Fikra duni za mbeba maboksi kuhusu mustakabali wa CHADEMA baada ya uchaguzi wao.

Mbowe ninasset ya serikali na chama tawala kina nufaika na uwepo wake chadema, how and why? Yeye ndie anae keep chadema from going aggressive kwenye siasa , yeye ndie anaelimit, na katika kulimit huko chama tawala ndio kimefaidika kuliko chadema

Look at them the kwa siasa za mbowe? Wamefaidika nini?

Lissu anakuja na sera nyoofu, hi is opposite of mbowe. And chama tawala na state dont want that
Wako willing ku offer pesa yoyote mbowe akae pale

Lakini pia probably that is lissu exit strategy, probably anajua he wont make it, but atleast atapate kisingizio
 
Whether Mbowe anatetea kiti cha uenyekiti au anashindwa, tayari 👉"ameingia" kwenye kapu moja na akina Lipumba, Momose Cheyo, Dovutwa, Mzee wa Ubwaba na marehemu Augustino Mrema

Wote hawa wana kitu kimoja in common: ULAFI wa pesa.
Ameingia au alikuwepo kitambo sema nyinyi waona karibu hamkujua.

Wajanja tulijua kitambo kama jamaa ni aina ya kina Lipumba, ila tulipotaka kuwajulisha na nyinyi ili mshtuke mapema mliishia kutukejeli na kutuona wababaishaji. Bora sasa hivi mmejionea wenyewe baada ya kuonesha wazi kile mlichokuwa hamkijui kuhusu mwenyekiti wenu.

Mwanasiasa wa kweli na mwenye moyo wa kizalendo kama mchungaji Mtikila amekufa hana chawa, wala mtu wa kumsikiliza hoja zake za kupigania Tanganyika, haki nk.

Lakini muhuni fulan na mfanya biashara wa siasa ndo akawa anaonekana mkombozi hadi kupelekea kumiliki mamilioni ya chawa wakiwemo wasomi mbali mbali.
 
Kwa nini asijiuzulu tu awaachie na wenzie nao wakiongoze hicho chama?
Wazo Kuntu Sana hili ndugu yangu Nyani Ngabu, sijui, labda atalifanyia kazi hili wazo lako. Iko hivi, Kampuni inapoyumba, solution huwa ni kutoa kiongozi wake, iko vivyo hivyo kwenye timu za mipira duniani kote, hata kwenye vyama vya siasa pia humu duniani.

Ni Tanzania pekee ambapo viongozi hawana tabia ya kuachia mawazo mapya wanaposhindwa kuwapa wananchi wao kitu walicho waahidi.

Mpaka sasa sijaona mawazo yeyote tofauti kutoka kwa Mbowe ni jinsi gani ataileta katiba mpya au tume huru.. yeye kaongelea tu kwamba anataka kuwepo hapo hadi afikie miaka 68- yaani miaka 2 kabla ya ule uliotajwa kwenye biblia. Tufike mahali tuwalazimishe kikatiba hawa viongozi waachie ngazi mara baada ya miaka 10 ili waendane na katiba ya nchi. Hawawezi kujitunguia tunguia tu mambo kinyume na katiba hata kama hiki ni chama chao. Mambo yote yanatakiwa kuakisi kitu kilichomo kwenye katiba- ndio maoni yangu hayo.

Hii ingeondia kabisa hili tatizo la Mbowe na akina Cheyo na Lipumba kungangania kuendelea kuwa viongozi, na sijui ni kwa nini watu wanapenda sana kuongoza wengine au labda hawataki kuongozwa- ni control freaks?
 
Walibya walisema hivyo dhidi ya Gaddaf, Libya ipo wapi sasa!!!
Si mtetei kwa sababu hoja aliyotoa ya umri kuhalalisha kupewa tena uwenyekiti sikubaliani nayo.
Yani Mbowe unamfananisha na Gaddafi ambae asilimia kubwa ya raia wake walineemeka chini ya utawala wake japo nchi ilikuwa ndani ya vikwazo vya muda mrefu.

Legacy ya Mbowe ni ipi kwa nchi yake, chama chake au jimbo lake?

Ebu msome muona mbali mwl Nyerere mara moja, utajifunza kitu.
 

Attachments

  • Screenshot_20241216-104004.jpg
    445.8 KB · Views: 1
Sasa pata picha kama Mbowe ndo angekuwa Rais wa Tanzania…..Angefia madarakani.
Sahihi. Yaani ukimsikiliza jinsi anavyojaribu kujenga hoja ya ukomo wa uongozi, unapata shida sana kuelewa logic yake. Moral Authority ya kuwafokea CCM waachie ngazi inakosekana kabisa

Na hii sasa ndio modus operandi ya viongozi wote wa vyama vya upinzani.
 
Gaddafi ambae asilimia kubwa ya raia wake walineemeka chini ya na utawala wake japo nchi ilikuwa ndani ya vikwazo vya muda mrefu
Unanitonesha kidonda cha namna walivyokuwa wapuuzi kiasi cha kusaliti kiongozi wao!
===
Aikael ana changamoto na Lissu anachangamoto; wote hawafai kuongoza chadema!
 
Unanitonesha kidonda cha namna walivyokuwa wapuuzi kiasi cha kusaliti kiongozi wao!
===
Aikael ana changamoto na Lissu anachangamoto; wote hawafai kuongoza chadema!
Katika watu ambao karma imeanza kuwadhibu mapema sana basi ni walibya. Wakifuatiwa na wa Iraq. Jamaa ni wapumbavu sana ndomaana dunia haina tena huruma na wao.

Mtoto akililia wembe mpe tu umkate ili ujinga umtoke.
 
Mbowe akibaki madarakani CHADEMA kutawahakikishia CCM kuendelea kubaki madarakani kwa miaka mingine 50. Hii ni kwa sababu Mbowe anakwenda sasa kufanya controlled demolition ya CHADEMA ambayo ndiyo threat kuu kwa CCM.
 
Mbowe amekuwa mtu wa hovyo sana, pia CDM wajifunze kutokana na makosa ya kuchezea katiba Yao, hasa kubadilisha ukomo wa vipindi viwili tu,

Sasa matokeo yake Mbowe amekuwa kinganganizi, hataki kutoka madarakani pamoja na kwamba alishaahidi hatogombea Tena,

Chadema imekuwa mali binafsi ya familia ya Mbowe, Mungu apishie mbali tusipata Rais mwenye tabia za kilaghai kama huyu, hatokuwa na tofauti na Mugabe,
 
Lissu na Mbowe na wengineo kama wapo, fanyeni mdahalo muwaeleze wanachama wenu kuhusu sera na itikadi zenu, malengo yenu, na wapi mnakotaka kukipeleka chama katika miaka 5/10 ijayo.
Mbowe atakubali? Pengine. FYI huyu jamaa kaalikwa Clubhouse mara chungu nzima lakini anakwepa
 
Ningependa kujua zaidi kuhusu namna Mbowe anavyohusika katika utekaji wa vijana wa CDM.

Amandla...
 
Either way, chadema itapoteana. Kitakachoiokoa Chadema ni Mbowe kushindwa na aendelee kumuunga mkono aliyeshinda. Tofauti na hapo chadema itakufa kama kina TLP na .wenzake NCCR.
 
Mapinduzi gani?
 
Sasa matokeo yake Mbowe amekuwa kinganganizi, hataki kutoka madarakani pamoja na kwamba alishaahidi hatogombea Tena,
Kama Mbowe atashinda tena, come 2029 anaweza kugombea tena bila chembe ya aibu kwa kisingizio cha "kuombwa na kubembelezwa na viongozi wa dini au wazee wa chama"

Madaraka yanalevya na madaraka makubwa ya muda mrefu yanalevya zaidi, especially pale ambapo hakuna means za kuwadhibiti walafi na waroho wa madaraka
 
Yetu macho na masikini, but it’s hard to imagine how CHADEMA will emerge unscathed from this seemingly full-fledged civil war!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…