Filamu ya Royal Tour Ingezinduliwa Tanzania Badala ya Marekani kuepuka gharama

Tunaambiwa kwamba filamu ya Royal Tour yenye kupromote Utalii imegharimu Shilingi za Kitanzania Bilioni tisa. (9).

Leo tunaambiwa Rais ana safari ya kikazi yeye na delegation yake marekani na moja wapo ya mambo atayoyafanya ni kuzindua filamu ya Roya Tour.

Kwakua hizo kazi nyingine atazofanya hatujaambiwa ni zipi hivyo main task inakuwa ni Kuzindua filamu yake.

Ukiachana na matumizi ya Bilioni Tisa kwenye maandalizi ya filamu bado tunatumia tena mapesa mengine kwenye Uzinduzi na badala ya kuufanya hapa nyumbani tunaufanyia Marekani.

Matumizi ya mapesa haya yanafanyika kipindi tukiwa kwenye wave ya Corona maana tumeambiwa ipo na Vita Vya Ukraine.

Ukiachana na uwepo wa korona na vita ya Ukraine , Uchumi wetu umekumbwa na pigo la kupanda kwa bei za bidhaa muhimu jambo linaloongeza ukali wa Maisha kwa wananchi wa kawaida.

Inaleta ukakasi wa matumizi ya aina hii ya mapesa wakati Taifa likipitia kipindi kigumu namna hii.

Sijui viongozi wetu wanafikiria nini ila haipendezi kuzindua Filamu huko ughaibuni kwa mapesa mengi wakati kuna mtanzania hapa hata mlo wake tu unakua wa kuvizia na wakati juzi tu hapa Waziri Ummy anatuletea takwimu kwamba bado kuna idadi ya watanzania wanaojisaidia maporini(hawana vyoo)

Ningeiomba tu Serikali ijaribu kubana matumizi hasa kipindi hiki badala ya kuendelea kutumia fedha ambazo hatuna kwa mambo ambayo yanaonekana kabisa yasingefaa kufanyika kwa kipindi hiki.

Vile vile timing ya uzinduzi nayo sio nzuri maana jumuia za kimataifa zinahangaika na vita vya Urusi na Ukraine hivyo mwamko wa filamu hiyo utakua mdogo.

Wangesubiri mambo yatulie kidogo kama kweli tunataka kuipromote hiyo video.

Asanteni.

On top of that,

Uzinduzi unafanyika Marekani kuvutia watalii wakati Taifa la Marekani limekataza Raia wake kuja Tanzania kutokana na uwepo wa Korona.

View attachment 2186609
Kuzinduliwa marekani inaweza isiwe shida.Ila nakubaliana na wewe kuwa ni wrong timing lakini inawezekana labda ingesubiri muda mrefu kuzinduliwa ingeweza kukosa mvuto.Cha msingj hapi ni kubana matumizi kwa kupunguza delegation zake kama alioenda nae UAE.
 
Filamu ya james bond imesubiri kama miaka minne toka kutengenezwa mpaka kuja kuwa released kutokana na corona hivyo kusema ikisubiri sana itakosa mvuto hiyo sio hoja.

Ni tatizo pia kuizindua marekani maana bado katika website yao marekani hawajatuondoa katika nchi ambazo hazifai kutembelewa.

Wanasema tuna kiwango kikubwa cha uhalifu, korona, ugaidi na hatuzingatii haki za mashoga.

Swala la gharama pia ni muhimu kulitazama haifai kwa nchi maskini kama yetu kutumia mapesa kwenda kuzindua filamu huko Ulaya.

Matumizi mabaya ya fedha kwa kweli.

Uzinduzi huu ungekua na tija huko marekani kama wangetuondoa kwenye hiyo website yao maana wamarekani wanaheshimu sana serikali yao.

Wanaogopa sana maswala ya ugaidi na uhalifu. Mpaka tutakapoondolewa kwenye hiyo website naona kama marekani sio chaguo sahihi la kuzinduliwa hiyo filamu kwa vigezo lukuki.
 
Ss watalii tunaowatafuta wako hapa Bongo au nje?!

Ama common sense is not so common
 
Sasa hivi sio wakati wa kuokoa gharama🐒

View attachment 2186561
Mwendazake hakuwahi kuokoa gharama hata siku moja
Yeye na kikosi chake walifuja sana hela za nchi hii
Alimweka hazina mpwa wake na akawa anajibebea manoti atakavyo hadi anagawa ovyo barabarani...
Alikuwa anaogopa kwenda ulaya sababu ya udhaifu wake kwenye mawasiliano ya lugha ya english.
 
Tunaambiwa kwamba filamu ya Royal Tour yenye kupromote Utalii imegharimu Shilingi za Kitanzania Bilioni tisa. (9).

Leo tunaambiwa Rais ana safari ya kikazi yeye na delegation yake marekani na moja wapo ya mambo atayoyafanya ni kuzindua filamu ya Roya Tour.

Kwakua hizo kazi nyingine atazofanya hatujaambiwa ni zipi hivyo main task inakuwa ni Kuzindua filamu yake.

Ukiachana na matumizi ya Bilioni Tisa kwenye maandalizi ya filamu bado tunatumia tena mapesa mengine kwenye Uzinduzi na badala ya kuufanya hapa nyumbani tunaufanyia Marekani.

Matumizi ya mapesa haya yanafanyika kipindi tukiwa kwenye wave ya Corona maana tumeambiwa ipo na Vita Vya Ukraine.

Ukiachana na uwepo wa korona na vita ya Ukraine , Uchumi wetu umekumbwa na pigo la kupanda kwa bei za bidhaa muhimu jambo linaloongeza ukali wa Maisha kwa wananchi wa kawaida.

Inaleta ukakasi wa matumizi ya aina hii ya mapesa wakati Taifa likipitia kipindi kigumu namna hii.

Sijui viongozi wetu wanafikiria nini ila haipendezi kuzindua Filamu huko ughaibuni kwa mapesa mengi wakati kuna mtanzania hapa hata mlo wake tu unakua wa kuvizia na wakati juzi tu hapa Waziri Ummy anatuletea takwimu kwamba bado kuna idadi ya watanzania wanaojisaidia maporini(hawana vyoo)

Ningeiomba tu Serikali ijaribu kubana matumizi hasa kipindi hiki badala ya kuendelea kutumia fedha ambazo hatuna kwa mambo ambayo yanaonekana kabisa yasingefaa kufanyika kwa kipindi hiki.

Vile vile timing ya uzinduzi nayo sio nzuri maana jumuia za kimataifa zinahangaika na vita vya Urusi na Ukraine hivyo mwamko wa filamu hiyo utakua mdogo.

Wangesubiri mambo yatulie kidogo kama kweli tunataka kuipromote hiyo video.

Asanteni.

On top of that,

Uzinduzi unafanyika Marekani kuvutia watalii wakati Taifa la Marekani limekataza Raia wake kuja Tanzania kutokana na uwepo wa Korona.

View attachment 2186609

Usinduzi ni kote kote,afu kumbuka gharama za filamu hazilipiwi na Serikali
 
Gharama za safari analipia nani??
State visit analipiaga nani?

Screenshot_20220414-145738.png
 
Ss watalii tunaowatafuta wako hapa Bongo au nje?!

Ama common sense is not so common
Hii ni dunia ya utandawazi hatufungwi na mipaka halisia tena.

Tunaweza zindua hapa na kufikia malengo yetu vile vile.

Ndio maana kuna uwezekano msanii wa marekani akawa maarufu hapa bila hata kufika hapa Tanzania.

Kikubwa na ubora na umuhimu wa jambo lenyewe.
 
State visit analipiaga nani?

View attachment 2187928
Screenshot_20220413-232427.png

Rais amwambie Kamala aondoe damaging information kwenye website ya Embassy yao au la safari itakua haina tija.

Bado Tangazo hilo ni valid as we speak na kwakua wazungu huwa wanasikiliza sana ushauri wa taasisi zao hakuna atayerisk kuja eneo lenye ugaidi, uhalifu na korona.
 
View attachment 2187929

Wazungu hawajaanza leo uzushi wao,ndio maana Rais kaenda huko kwao na atakutana na watu mbalimbali na atawaambia hakuna kitu kama hicho..

Wewe unaona hayo waliyoongea hapo juu yapo?
 
Mapesa meengi yameungua ila kwakweli sidhani kama tutafanikiwa kwa lolote.

Filamu inazinduliwa kwa ajili ya utalii wakati walengwa wenyewe mamefocus kwenye vita muda huu.

Pia inashangaza tunasema kuna korona halafu tunatengeneza video na kuizindua wakati wa korona.
Kwa hiyo Marekani hawafanyi kazi sasa hivi, wanahangaika na vita ya Ukraine? We jamaa ni chizi, hivi hujui huko Russia maisha yanaendelea kama kawaida wala vita hawana habari nao, wanaohangaika navyo ni wanajeshi wao tu walioko Ukraine?
 
Wazungu hawajaanza leo uzushi wao,ndio maana Rais kaenda huko kwao na atakutana na watu mbalimbali na atawaambia hakuna kitu kama hicho..
Sasa unategemea vipi watu wanaoishi kwa uzushi??

Sidhani kama wataondoa kiurahisi namna hiyo.

Hao watu sio watu wazuri in the first place na ni vyema this administration ifahamu mapema kabisa kuwa hatupaswi kuwa nao karibu sana.

Hakuna aliyesalimika kwa kuwa karibu nao.
 
Mwendazake hakuwahi kuokoa gharama hata siku moja
Yeye na kikosi chake walifuja sana hela za nchi hii
Alimweka hazina mpwa wake na akawa anajibebea manoti atakavyo hadi anagawa ovyo barabarani...
Alikuwa anaogopa kwenda ulaya sababu ya udhaifu wake kwenye mawasiliano ya lugha ya english.
Sawa muda utatuambia tu kuwa was the worst or the best president. Bila shaka sasa tumeshaanza kuona dalili. Tuendelee kulamba asali. Nchi imefunguliwa.
 
Kwa hiyo Marekani hawafanyi kazi sasa hivi, wanahangaika na vita ya Ukraine? We jamaa ni chizi, hivi hujui huko Russia maisha yanaendelea kama kawaida wala vita hawana habari nao, wanaohangaika navyo ni wanajeshi wao tu walioko Ukraine?
Chizi ni wewe usiyefahamu kwamba ni jambo gani kwa sasa linalopata media attention.
 
Sasa unategemea vipi watu wanaoishi kwa uzushi??

Sidhani kama wataondoa kiurahisi namna hiyo.

Hao watu sio watu wazuri in the first place na ni vyema this administration ifahamu mapema kabisa kuwa hatupaswi kuwa nao karibu sana.

Hakuna aliyesalimika kwa kuwa karibu nao.
Hata wasipoondoa kikubwa hawajazuia raia wao kuja ila wamewapa tahadhari..

Pili tunawategemeaje? Hapo tumeenda kutangaza soko la utalii kwao na kuwaonyesha fursa zaidi za biashara..

US ndio investors no.1 Tzn ila kwenye watalii namba yao ni ndogo Sana.
 
kubana matumizi ya serikali ni jambo la msingi sana, ukiruhusu hela zitumbuliwe tu kisa unaziingiza zingine sio kweli hakuna biashara ya hivyo. Kuna mahali lazima tujisahihishe
Sishabikii hiyo Royal tour, Ila kuvutia wanunuzi wa bidhaa na huduma zako unahitaji uwekezaji mzuri. Mnunuzi hakufati, na akikufuata 1 ujue Kuna wanunuzi 9 wameishia njiani. Mnunuzi wa utalii ni American, Eropeans na kiasi Asians yalupasa uwapelekee packages hukohuko. Njaa ipo Moyale na Wajir wewe na mpunga wako unautangazia Madibira na Rujewa huo ni wendawazimu.

Kwenye suala la kutokuja Tanzania, watu wengi wamefunguka akili (wameshajua coronavirus haiondoki). Mpaka juzi hapa nilikuwa na volunteers wa marekani wanakuja hapahapa bongo Pamoja na hizo warning.
 
Kikwete hajawahi kuacha kusafiri wala kubana matumizi.

Kivuli hufanana ma mwenye kivuli.
Hawa watu wasifikiri kwa ukomo wa nyadhifa na vile wanavyohudumiwa na serikali.Watufikiriye zaidi sisi watanzania wa kipato cha buku huku mtaani.
 
State visit analipiaga nani?

View attachment 2187928
Wananchi wanapaswa kujua sasa ni nani anamlipia Rais wetu safari ya wiki mbili marekani ili tupunguze kelele.

Ni kodi zetu au hao waliotengeneza filamu?

Kama ni kodi zetu that is a bad investment.

Kama ni aliyetengeneza filamu wananchi wanapaswa kujua aliyegharamia utengenezwaji huo na safari hiyo.
 
Back
Top Bottom