu akimkosoa Freeman Mbowe hadharani na kwa uwazi kiasi hicho.
Pamoja na kunifumbua masikio, huo mjadala ulizichochea fikra zangu na kupelekea kuwa na maswali mengi zaidi.
Inavyoelekea huko CHADEMA kuna mpasuko ambao ulikuwa unachemka kwa muda mrefu.
Sidhani kama kwenye miaka ya nyuma tokea Mbowe awe mwenyekiti, aliwahi kupewa changamoto kwenye hizo Chaguzi zao za ndani ya chama. Kama imewahi kutokea, mnaojua mtatujuza na kutukumbusha.
Sasa safari hii sijui ni kitu gani kilichomfanya Lissu naye kugombea hiyo nafasi ya uenyekiti wa chama.
Sijui huo uchaguzi wao utafanyika lini.
Na ukishafanyika na mshindi kujulikana, napata shida kuamini kuwa hali ndani ya chama itakuwa salama.
CHADEMA inaweza kutoka kwenye huo ikiwa ni dhoofu sana.
Atayeshindwa atakubali kuwa kashindwa kihalali na baada ya hapo atabaki kuendelea kukijenga chama?
Wakati mwingine napatwa na fikra za huenda Tundu Lissu katumia mwanya huo wa kumpa changamoto Mbowe ili aje kupata kisingizio cha kujitoa kwenye chama hapo mbeleni…
Kwa sasa tumewasikia hao wawili wakiwa hawako pamoja.
Ningependa sana kuona wanafanya mdahalo ili wapiga kura wao wapate fursa ya kuwaona wawili hao wakijinadi mbele zao.
Ila Mbowe naye…..dah. CHADEMA imesha plateau chini ya uongozi wake.
Kwa nini asijiuzulu tu awaachie na wenzie nao wakiongoze hicho chama?kum
Demokrasia inataka kura ziamue.
Lossu anajua atashindwa na ataondoka CHADEMA kwa hiyari au kufukuzwa maana makosa yake hayavumiliki.
Lissu ameamua aibomoe CHADEMA ili baada ya uchaguzi ife kwa sababu anajua wazi yeye hatakuwepo hivyo anaona kwa nini akiache chama kikiwa imara kwa Mbowe wakati naye alishiriki kukijenga bora wakose wote.
Fikiria Lissu anasema hadharani namna majadiliano ya hoja ndani ya vikao mjumbe gani alisimamia hoja pi. Tangu lini mjumbe ndani ya kikao kuunga mkono hoja tofauti na mwenzake ionekane kosa na huku nje watu wanahukumu: hapa nazungumzia Lissu kudai yeye, Msugwa, Lema; Heahe ndio walipinga maridhiano na wengine waliobakia waliounga mkono maridhiano ni wasaliti na watu huko space wanakubaliana naye! Hii inaonyesha watu wengi hawana akili ya kureason, mitazamo tofauti ya hoja ndani ya vikao halali iwe kosa la usaliti.
Hoja ya kupinga maridhiano ilishindwa kwa hoja na hiyo ndiyo nguvu ya vikao hata mwalimu Nyerere aliwahi kuwa mawazo hayapigwi rungs bali yanashindwa kwa hoja.. ina maana Lissu akishinda uenyekiti atawaburuza wajumbe waafiki mawazo yake katika kila jambo?
Hao wanaomshangilia huko space/ club house je ndivyo vkaao ndani ya vyama vinapoaswa viendeshwe yaani huku nje watu waambiwe nani alisema nini katika kikao eti kwa sababu inatakiwa uwazi?
Kwa makosa haya ya Lissu ikiwa CHADEMA watamuacha baada ya uchaguzi nitawahangaa sana ingawa ninajua Lissu ndio bye bye tena.