Fikra Pevu: Umewahi kumpima January Makamba katika Nafasi ya Uwaziri Mkuu?

Fikra Pevu: Umewahi kumpima January Makamba katika Nafasi ya Uwaziri Mkuu?

Sioni potential ya JM kwenye nafasi nyeti kama waziri mkuu. Alichofanikiwa ni kutengeneza mtandao, ambao hata hivo aliurithi toka kwa lowasa baada ya kuhamia chadema. Hakuna alama yoyote aliyoacha ktk nyadifa mbalimbali alizopata kushikilia. Zaidi amekuwa mzee wa madili ya kuunganisha matajiri na wawekezaji kwa viongozi wakubwa serikalini
 
Kama TISS ndiyo idara nyeti na inayowajibika kufanya maamuzi ya muhimu sana kwa niaba ya taifa la Tanzania basi inatakiwa kuwa huru bila ya kuhodhiwa na kikundi cha watu wachache. Idara hii nadhani ndiyo ambayo ingetakiwa kuthibitisha wagombea u-rais, kwa vyama vyote. Hata mapendekezo ya jina la mgombea mwenza TISS inabidi wawe makini sana, mizahaa iachwe, vivyo hivyo kwa nafasi ya Waziri Mkuu, na Baraza la Mawaziri.
 
Ifike mahali nchi iwe huru kutoka tawala za kifamilia. Sioni lolote hapa zaidi ya tawala za kifamilia jambo ambalo ni hatari sana. Tutoke huko. Wapo watu wengi tu wazuri ikiwa mamlaka zinaangalia “nchi na utaifa”.

watu walioshutumiwa na minong’ono ya uhaini na kumteta Rais aliye ofisini bado mnawapa nafasi ofisi za umma???

Uhuru wa fikra uko wapi?
 
Makamba angeweza/angekuwa PM bora kuliko Majaliwa. Majaliwa simuelewi kabisa.
 
Lowassa ndio PM pekee aliepata Nafasi hiyo akiwa Maarufu, na gharama ya hilo CCM imelipia
Haitojirudia tena
 
Ha ha ha siasa tamu sana.

Mh. January Makamba ameshawahi kuingia TOP 5 ya kuomba ridhaa ya Urais ndani ya CCM, hiyo nayo ni CV ya kufanya kazi nafasi yoyote ile.

All and all MAMLAKA HUTOKA MBINGUNI KWA BWANA.

#YetzerHaTov
#NchiKwanza
#KaziIendelee
#ChanjoNiBoraKulikoTiba
Augustino Mrema aligombea kabisa. Lipumba aligombea kabisa. Kuna yule mama aliyechaguliwa kuwa RC aligombea kabisa. Kufika kwenye top 5 siyo kigezo hata kidogo.
 
Si kila lisemwalo lazima liwe ila kila liwalo lazima lilisemwa!

Unamfikiria vipi mtu senior kama Makamba kupata nafasi ya Uwaziri Mkuu?

Sifa zake kuu ni zipi? Umahiri na udhaifu wake kwa Nafasi hiyo ni upi?

Keep in mind ni uzi tu wa kumfikiria JM katika nafasi hiyo na ikitokea lolote ichukuliwe ni coincidence tu
Nionavyo

Sisi hatuna shida kubwa sana ya kuwa na watu mahiri wa kuchambua mambo. Shida kubwa ya watanzania ni kukosa uungwana ama utu. Bahati mbaya suala hili halipimwi kirahisi sana. Aidha, kwa kukosa huo uungwana au utu, ndipo watu waliokabidhiwa fursa za kututafutia viongozi(vetting) hututenda pakubwa. Kwahiyo, JM huenda anavutia kwa baadhi ya watu, lakini kipengele cha uungwana na utu , anaweza asiwe bora sana. Bahati mbaya huu ni ugonjwa wa wengi wetu, si yeye pekee. Ni matokeo ya mafundisho kama si utamaduni.
 
Shida kubwa kabisa ya January ni hii kutumia watu wake wa mtandaoni kumuimbia maapambio na kumtukuza.
Hilo kweli analiweza, ana vijana kila kona kwa shughuli hiyo.
Naona hadi dada wa USA alimtumia na bado anamtumia.
January nina uhakika hutakuja kufanikiwa.
 
Yaani JM wanamuona watu yuko smart amavyoongea ila kwa taarifa yenu huyo mi empty set hana utendaji wowote kabebwa tu na mazingira ya baba yake kuwa kwenye system! Maneno mengi vitendo sifuri!
Bingwa wa mipasho na vibonzo vyakukebehi viongozi, tamaa zaidi ya fisi wenye mabaka!
ukawa era.jpg
 
Shida kubwa kabisa ya January ni hii kutumia watu wake wa mtandaoni kumuimbia maapambio na kumtukuza.
Hilo kweli analiweza, ana vijana kila kona kwa shughuli hiyo.
Naona hadi dada wa USA alimtumia na bado anamtumia.
January nina uhakika hutakuja kufanikiwa.
ukawa era.jpg
 
Nikiangalia ushabiki wake wa mambo ya mpira (namna anavyoshabikia kitoto) na ile sheria mbovu ya mawasiliano, namuona mtu wa kawaida sana, I mean the very average Joe
Mambo ya ushabiki was mpira usiyaingize kweneye vitu vya maana.. Siku zote mazungumzo ya mpira kama hiz timu zetu simba na Yanga yapo kimatani zaidi.. So acha kumuhukumu kwa hilo, jamaa you very bright na anadeserve kushika hyo nafasi
 
Si kila lisemwalo lazima liwe ila kila liwalo lazima lilisemwa!

Unamfikiria vipi mtu senior kama Makamba kupata nafasi ya Uwaziri Mkuu?

Sifa zake kuu ni zipi? Umahiri na udhaifu wake kwa Nafasi hiyo ni upi?

Keep in mind ni uzi tu wa kumfikiria JM katika nafasi hiyo na ikitokea lolote ichukuliwe ni coincidence tu
Jm ni mediocre
 
Si kila lisemwalo lazima liwe ila kila liwalo lazima lilisemwa!

Unamfikiria vipi mtu senior kama Makamba kupata nafasi ya Uwaziri Mkuu?...
Muislamu hawezi kupewa tena.
Hata 2025 muislam siyo , hawezi pewa.
Hii nchi CCM wanajua ni kubadilishana Dini.
 
Si kila lisemwalo lazima liwe ila kila liwalo lazima lilisemwa!

Unamfikiria vipi mtu senior kama Makamba kupata nafasi ya Uwaziri Mkuu?...
Nadhani anatosha maana hata katika mbio za urais alifika top 5.

Japo mimi namtazama zaidi katika nafasi ya waziri wa mambo ya Nje kulingana na ndoto zake
 
Back
Top Bottom