Mwizukulu mgikuru
JF-Expert Member
- Oct 21, 2021
- 5,715
- 13,739
Jana nilikuwa napiga story na mama yangu mzazi. Katikati ya mazungumzo yetu, aliniambia kwamba laiti kama yeye angekuwa mwanaume, basi asingeoa. Badala yake, angezaa tu na wanawake tofauti ili apate watoto na maisha yaendelee. Bi mkubwa wangu huyu yupo kwenye miaka 65 sasa.
Ninachoamini mimi ni kwamba huwezi kuwa na heshima katika jamii yetu ya Kiafrika mpaka uwe na familia. Hata uongozi wa juu serikalini, kama urais, hauwezi kupewa mpaka wahakikishe kwamba una mke. Pia, sidhani kama unaweza kuishi kwa uchamungu kama unaishi kiholela. Naamini ukiwa na mke ni tiketi kubwa ya kumcha Mungu, kwani kuna asilimia chache sana za kuwa mzinifu ukiwa katika ndoa.
Sasa, bi mkubwa wangu anawaza nini? 😎 Au ndio anataka kunithibitishia kuwa ni kweli motoni wamejaa wanawake?